nimekuwa nikijiuliza kwa nini simu za mkononi zinahitaji minara mingi tofauti na ile ya redio.karibu maeneo mengi yana minara ya simu lakini minara ya redio sijawahi kuiona huku mitaani lakini bado redio hizo zinasikika karibu maeneo yote. pia nafahamu kuwa redio na simu zote zinatumia electromagnetic waves sasa nini kinasababisha tofauti hii?
Niliwai kujiuliza maswali kama haya na kusoma article na kitabu vilinifafanulia vizuri sana
Ila ngoja nijaribu kueleza kuona kama nilikariri au kuelewa yale niliyoyasoma . teh teh teh teh. Watalama watanikosoa.
Ni hivi
Kimsingi simu ni kama radio kama ulivyosema lakini tofauti yake na radio ni kuwa Radio zimetengenezwa kupokea tu matangazo.(google maneno kama
broadcast,
Muliticast,
unicast uelewe zaidi ) Wakati simu za mkononi zinapokea na zinatakiwa kuwa kuwa uwezo wa kurusha matangazo. Kwa hiyo simu zina
transmiiter japo transmiister za kwenye simu uwezo wake ni mdogo sana hivyo kuhitaji retramsiiter ambayo ndio hiyo minara
Kwa lugha nyepesi unaweza kusema kila simu ni kama kituo cha radio lakini transimmiter za kwenye simu za mkononi hazina uwezo(
power) kurusha matangazo na hivyo kuhitaji uwepo wa mnara maeneo ya karibu. Ndiyo maana simu zinahitaji kuwa na minara karibu tofauti na radio sabbau radio kazi yake ni kupokea tu wakati simu ili iwe na maana inatakiwa kuwa na uwezo kupokea na kupiga ( transmit).
Sasa power ya simu binasfi haitoshi kurusha mawimbi kutoka kwa mpigaji mpaka kwa mpokeaji bila kupitia kituo fulani( Mnara) na hivyo hivyo power ya reciver kwa mpokeaji haina nguvu ya kumfanya mtu apokee pokea mawasilino bila kupitia kwenye re transmiiter ya karibu(Mnara)
Vile vile kuna uhaba wa frequency.au Masafa.
Mahitaji ya masafa ni makubwa sana kuliko uwezo uliopo. Imebidi zitumiwe mbinu za kuwezesha kitu kinaitwa
frequency re use. Kwa hiyo kampuni za simu zinatenga mji katika
Cell mbali mbali . kila cell inaweza kutumia frequency fulani
. Frequncy iliyotumika inaweza kutumika tena na kituo cha mbali kidogo.
Mfano Cell au mnara wa tigo kijitonyama unaweza kutumia frequency/ masafa ya x then mnara wao Posta ukatumia frequency Y na mnra wa Uwanja wa ndege ukatumia tena frequency X na mnara wa mbagala ukatumia tena frequency Y. Hii inawawezesha kutumia frequency ndogo waliyopewa kuwahudumia wateja wengi.
Hope nimejaribu nikipata ile link ya kitabu na article nilizosma nita kudondoshea hapa.