Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
Hali ya mambo inavyokwenda kwenye nchi hii inafanya turejee nyuma na kujihoji kuwa kwa nini "Tulipigania Uhuru wa Tanganyika?".
Damu za wazee wetu zinatulilia, zinahoji uhalali wa sisi kurithi nchi nchi hii,
Madini tumeshindwa kuyalinda na sasa nchi imebaki ukiwa, nchi imepasuliwa miamba kuanzia kas hadi kusi, nchi imebaki matundu tena wasivyo na aibu wameyacha wazi bila kufukia,
Ndio, wangefukia na nini wakati vifusi vyote wamepakia kwenda navyo ulaya?
Wamemaliza madini sasa wamehamia kwenye mbuga, huku jangiri sio mgeni bali ni serikali yenyewe tuliyoipa dhamana!
Sasa watanzania wanasubiri msaada wa mamlaka za Hong Kong ili kubaini wezi, jiulizi zimepitaje bandarini mpaka mashariki ya mbali?
Hivi tumwamini nani kama tuliyempa mamlaka hasimamii sheria za nchi?
Mwezi juzi tu wamekwapua twiga wetu wazimawazima na kuwakunja mpaka wakatosha kwenye ganda la kiberiti na wakatokomea nao mpaka Qatar.
Ndege ya jeshi la Qatar ndio iliyotumika ubeba twiga na sungura wetu wakiwa hai!
Hebu jiulize ni nchi gani duniani ambayo ndege ya kijeshi ya kigeni inaweza kutua bila usalama na IKULU vya nchi hiyo kuwa na taarifa za msingi?
Hali ya kijamii ni mbaya sana, elimu inazidi kudorola, afaya imebaki mfukoni mwa mgonjwa,
Kwaujumla hawatupi nafasi tupumue, wakimaliza hapa wanahamia pale!
Swali ni kwa nini tulipigania Uhuru wa Tanganyika?.
Kama ni ili tujitawale mbona siasa zetu chafu?
Kama ni ili tuwe huru kutoka mikononi mwa wakoloni wanyonyaji, sasa mbona tupo na mkoloni mweusi ccm mbaya kuliko mzungu mwenye pua ndefu?!
Naamini taifa limewakosea wale wazee wetu 17 wapigania uhuru wa nchi yetu, na damu yao inatulilia,
Hebu tutafute maana halisi ya Watanganyika kudai uhuru ilikuwa ni nini?
Na je tunaishi katika lengo hilo?