Hoja yako ilikuwa nzuri sana, isipokuwa iliharibiwa na madai ya kumwagika damu!Kwahiyo unamaana kuwa hiyo ndio sababu ya yanayotokea leo katika nchi hii?
Watanganyika hawakupigania UHURU wa nchi yao?
Unamaana UHURU wa Tanganyika wale wazee 17 waliletewa kwenye kisosi tu?
Hebu fafanua zaidi mkuu!
Kila mtoto wa shule ya chekechea Tanzania anajua Tanganyika haikupigania uhuru kwa damu, hata chekechekea za kata zinalijua hili.
Inaweza kuonekana ni kitu kidogo sana, Watanzania hatujali vitu vidogo vidogo, lakini kwangu nikisoma kitu kama kile, najiuliza hivi huyu mtu kweli unajua chochote kuhusu historia ya nchi hii mpaka aje kutupa prescription hapa za matatizo yetu ya leo?