Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Kwa nini huwa tunawachukia watu fulani? Kwa nini mtu anaweza kukuambia kitu kidogo cha kukusaidia lakini ukakasirika na kumfutilia kabisa mbali na maisha yako? Nianze na hitimisho: Chuki kwa mtu, aghalabu, ni ujumbe wa mgogoro wa kihisia usiotatuliwa. Chuki ni njia ya mkato ya kupambana na zimwi tuliloshindwa kulishughulikia. Nitaeleza.
Kila mtu, kwa namna yake, ana ule ukurasa wa tabia zake asiopenda kuusoma kwa sauti. Inaweza kuwa historia ya kufeli, kuibia mitihani, kuachishwa kazi, fedheha ya umasikini, kuachwa kwa aibu, ugomvi uliokuachia majeraha, tabia mbaya usizopenda kujitambulisha nazo na kadhalika. Ufikirie ukurasa huu kama mzimu unaoweka rehani heshima yako na unapambana kuudhibiti usifahamike na watu ukakuletea madhara.
Sasa kuna wale watu, ambao kwa sababu zao mbalimbali, hupenda kukusomea ukurasa huu kwa sauti hata kama wanajua huupendi. Hawa wanaweza kuwa watu uliokua nao, uliosoma nao, uliowahi kufanya nao kazi mahali ulikoharibu na kadhalika. Hawa ni watu ambao hata ukionekana kufanikiwa wako na wewe kukumbusha udhaifu wako, na hawakuruhusu kabisa uufunike ukurasa huu uendelee na maisha yako mengine.
Kwa vile hatupendi historia zetu zinazotutia unyonge, mara nyingi tunashawishika kujilinda kwa kujitenga na watu hawa na wakati mwingine ikibidi kuwachukia. Hapa ndipo inapokuja nadharia ya mshunuzi Carl Gustav Jung. Unapowachukia na kujitenga na watu wanaokukumbusha unyonge (mzimu) wako, Carl Jung anasema hiyo ni njia yako ya mkato unayotumia kuusoma ukurasa huu bila kupata maumivu makali. Unapomchukia mtu Carl Jung anasema wewe unaogopa kukutanishwa na zimwi linalokutafuna maana, kwa hali ya kawaida, chuki sio hulka ya mwanadamu. Chuki ni ujumbe wa wapi una kidonda. Huwezi kumchukia mtu kwa kukuzushia tabia mbaya unazojua fika huna. Chuki ni kama handaki tunalotumia kufukia tatizo halisi usilotaka lifahamike na watu.
Kuishinda chuki uliyonayo kwa mtu, Carl Gustav Jung anasema unahitaji mchakato wa dhati wa kukabiliana na kipande kibaya cha maisha yako, kipande usichokipenda, kipande kinachokufanya ujisikie aibu, fedheha, dhalili na hasira dhidi yako mwenyewe. Ukiweza kushughulikia kipande hiki unakutana na wewe mwingine, wewe halisi aliyebadilika kiasi cha kutokuogopa tena historia yako. Ukifika hapo, Jung anasema, unapata uhuru wa kuishi na historia yako, kukumbuka makosa yako bila maumivu, na hivyo, hutomchukia mtu hata kama kila mkikutana anakusomea ukurasa wa maisha yako usioupenda kuusoma kwa sauti.