Kwa nini tunaendelea kuwapigia kura viongozi ambao hawaperform ktk kipindi chao

Kwa nini tunaendelea kuwapigia kura viongozi ambao hawaperform ktk kipindi chao

kwanini tunaendelea kuwapigia kura

  • kwanini

    Votes: 1 100.0%
  • tunawapigia

    Votes: 0 0.0%
  • kura

    Votes: 0 0.0%
  • viongozi

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    1
Uliyoyasema ni kweli lakini, tuna vingi sana vinavyosababisha na unaweza ukaona kila mahali pana at least sababu moja kati ya hizo nilizozitaja. Kukaribia kura za mpinzani wako si kushinda. Kinachotakiwa ni kupata kura zaidi yake...... na si chenga twalawa ...........lakini kufungwa .......... twafungwa

lakini ndo hapo linapokuja swala la wanaohesabu kura hizo?
wasimamizi hao
Je tutafika ??
 
ila am so confused inakuwaje katika akili ya kufikirika tunaendelea kufanya hivi .wakati mabadiliko matunda na mafanikio hayaonekani

kuna Mbunge mmoja kaja hapa wa CCM kanunua masanga kwa vijana vijana baada ya kulewa wakaanza kumzomea 🙂lakini kuzomea tu haisaidii ni vitendo zaidi ndo vinatakiwa ili kuleta mabadiliko ktk nchi hii
Walipaswa wa mtwange vichwa eehhh teh teh....hata hiyo zomezome ni mwanzo mzuri kwani ujumbe si aliupata...
 
Sababu ni hizi.........

1. Kipindi cha uchaguzi ndiyo utaona TV zote zinaonyesha vita, huku zikitangaza kuwa kumchagua yeyote nje ya CCM ni kutaka vita. Kwa vile hatujazowea vita, lazima tuogope."

yaani hapo ndio huwa siielewi hii strategy ya nambari wani,wanatuonesha kwamba wapinzani wakishindwa kutakuwa na vita,hivi hii si inamaanisha kuwa wao wakishindwa ndio wataazisha vita?vinginevyo sioni kwanini waseme wapinzani wakishinda kutakuwa na vita.
 
we unadhani lowasa anaweza kupingwa? atapigiwa kura tu.....mwenye pesa sio mwenzio anaweza kununua kila kitu isipokuwa uzima wa milele,rejea----twanga pepeta-MTU MWENYE PESA.Watz wakipata pilau kofia fulana na pipi kwa ajili ya watoto wao inatosha kumrudisha kiongozi aliyeperform madly..........wa2 ni warahisi wa kurubuniwa kwa sababu ya vijisenti vyao..................
 
Tunawapigia kura viongozi wabovu kwasababu wapiga kura wengi bado hawajasoma waraka wa wakatoliki.Waraka wa wakatoliki umebeba mambo muhimu sana kwa wapiga kura ambao hawana elimu ya uraia.

Unafikiri Kingumge mjinga kulishambulia kanisa katoliki.Hataki wadanganyika wazinduke.
 
Upuzi tu unaogelewa hapa,Yule Injinia wa Kyela Wanataka wamtoe yule mbunge wao sijuhi anaitwa nani vile.Kisa amewasahau uko kwao na wanamwona tu kwenye TV akipiga kelele Kitaifa,watu hapa wakamjia juu na kusema katumwa na Mafisadi,leo nyie wenyewe mnalalamika hapa kile kile Injinia alikuwa ana lalamika.Injinia wa mabomba anasema Mbunge wake hajaperform kule kwao watu wa nje mnakuja juu bila ata kufanya kautafiti kidogo,Kuna mmoja hapa mpaka akaenda mbali kwa kusema wananchi wa kyela wavivu wanataka wafanyiwe kila kitu na mbunge wao....Watu tumekuwa wapuzi hapa kazi kugeukageuka kwa kutegemea mapenzi yetu kwa mtu furani bila kufanya uchunguzi kwanini wengine wanalalamika.
 
hawakubariki hata kidogo mie mbunge wetu lol kimeo lakini ndo mauzauza yayotokea everyday


Kwani shosti we uko jimbo gani. Mi niko Kawe na mbunge wangu anaitwa Rita Mlaki. Am telling you, afadhali mbunge wenu kuliko huyu. Hamna kitu kabisa mle.
 
Swali hili ni zuri sana.Hata hivyo si swali rahisi sana.Kwa ufupi ninaweza tu kusema kwamba there is alot of manipulation going on behind the scenes of our own selves kiasi kwamba wametufanya kuwa kama mataahira hivi.Wengi wetu mawazo yetu ni guided,sio original.Wanatumia mbinu nyingi sana.Hata simu au computer ambayo naamini unaipenda sana inatumika kwa malengo hayo.Zipo mbinu nyinyi sana nimetaja moja au mbili tu.Kma unataka kujua mbinu hizo zaidi nenda [ame]http://en.wikipedia.org/wiki/Mind_control[/ame]. Kwa shughuli hii viongozi wetu wanatumiwa na agents wa nchi za magharibi kuifanikisha.Hakuna ubishi kwamba na wao wanafaidika na harakati hizo,kwa vile tunakuwa rahisi kuswaga.

Lakini pia tusisahau kuwa wizi wa kura upo kwa kiwango cha juu sana!
Nashangaa nasikitika na sipati majibu kabisa
Hivi huwa ni akili zetu watanzania au ??
Tunaelewa kabisa huyu ni mbunge wetu whatever lakini katika kipindi chake cha miaka 5/10 or more hajafanya lolote zaidi ya kulala na kutowakilisha hoja zetu |Bungeni kijijini au maeneo yetu hayatamaniki ,hatuna maji ,umeme,barabara mbovu magari hayapiti ,hatuna mahospital ,kina mama wajawazito na watoto wanateseka ..ni matatizo yanayoonekana bila kificho
Inakuwaje bado tunaendelea kuwapigia kura na kuwaweka madarakani?😕😡
Inakuwaje lakini??
 
Kwani shosti we uko jimbo gani. Mi niko Kawe na mbunge wangu anaitwa Rita Mlaki. Am telling you, afadhali mbunge wenu kuliko huyu. Hamna kitu kabisa mle.

aaaaha ahhaa aaaaah Mabina mbunge wangu ..hafai hata kupungiwa mkono akiwa anapita -hafai hata kutizamwa popote na hafai zaidi katika ufalme wowote
afadhari huyo Rita mlaki
 
Kwa mantiki hii hakuna haja ya kupiga kura unless kuwepo na transparent process.
 
Kwa mantiki hii hakuna haja ya kupiga kura unless kuwepo na transparent process.

ndo maana mie nikauliza hivi kwa nini huwa tunapiga kura ,ingependeza kam siku moja nchi nzima ikaweka mgomo baridi kwa swala hili
 
ndo maana mie nikauliza hivi kwa nini huwa tunapiga kura ,ingependeza kam siku moja nchi nzima ikaweka mgomo baridi kwa swala hili
Kinachoboa ni kuwa hata ukikunji kupiga kura, bado huyo usiyempenda atashinda tuuuuuuu.... Tatizo ni kuwa badala ya ku-deal na source, sisi tunahangaika na outcomes. Kwangu tatizo linaanzia hapa......

1. Tume ya uchaguzi ........... Chama chatu tupu
2. Wachapisha karatasi za kupigia kura.........chama chetu tupu
3. Wahesabu kura..................chama chetu tupu
4. Wasafirisha kura toka vituoni.......chama chetu tupu
5. Walinda kura zisiibiwe..............chama chetu tupu.
6. Watangaza matokeo..............chama chetu tupu.
7.Wagombea..............chama chetu tupu.
8. Mawakala.......chama chetu tupu
9. Walinzi vituo vya kupigia kura..............chama chetu tupu

Kwa hiyo ili kuondoa tatizo, ni lazima mfumo mzima unaohusu uchaguzi ubadirike, kuanzia kufikiri kuhusu uchaguzi hadi kumpata mshindi wa uchaguzi huka. Mmoja wa wshindani akiwa ndiye anaye-control kila kitu, lazima atavutia kwake kwa namna au gharama yoyote, hata ikibidi kuuwa, kufunga watu hadi uchaguzi upite etc......... KAZI BADO KUBWA SANA
 
aaaaha ahhaa aaaaah Mabina mbunge wangu ..hafai hata kupungiwa mkono akiwa anapita -hafai hata kutizamwa popote na hafai zaidi katika ufalme wowote
afadhari huyo Rita mlaki

Mabina? Duh huyo kweli kimeo. Wala sijawahi kumsikia. Jimbo gani hilo? Mpigeni mawe. Lakini hata Ritha Mlaki mmemjua kwa kuwa alikuwa naibu waziri, aliyeteuliwa na mzee wa Kiwira. Naskia alikuwa nyumba ndogo yake. Hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi!
 
Back
Top Bottom