Kukosa kupata ujauzito kunasababishwa na vitu vingi da angu, 40% huwa inachangiwa na mke mwenyewe na 40% inatokana na mume na 20% inachangiwa na wanandoa wote kwa pamoja. Mume: wakati wa tendo la kujamiana mume lazima awe na uwezo wa kutoa mbegu nyingi (si chini ya 20mil) kwa mkupuo mmoja kwenye majimaji yanayotosha kuziwezesha mbegu kuogelea kwa nafani kuelekea yai lililopeku liliko. Pia mbegu hizo lazima ziwe zimekomaa, zenye umbo halisi (kichwa kikubwa na mkia mmoja mrefu). Hivyo, mumeo nae anaweza kuwa kikwazo akikosa sifa hizi. Mshauri mumeo asivae nguo na chupi za kubana sana ili kuruhusu sperms nyingi zitengenezwe (spamatogenesis), pia mwambie mumeo asitombe kila siku kila mara ili kuruhusu mbegu zake zipate muda wa kukomaa na kuwa nyingi siku ya kujamiana na wewe siku ya 12-15 tangu MP yako ianze (sio kwisha). Ajiepushe kukaa ama kuoga maji ya moto sana kwenye mapumbu. apunguze unene kama anao na kutibu vidonga vya tumbo, kisukari na presha kama anavyo pia. Muulize kama ameshawahi kuugua gono, kaswende ama pangusa huko nyuma. Mke: Chunguza kama mayai yako yanakomaa (ovulation), na mirija iko wazi. Pia kumbuka kama umeshawahi kutoa mimba kwa njia ya kukwangua (D&C) zaidi ya maramoja na kuendeleA HUENDA uterus yako imepata shida. Punguza unene, hasira na kazi nyingi sana. weka mto matakoni ili utengeneze slope ya spams kuelekea kwenye mayai, endelea kulala chali baada ya mume kuweka mbegu zake. Pia..