Kwa nini Tanzani na Kenya zinafanana sana mambo yake?

Kwa nini Tanzani na Kenya zinafanana sana mambo yake?

Wapi nimeleta ligi hapo ..nimefananisha tabia za watu wa pwani ya Kenya na Tanzania na kuona ni moja ni kama nilivyofananisha watu wa bara wa Kenya na Tz..

Brother naona umetokea pwani , sasa hiyo inferiority yako usituletee wengine ambao hatuhusiki.. Hakuna asiyejua watu wa pwani mpo vizuri kwenye ustaarabu wa ndani ya nyumba,ukarimu , kucheza ngoma za kiasili , jando ,unyago na vyakula.. out of that sijaona sifa nyingine na nzuri zaidi hata wewe mwenyewe hujaziona na ndio maana hujazitaja...

Ni kama mchagga anijie juu kisa kumuambia kuwa ni mzuri katika biashara lakini bahili au wahaya ni wazuri katika elimu lakini wanapenda kujikweza ...sasa sijajua ni nini kilichokupanikisha RELAX MZEE

Mimi sina hiyo unayoiita inferiority complex, labda wewe ndo unayo kwani sijawahi kukutana na mtu wa Pwani ambaye hata huwa anaongea khs haya mambo ya kudharau na kukejeli wengine isipokuwa watu kama nyie ndo kila siku hapa hushinda kutukana na kukejeli watu Pwani na ni upi mchango wa Mchaga kwa TZ unaoungelea ukilinganisha na Pwani?
 
Samahani bro huwa sina kawaida ya kubishana na watu bila mantiki ..sijamshusha wala kumkweza mtu maana nimeongelea mtazamo wangu ambao unaegemea katika uhalisia wa niliyoyaona na wala sipo biased ..
Uwe mchagga mzaramo au mbena ..wote ni watanzania na binadamu mwisho wa siku

I'm sorry kama nimekupa any wrong impression...
 
Duh kuna kazi na shughuli hii ni shughuli
 
Eneo lote la Africa mashariki kama lilivyowahi kuwa koloni la muingereza na ndivyo hivyo baadhi ya mambo yetu tunayaendesha kwa kufanana. Kama makoloni yasingeanzishwa kwa hakika Afrika ingeonekana hivi:
africa-map-ethnic-george-peter-murdock-1959.jpg
 
Leo hii ndio mnajiuliza maswali ya msingi kama hayo, miaka ya hivi majuzi hapakua na Tanzania wala Kenya, kabla mzungu hajaja na kuchora mpaka na kuwaambia wa huko wajiite Watanzania na wa huku waitwe Wakenya. Kawakuta Wamaasai na Wajaluo, Wadigo n.k. na kuchora mpaka ndani yao hata baina ya ndugu ambao wanachangia baba na mama.

Tatizo ni kwamba Tanzania, Nyerere alianza kufanya experiments/majaribio ya mifumo ya kiujamaa kwa kuiga Warusi na Wachina halafu akaja kuyatelekezea kati na kuwachanganya kiasi kwamba mpo mpo tu, hamjijui kama nyie wajamaa au mabepari, imeshindikana kuamua kimoja sasa mnaishia kuwa na chuki na wivu kwa sisi wengine ambao tulikomaa na mfumo mmoja.

Mtanzania akitoka na kuingia Kenya au Uganda anaishia kuwa mwoga mwoga na kushangaa shangaa, akirudi kwao anaongea mabaya tu, hana lolote nzuri la kusema. Lakini Mkenya akiingia Tanzania au Uganda anajimix tena kwa muda mfupi na kuendana na yeyote bila uwoga wowote. Mimi ilinichukua muda mfupi sana kuwa mchakarikaji na mtu wa mishe ndani ya hiyo Dar yenu.
wakenya kwa kujipa promo!!!hata hivyo mi mwenyewe nairobi ilinichanganya kidogo lifestyle yenu,lugha ile sheng dah ilikuwa inanimix,japokuwa sikuja kutafuta maisha,ikabidi nirudi tu bongo!!
note:maisha ya nairobi mnayaweza wenyewe wakenya doh!
 
Hata wewe unafanya ule ule ujinga wenu wa kila siku kuzodoa watu wa Pwani, ustaarabu umefika Pwani kabla ya huko Mikoani, kwa maana nyingine Pwani ndiyo Tanzania, watu wa Mikoani bila ya Pwani hakuna Tanzania msisahau hilo, hata kunywa chai na kitoweo asubuhi ni ustaarabu wa Pwani, elimu yenyewe kusoma na kuandika kulianzia Pwani ndo kukasambaa Mikoani, hata jina la Tanga-Nyika hiyo ndo maana yake yaani Tanga (Pwani) na Nyika (msitu), hivyo kuwa mwangalifu kidogo kwenye haya mambo na usilete dharau na kejeli kwenye mambo ambayo nafikiri hata hauyaelewi.

Punchline!
Sitaki kuleta ligi zenu za kijinga za Pwani vs Mikoani, TZ vs Kenya bali nilitaka kuweka rekodi sawa, hizo dharau zenu hazina mshiko kwani mchango wa Mikoani kwenye TZ ni mdogo ulikinganisisha na Pwani!
naona hujamuelewa jamaa,soma vizuri umuelewe jamaa anajaribu kueleza kitu gani..
 
Hata wewe unafanya ule ule ujinga wenu wa kila siku kuzodoa watu wa Pwani, ustaarabu umefika Pwani kabla ya huko Mikoani, kwa maana nyingine Pwani ndiyo Tanzania, watu wa Mikoani bila ya Pwani hakuna Tanzania msisahau hilo, hata kunywa chai na kitoweo asubuhi ni ustaarabu wa Pwani, elimu yenyewe kusoma na kuandika kulianzia Pwani ndo kukasambaa Mikoani, hata jina la Tanga-Nyika hiyo ndo maana yake yaani Tanga (Pwani) na Nyika (msitu), hivyo kuwa mwangalifu kidogo kwenye haya mambo na usilete dharau na kejeli kwenye mambo ambayo nafikiri hata hauyaelewi.

Punchline!
Sitaki kuleta ligi zenu za kijinga za Pwani vs Mikoani, TZ vs Kenya bali nilitaka kuweka rekodi sawa, hizo dharau zenu hazina mshiko kwani mchango wa Mikoani kwenye TZ ni mdogo ulikinganisisha na Pwani!
Hili la Tanganyika ,umetuuzia chai kutoka wikipedia
 
Back
Top Bottom