Elections 2010 Kwa nini Sitta asiuteme wadhifa wake wa uwaziri akahamia CHADEMA?

Elections 2010 Kwa nini Sitta asiuteme wadhifa wake wa uwaziri akahamia CHADEMA?

kwanza sitta anastahili kushtakiwa kwa matumizi mabaya ya pesa za serikali, ilikuwaje ajenge ofisi kubwa ya spika jimboni kwake urambo??? kwani huko ndiko makao ya spika au makao ya mbunge wa urambo?? ina maana alifikiri angekuwa spika milele?hatatoka wala kufa?? ina maana sasa anna makinda nae akajenge ofisi jimboni kwake njombe? na ikitokea makinda akatoka akaja spika mwingine toka lindi nae akajengewe ofisi jimboni kwake??

taarifa ngapi dhidi ya sitta za matumizi mabaya ya fedha za ofisi, mahusiano yake ya hovyo na wanawake? aargh, wote wachumia matumbo tu.

huyu sitta ni mpambanaji kweli ila ni mpambanaji wa masuala yake na tumbo lake na pia yale ambayo aninterest nayo tu, hana lolote, ni mnafiki mkubwa, mbona amekubali kunyamazishwa ndani ya CCM? si angetoka kama alivyotoka mpendazoe?? binafsi naamini walioko CCM ni wanafiki wakubwa na hawana lolote la kutaka kuleta maendeleo ya kweli nchi hii
 
Ningependa kumuona mpiganaji samuel 6 akijiuzuru uwaziri afu akakitema chama cha mafisadi(ccm) na kujiunga chadema ili aongeze nguvu maana mwaka 2015 tunajiandaa kuchukua nchi tukiwa na watu makini na wenye uchungu na nchi kama kina sitta na wengine kama mp george simbachawene( mbunge wa kibakwe)?

Naomba maoni

huyo unamfahamu??
 
6 ana sura 2, ni fisadi na mpambanaji vilevile. Nadhani walimwengua kwenye ulaji sehemu. Kajenga ofisi ya mamilioni kwao, angejenga hospitali au hizo pesa angenunua madawati kwenye shule ningemwelewa.
 
Tatizo la huyu jamaa ni kigeugeu na mnafiki mkubwa.Watu wa namna hii hawahitajiki CHADEMA!!
 
Bado anafaa kwa sababu bila sita kuachia hoja binafsi bungeni mambo yangekuwa kimyaaaaaaaaaaa mpaka leo.
 
Huwezi kutaja wapiganaji wa nchi hii bila kumtaja Samwel Sitta. Huyu ni mzalendo wa kweli, acha kusikiliza porojo za mafisadi kuhusu huyu mwamba. Alipigana akiwa Spika wa Bunge na sasa anaendelea kupigana akiwa ndani ya serikali ya JK ingawa wamemuingiza humo kinafikinafiki tu.[/
QUOTE]

Wewe una akili haya yote tunayo hangaika nayo yameibuka ndani ya uongozi wake. Kama angeamua kuminya issues angeminya kama waliomtangulia. Unaposema sasa hivi angalia wapi chanzo cha unachokisema. Na kama ujuavyo bila kuvunga vunga ndani ya CCm unapotea yaani una dead bila hata kuwaeleza wananchi lengo lako. WE jiunge na CCM alafu uropoke uje uone cha moto. Weeeeeeeeeee. Mwaya 6 jiunge na unapopaona panafaa ili ueleze maovu la sivyo hukohuko ndani wata ku equalize
 
Hana lolote,mlafi tu na mtu wa kuweka maslahi yake na chuki zake binafsi mbele? si tayari yupo Shibuda wa kuharibu,mnatafuta na mwingine....kama mwanaume sana asingekubali kuapishwa.........sioni ataongeza nini,abaki huko alipo.
 
Maoni ya kichochezi hayampendi rais wetu ajaye kupitia ccm yaani sita
 
Rais wa jamhuri ya muungano wa tz samuel sitta 2015 - 2020
 
Ningependa kumuona mpiganaji samuel 6 akijiuzuru uwaziri afu akakitema chama cha mafisadi(ccm) na kujiunga chadema ili aongeze nguvu maana mwaka 2015 tunajiandaa kuchukua nchi tukiwa na watu makini na wenye uchungu na nchi kama kina sitta na wengineo kama mp george simbachawene( mbunge wa kibakwe)?

Naomba maoni

kwa maoni yangu tunahitaji wapiganaji kama Sita, Mwakyembe, na wengine wengi kwa ujasiri wao bila kujali wapo katika bus gani kwani ni ukweli usiopingika kwamba hata katika CDM NA CUF KUNA WASALITI WA WANANCHI SOTE TUMEWAONA SWALA NI KUPATA WATU WENYE NIA YA DHATI KUTUTETEA.
 
jamani hamna mtu anayeweza kujenga ofisi bila ya kufuata sheria zilizopo nina uhakika yuko entitled to get office at his constituent with the same quality as at the Parliament at his capacity at that time i.e. Speaker! La sivyo mafisadi wangemlipua!
 
Ningependa kumuona mpiganaji samuel 6 akijiuzuru uwaziri afu akakitema chama cha mafisadi(ccm) na kujiunga chadema ili aongeze nguvu maana mwaka 2015 tunajiandaa kuchukua nchi tukiwa na watu makini na wenye uchungu na nchi kama kina sitta na wengineo kama mp george simbachawene( mbunge wa kibakwe)?

Naomba maoni

Miye kwa maoni yangu abaki humo humo ndani ili aendelee kuipa wakati mgumu/kuichachafya Serikali kutokana na ufisadi wake. Yeye, Mwakyembe na Mawaziri wengine wenye kupenda maslahi ya nchi yetu wakisimama imara basi wanaweza kabisa kuisambaratisha Serikali iliyojaa ufisadi wa hali ya juu.

 
Hey felw great thinkers, Mimi sina shda na uwepo wa 6 na wapambanaj wengne ndan ya ccm na tena hawatakiw kutoka huko,we hv to ask our selves whts our aims? We want to bring discipline and equal distribution of resources no mater wch part does so.lakn pia siku zote tutatue tatzo na sio kukimbia tatzo hiyo ni ishara ya uoga na kushndwa,swal tujiulze je kesho CDM wakiingia wachaf tuondoke na kuanzsha chama kingine jib ni hapana tutapigana na kuwaondoa wachaf.
 
Sioni haya ya 6 kujiunga na Chadema....angekuwa na uchungu wa kweli wala asingekuwa CCM leo.
 
Hey felw great thinkers, Mimi sina shda na uwepo wa 6 na wapambanaj wengne ndan ya ccm na tena hawatakiw kutoka huko,we hv to ask our selves whts our aims? We want to bring discipline and equal distribution of resources no mater wch part does so.lakn pia siku zote tutatue tatzo na sio kukimbia tatzo hiyo ni ishara ya uoga na kushndwa,swal tujiulze je kesho CDM wakiingia wachaf tuondoke na kuanzsha chama kingine jib ni hapana tutapigana na kuwaondoa wachaf.

Nakupa five mkuu. Very well presented. Mwache six abaki huko huko, tunahitaji wazalendo wakweli kwenye kila chama ili tuweze kusukuma gurudumu la maendeleo mbele. Mind you, constructive criticism is always good, inafanya mtu afikiri kabla ya kutenda. That being said, tukiwa nawapenda maendeleo kwenye kila chama Kutakuwa na mashindano ya kuiendeleza Tanzania na sio kuiibia Tanzania.
 
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Nakubaliana na mapungufu aliyonayo sita lakini ukilinganisha na ra, el, jk, bm, nk wa ccm he become saint! Sita might be the very person we need! Kama angekuwa sawa nao kwa nini wamemsakama na kumfanyia hila za waziwazi...............mwenye akili afikiri!
 
Back
Top Bottom