Mi kila siku najiuliza "kwa nini Tanzania ni maskini?' Na jibu sipati. Najiuliza kwa sababu naona ni kama watu wana majibu ya kila swali. Humu humu JF uliza swali lolote, hata liwe technical vipi, mijitu inajibu bila wasiwasi na ni majibu yenye logic. Ikitokea problem yoyote watu wanakuwa walikuwa tayari na plan ya nini kilitakiwa kifanyike ili problem hiyo isitokee!!
Na watu hawa wote wapo makazini na wengine kwenye biashara zao flani. Sasa kama watu wana majibu yote na plan zote na solution zote, kwanini bado kasi yetu ya maendeleo ni ndogo hivi???? Na rasilimali zingine zote tunazo kibao!