Mimi binafsi nilishiriki kwenye mchakato. Nilipata fursa ya kukutana na tume nikiwa na kundi la watu wapatao ishirini na tano. Kuhusu suala la Muungano timu yangu ilipendekeza SERIKALI 3. Sababu muhimu ilikuwa kama ifuatavyo:
- Kama Muungano ulikuwa wa nchi mbili, ni vema hizo nchi zikaendelea kuwa na historia yake (Serikali ya Tanganyika.....Serikali ya Mapinduzi) ili kuwakumbusha vizazi kuwa Tanzania ilitokana na nia njema ya kuunganisha nguvu ya pamoja (Umoja ni Nguvu) ili kuweza kutetea maslahi yetu.
- Kwa sasa muundo wa serikali mbili hauleti picha kama kuna nchi ziliungana wakati moja ime-maintain identity yake (SMZ) na nyingine imesahaurika (Tanganyika). Hii haileti usawa kabisa
- Mgawanyo wa rasilimali na fursa utaendana sawa na mchango wa mwanachama - proportionate distribution based on equity not on equal! Kama Zanzibar ni raia mil 6 hawawezi kudai haki sawa na raia milioni sitini (huu ni mfano tu), hawawezi kuwa na nafasi za uongozi sawa. Similar hata mgawanyo wa fedha utaendana na mikakati ya pamoja kwa kuzingatia mahitaji ya makundi mbalimbali
- Serikali kuu (Muungano) itakuwa na watendaji wachache....ambayo wanakuwa na political power kwa zile za Muungano kwa kufuata mijadala, ushawishi na makubaliano
Sasa, endapo mfumo wa SERIKALI 3 haukubariki, tuliishauri tume ipendekeze Serikali1. Sababu za msingi ni hizi
- Hapo hakuna mimi Mpemba, Mgazija wala Mtanganyika. Wote tunakuwa watanzania
- Mgawanyo wa rasilimali utawekwa sawa bila kujali ni visiwani au bara, wote ni watz wanahitaji huduma toka serikali yao
- Itapunguza maneno yasiyo ya lazima kusema kuna sheria ya Znz na sharia ya bara. Tutaongozwa na serikali moja tu.
- Itaondoa mijadala ya Zanzibar ni nchi /////si nchi. Na je Tanganyika ni nchi au si/// nchi? Itakuwa nchi moja, lugha moja taifa moja na jamii moja ya watanzania
- Hakutakuwepo kubaghuliwa wabara waendapo Zanzibar maana ilmradi ni Mtz ruksa kuishi popote na kuendeleza maisha yako
- Serikali ya mzigo (mawaziri kibao) itakuwa imeondoka, na hivyo hela nyingi kuingizwa kwenye maendeleo badala ya kuhudumia viogozi. Pia hakutakuwepo na orodha ndefu ya viongozi wastaafu wanaokula pensheni bali orodha itakuwa ndogo
NI UPOTOVU WA NIDHAMU KUMSHAMBULIA MZEE WARIOBA, LABDA WALE WANAOMSHAMBULIA HAWAKUPATA MUDA (HAWAKUTAKA KWENDA) KUKUTANA NA TUMI YA MZEE WARIOBA WAKASUBIRI KUJA KUMSULUBISHA KWENYE VYOMBO VYA HABARI. HII SIO SAHIHI