Kwa nini TANESCO hawatoi fidia kwa wananchi wanaowaharibia mali zao?

Kwa nini TANESCO hawatoi fidia kwa wananchi wanaowaharibia mali zao?

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
2,660
Reaction score
3,501
Tumezoea miradi ya ujenzi wa barabara, majengo na viwanja mbalimbali, inapopelekwa mahali fulani na kukuta wananchi basi wananchi wanapewa fidia kwa uharibifu wa mali zao utakaosababishwa na ujenzi huo

Lakini naona hali hii ni kinyume kabisa inapokuja miradi mingine kama maji ma umeme. Naomba leo nijikite kwenye umeme al maarufu TANESCO

Hawa jamaa wakija kwanza wanakuja vijana tu wa kazi wanaanza kazi hutamwona kiongozi wao na wala hutaelewa uzungumze na yupi maana wote unakuta ukiwaangalia wanafanana

Hawa jamaa wakija kwenye kazi zao wakikukuta humo mfano nyumbani au shambani hakuna cha salamu, mwenyewe hapa ni nani, wala naomba kadha wa kadha kama ilivyo zoeleka kwa watanzania bali wao wakifika ni kufanya kazi tu na kuondoka kimyakimya

Hawa jamaa wakihakikisha tu kuna mti kwenye usawa wa sehemu zinapopita nguzo/waya zao basi mti huo hauna bahati hata uwe na kimo cha mita moja na haijalishi ni mti wa aina gani

Hawa jamaa bwana wanakuja mwezi wa 8 mikorosho imepakia hatari wanafyeka yote chini halafu wakiondoka wanarudi karibu na mwezi wa 11 ndipo wanafanya kile kilichosababisha wakate miti hiyo

Sasa hoja yangu ni kwa nini hawa jamaa hawalipi fidia kwa wananchi wanaowaharibia mali zao? Sina nijuacho kitaalamu lakini akili yangu inaniambia TANESCO ni mali ya serekali kama wale wengine

Naomba wataalam mniweke Sawa katika hili
 
Back
Top Bottom