Kwa nini "ss" au "tt" ?

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Kwa nini watu wengi wanaandika majina yao kwa kutumia herufi mbili kwa mf. Zitto na Sio Zito, ao Wassira na Wasira? hiyo "ss" au "tt" inatamkwaje? kwa maana "s" au "t" inaeleweka inavyotamkwa, sasa zikiwa mbili inakuwaje, na ni lugha ghani inatumika kutamka hizo tt au ss mbili?
 
Hebbu tuwaulize wenye majjina hhayo wattatuambia
 
Mambo ya secondary hayo, chezea kidhungu wewe
 
Ipo tofauti ya ziTTo na ziTo ,ya kwanza utaitamka kwa kukazia mfano wa lahaja wazitumiazo ndugu zetu wa kisukuma na kinyamwezi katika matamshi yao ziTTO itatamkwa kwa mkazo kama " wakati ya pili zito itakuwa "ziTOH"
WaSSira itatamkwa kama "waZSira"
 
Ipo tofauti ya ziTTo na ziTo ,ya kwanza utaitamka kwa kukazia mfano wa lahaja wazitumiazo ndugu zetu wa kisukuma na kinyamwezi katika matamshi yao ziTTO itatamkwa kwa mkazo kama " wakati ya pili zito itakuwa "ziTOH"
WaSSira itatamkwa kama "waZSira"

Hiyo ni lugha Gani?

 
Kwani unafikiri ZITTO au WASSIRA ni kiswahili?nimekufafanulia matamshi ya kibantu tu!

Ndio maana nakuuliza hiyo Ni Lugha Gani hiyo uliyotumia kuelezea? kwani Kiswahili chetu ni Kibantu kwa 100% sasa ndio maana nashindwa kuelewa umetumia lugha gani kuelezea, kwani kwenye kibantu hakuna neno lolote linalo andikwa kwa tt au ss kuna t au s moja tu, ila unaweza kuaandika kwa mf.titi au sisi, labda hivyo, ambapo inapoteza maana, lakini kwenye maneno yote ya Kibantu lazima kuwe na silabi yaani a,e,i,o,u baada ya herufi!

 
Hapana kiswahili si kibantu asilimia mia,mfano maneno machache ya mwanzo ya hoja yako(maana-ma'anah ,lugha-lughat,kiswahili-suahel asili-asli)yamekopwa kutoka lughat l'arabiya.tuna maneno ya kilatini (meza ,sabuni,bendera)kiingereza mifano unayo,kihindi ,kichinaalimradi kiswahili si 100%kibantu.
Nikirudi kwenye hoja ya msingi nimekusaidia jinsi ya kutamka tu !hebu katembelee maeneo ya usukumani halafu jaribu kusikiliza matamshi yao then attempt kuyaweka katika maandishi hapo ndipo utanielewa namaanisha nini.
 

Unachanganya vitu viwili Lugha na maneno ya kuazima, Kiswahili ni Kibantu kwa 100% ila kimeazima maneno mengi kutoka Lugha nyingine na Lugha zote Duniani zimefanya hivyo, kwa mf. kiingereza zaidi ya asilimia 60% ya maneno yake ni ya kilatini, lakini hakiitwi Kilatini bali ni kiingereza na ni lugha 2 tofauti kabisa au kijapani nusu nzima ya maneno ni ya Kichina lkn ni Lugha mbili Tofauti!

Hakuna kitu kama hicho Lugha haindikwi unavotamka, kuna Biblia zilizoandikwa kisukuma, au Kichaga au sijui Kihaya na hamna kitu kama Hicho hakuna mahali ambapo kuna tt kwa wakati mmoja au ss au ll ktk Kibantu hatuna huo Mfumo, ni hivyo tu!

Ila unaweza ukaandika neno lenye silabi mbili kwa mf. aa oo ee ii hapo sawa lkn sio herufi tu, kwa kifupi ni kwamba ktk Kiswahili au Kibantu hatuna neno ambalo linaishia tu na kwa mfano t bila ya silabi, m au n au s au herufi yoyote ile, na ndio maana Watz wengi wakiongea Kiingereza wanasema goingi badada ya going, au schooli badala ya school au plastiki badala ya plastic, Hoteli badala ya hotel na hilo tatizo ni kwa Wabantu woote awe Muhaye, Msukuma au Mgogo...



 
sasa mbona unakinzana na hoja yako mwenyewe? kama unasema kiingireza 60% kimekopa maneno kutoka lugha nyingine na bado kinaitwa kiingereza kwanini unakataa kuwa kiswahili pia si 100% kibantu?
JApokuwa nashawishika kwa namana fulani kukubaliana na wewe kwenye paragrafu yako ya mwisho,nafikiri ni wakati mzuri sasa tuwakaribishe wadau wengine watuweke sawa ila namaliza kwa kukazia tena ,sikumaanisha ufasaha wa maandishi bali utatamka vipi ziTTo na ziTo au waSSira na waSira!
 


Sijui sehemu nyingine lakini kwa mtu anaekuja au kuishi Marekani, kuna kanuni za kusoma maneno.

Tuanze na vowels: a, e, i, o, u. ukizisoma hizi vowels kiswahili basi unazitamka kama zilivyo. Hizo zinaitwa "hard vowels" Lakini ukizisoma kizungu basi unazitamka ei, i, ai, o, yu (au soft vowels).

Kanuni za kutamka maneno za kimarekani (American english) ni kuwa vowel ikifuatiwa na consonant moja basi hiyo vowel itakuwa soft-vowel. Kwa hiyo ZITO itatamkwa ZAITO na WASIRA itatamkwa WEISIRA. Ukitaka mmarekani amuite Zito kama sisi watanzania tunavyomuita basi andika jina lake Zitto, na Wasira liandike Wassira.

Maoni yangu.
Mara nyingi lugha zinaingiliana na majina ya watu wengi yamerekebishwa kulingana na nani unawasiliana nae. Kwa mfano, ukitaka Mjerumani aiite TANZANIA kama tunavyoiita sisi basi uianndike TANSANIA. Ukisisitiza kuiandika TANZANIA basi mjerumani atasema TANTSANIA kwa sababu katika kijerumani S yetu inatamkwa Z, na Z yetu inatamkwa TS.

Ukienda Uganda mambo ni mengine. Majina mengi yana Ss na hayahusiani kabisa na soft au hard vowels.
 

Kama sababu ni kumfanya Mzungu aweze kutamka, nijuavyo mimi Wazungu hawana shida, ukiwaambia jina lako linavyotamkwa watalitamka hivyo hivyo unavyotaka wewe, kuna mifano mingi tu ya Watu wenye majina yasiyo ya kimarekani na yanatamkwa kama wenye Majina wanavyotaka kwa mfano kuna akina Talib Kweli, Kanye, akina Mohamed Ali, Dikembe Mutombo, Jakaya Kikwete, Mkapa, Mizengo Pinda,Nyerere, Mobutu, Thabo Mbeki, Mandela, Zuma, Mugabe, Kwame, au Wachina, Wajapan au Wakorea na Wahindi kama akina Gadhi, hao wote mbona hawajabdailisha ili Wamarekani waweze kutamka?
 

Point well taken. Swali ni kuwa kwa nini watu wanafanya hivyo. Mpaka sasa kuna watu wanapronounce UGANDA kama YUGANDA, na KENYA kama KINYA.

Pengine waheshimiwa ZITTO na WASSIRA wanaweza kutusaidia sababu zao za kuongeza hizo consonants.

Jibu lako zuri. Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…