Kwa nini tunashauriwa unapoiwasha gari uiwache ingurume kwa muda kabla kutia gia

Kwa nini tunashauriwa unapoiwasha gari uiwache ingurume kwa muda kabla kutia gia

Habari wadau , hope mu wazima.

Leo nahitaji munisaidie ufafanuzi kuhusiana na hili kuiwacha gari ingurume kama imelala muda mrefu kusudi wengine wanasema temperature ishuke lakin wengine wanadai ni kuifanya oil ipande kwenye mashine.

Sasa kuna ukweli wowote hapa? Na ikiwa hali ndio hiyo vipi kuhusu vyombo vyengine vya moto vya maringi mawili navyo tuwache ingurume ili oil ipande ama hakuna madhara

Naomba kuwasilisha
Ili oil ziweze kusambaa kwenye ijini na joints mbalimbal;i kuzxilainisha na kupunguza msuguano.
 
Hujui kuwa unapokanyaga mafuta na mshale wa RPM ukanyanyuka sana ndivyo ambavyo ulaji wa mafuta hufanyika kwa kasi pia?

Ndiyo maana tunapowasha gari tunasubiri kidogo ipate moto ndiyo uondoe gari..

Sehem ya kutumia lita 10, utajikuta umetumia lita 15 au zaidi na hivyo kukufanya uone gari yako inakula sana mafuta kumbe gari haina tatizo isipokua tatizo ni namna unavyokanyaga.
 
Gud Answer
Kwakiswahil ni Oil/Vilainishi viweze kutembea sehemu zote muhimu ili kuzuia Msuguano usio wa lazima.
Engine imetengenezwa kwa kiwango kikubwa sana,unapoona taa ya oil tu imezima kwa zile sekunde tatu, basi oil hua imeshafika maeneo yote husika ili kuweka ulainishi wa vyuma
 
Kuiacha gari iungurume kidogo ni muhimu.

1. Gari zote zinawakia kwenye Open loop. Hapa mafuta mengi huwa yanaenda. Ikishapata joto ndio inaenda kwenye closed loop.

2. Msuguaono huwa mkubwa gari ikiwa ya baridi.

3. Oil karibu yote huwa inashuka chini hasa kwenye engine. Hivyo ukisubiri unaipa muda gari yako ili oil ipande.
 
Engine imetengenezwa kwa kiwango kikubwa sana,unapoona taa ya oil tu imezima kwa zile sekunde tatu, basi oil hua imeshafika maeneo yote husika ili kuweka ulainishi wa vyuma

Kuna gari haziwashi hiyo taa lakini oil haifiki baadhi ya naeneo.

Unalijua hilo?
 
Kuna gari haziwashi hiyo taa lakini oil haifiki baadhi ya naeneo.

Unalijua hilo?

Majority ya magari madogo hayahitaji kusubiri more than 5 seconds ambayo nayo sio muda wa kusema unasubiri. Oil huwa inapanda instantly na katika galley za oil kwenye injini mafuta si yote yanayoshuka. Pia katika bearings za muhimu imekuwa designed by default kutokuwa kavu pindi gari inapozimwa (yaani oil haipo kabisa). Kiasi kinchorudi kwenye oil sump ni kile hasa kinachokaa kwenye valve train na bado kwenye valve pia oil huwa bado ipo kidogo.

Nadhani cha msingi labda coolant inakuwa bado ni ya baridi hivyo throttle inakiwa open ili kuharakisha zoezi la kuipa joto ili gari liwe kwenye operating temperature nayo haikuzuii kuendesha gari hadi ipate joto ila zingatia kutokwenda kwenye rpm kubwa kabla ya operating temperature kufikia.

Oil hupanda instantly na lubrication huanza tu pale oil pump inapoanza first revolution.

MAONI BINAFSI.
 
Kuna gari zinapiga pink sound ukikanyaga accelerator unaijua tafsiri yake?
 
Sababu ya kitaalaamu huwa ni kufanya engine ipate joto sahihi kwaajiri ya kuruhusu oil iweze kuflow vema na kufanya kazi yake ya kusaidia kusiwapo na msuguno.

Kwa inchi za baridi huwa kuna hadi heater za magari kwaajiri ya kuipa joto engine kabla ya kuiwasha.....

Ila kwa afrika tuna bahati ya hali ya joto na ubaridi wastani nyakati za asubuhi. So ukiwasha gari ni dakika 5 tu zinatosha kuwa tayari kwaajiri ya kuchapa lami.

Anyways ni hiyo tu sababu ya msingi.
 
Wale wenye vi-degree piteni hapa mupate elimu,,,wengiwenu hamjui ku2mia magari,,munajuwa kuwasha na kutula gia.
 
Oil inaweza kuwa haifiki vizuri baadhi ya maeneo. Hasa Oil inapokuwa nzito.

Oil pressure inakuwa normal ila baadhi ya sehemu zibakuwa hazina oil.

Kuna mlio gari huwa inatoa madhalani ukikanyaga accelerator.
 
Unaandaa gari kwa ajili ya tendo la safari. Na wakati wa kuzima pia usilizime ghafla baada ya safari ya masaa mengi unaliacha kwenye idle mode kwa muda kidogo.
Stori za vijiwe vya Singeli
 
Oil inaweza kuwa haifiki vizuri baadhi ya maeneo. Hasa Oil inapokuwa nzito.

Oil pressure inakuwa normal ila baadhi ya sehemu zibakuwa hazina oil.

Kuna mlio gari huwa inatoa madhalani ukikanyaga accelerator.

Kuna mmama mmoja ivi,,,ana lipikapu yeye anajuwa kuwasha na kukanyaga maresi kisha anatimka.
 
Back
Top Bottom