Kwa nini "ss" au "tt" ?

Kwa nini "ss" au "tt" ?

Unachanganya vitu viwili Lugha na maneno ya kuazima, Kiswahili ni Kibantu kwa 100% ila kimeazima maneno mengi kutoka Lugha nyingine na Lugha zote Duniani zimefanya hivyo, kwa mf. kiingereza zaidi ya asilimia 60% ya maneno yake ni ya kilatini, lakini hakiitwi Kilatini bali ni kiingereza na ni lugha 2 tofauti kabisa au kijapani nusu nzima ya maneno ni ya Kichina lkn ni Lugha mbili Tofauti!

Hakuna kitu kama hicho Lugha haindikwi unavotamka, kuna Biblia zilizoandikwa kisukuma, au Kichaga au sijui Kihaya na hamna kitu kama Hicho hakuna mahali ambapo kuna tt kwa wakati mmoja au ss au ll ktk Kibantu hatuna huo Mfumo, ni hivyo tu!

Ila unaweza ukaandika neno lenye silabi mbili kwa mf. aa oo ee ii hapo sawa lkn sio herufi tu, kwa kifupi ni kwamba ktk Kiswahili au Kibantu hatuna neno ambalo linaishia tu na kwa mfano t bila ya silabi, m au n au s au herufi yoyote ile, na ndio maana Watz wengi wakiongea Kiingereza wanasema goingi badada ya going, au schooli badala ya school au plastiki badala ya plastic, Hoteli badala ya hotel na hilo tatizo ni kwa Wabantu woote awe Muhaye, Msukuma au Mgogo...


Kwa kweli huhitaji msaada. ni kusumbua tu
 
Point well taken. Swali ni kuwa kwa nini watu wanafanya hivyo. Mpaka sasa kuna watu wanapronounce UGANDA kama YUGANDA, na KENYA kama KINYA.

Pengine waheshimiwa ZITTO na WASSIRA wanaweza kutusaidia sababu zao za kuongeza hizo consonants.

Jibu lako zuri. Asante.

Huku Kenya UGANDA hutamukwa YUGANDA. kuitamka UGANDA ni kwa runinga wakati wa habari pekee..ama katika somo la kiswahili. Matamshi halili ya KENYA ni KEN halafu YA. Hata wazungu hawasemi Kinya bali Kinia, au Kenia
 
weka picha

double_s_logo.jpg
 
Huku Kenya UGANDA hutamukwa YUGANDA. kuitamka UGANDA ni kwa runinga wakati wa habari pekee..ama katika somo la kiswahili. Matamshi halili ya KENYA ni KEN halafu YA. Hata wazungu hawasemi Kinya bali Kinia, au Kenia


Asante mkuu kwa sahihisho.
 
Back
Top Bottom