Nimekupata vizuri sasa mkuu kichuguu. Sasa tukitaka kupambana na hili tatizo la hela hafu mtaani tunafanyaje?
Napenda kuungana na wote waliochangia kuwa ni gharama isiyo ya lazima kuchapisha hela mpya. Fedha nyingi zipo mijini na kubadili sarafu ina maana ni kwa nchi nzima. Ukisoma ripoti ya hali ya huduma za fedha nchini (2006 , study mpya itakuwa tayari June 2009) utagundua kuwa huduma za kibenki zinapatikana kwa watu 1.6mil tu wengi wakiwa mijini. Nilikuwa Morogoro ndani ndani hivi majuzi ni kuwa ukitaka kupata huduma za benki inabidi kupiga mwendo wa km 160! mpaka morogoro mjini. Sasa kuna watu zaidi ya Mil 25 ambao kwa namna moja au nyingi na kwa uwezo tofauti tofauti wana fedha mifukoni mwao wapo mbali sana na benki. Kwa hali hiyo ukibadili sarafu kwa ajili ya mafisadi wachache ni watanzania wengi watapoteza kiwango kikubwa cha fedha (pengine hata kiwango ambacho mafisadi wanacho) na muda wa kuzibadili ambao ungeelekezwa kwenye shughuli za kiuchumi, GDP itaporomoka kama kweli wanatumia vigezo stahili. Kuhusiana na gharama pia ijulikane kwenye mfumo wa TZD ni kuwa inabidi kubadili kila kitu kwa mfano vouchers, payment systems, mikataba, baadhi ya sheria za nchi zenye viwango vya hela, nk nk. Gharama zote hizi ni ghali na unbearable!. Unless wataalamu waje na model ambayo itanonyesha kuwa tutafaidika kwa hili.
Pili kama lengo ni kuwabana mafisadi wachache (sidhani kama syndicate nzima inazidi watu mia tano) ni kuijenge uwezo mahakama zetu ziweze kuwashughulikia tu kwa mujibu wa sheria.
Tatu: Sina hakika kuwa kuna hela nyingi mitaani kwa sasa kuliko ilivyokuwa miaka miwili iliyopita. Nakumbuka watu walikuwa na hela nafikiri hizo za kifisadi ukienda kuangalia kiwanja mahali tu unaambiwa bei ya kufa mtu.. ukibisha naambiwa mbona jirani yangu ameuza kwa bai hiyo hivi majuzi. Kigezo cha kuwepo hela nyingi ni kuongezeka kwa inflation kwa maana ya kuwa watu wengi sasa wana hela nyingi na vinavyozalishwa ni vichache. Inflation tunayoiona sasa ni kwa sababu gharama za uzalishaji na kodi zimekuwa kubwa kwa hiyo ilalazimika vitu viuzwe bei mbaya. Wakati wa mzee ruksa ilifika mahali watu wanakuwa na hela nyingi mpaka wanazichomekea kwenye soksi na kuna wakati mtu alikuwa akiingia baa anasema fungeni wape watu vinjwaji. Hapo inflation ilikuwa 30% na kukopa benki kama 35%.
Kufanya direct intervention kwa kutoa fedha kwenye mzunguko ni mfumo wa kizamani. Kwa sasa kinachotakiwa ni serikali kutoa fedha zake katika mabenki ya biashara na kuzirudisha BoT. Pili serikali iimarisha masoko ya mitaji. Nitakupa mfano mmoja wa NMB. Walikuwa wamelega kupata bil 60 lakini maombi yalikuwa bil 200 kama sijakosea. Sasa hii ina maana gani. Ni kuwa kama tukiwa na kampuni imara zenye mwelekeo mzuri, watu wapo tayari kuwekeza kwenye hizo kampuni. Wakiwekeza ni kuwa wanatoa fedha kwenye mzunguko na hizi zitatumika kujenga makampuni imara yatakayotoa ajira zaidi na kutumia malighafi ya watanzania walio vijijini pengine. Badala ya kuwa na soko tu la hisa la Dar, tuwe na masoko mengine ili isaidie kutoa fedha kwa wananchi na kukuza mitaji. Tatu serikali kupitia vyombo vyake vya fedha viandae mkakati maalum wa kuharakisha usambazaji wa huduma za fedha. Kuwe na mabenki, mutual funds, waadae wataalamu wa kutosha. Ikiwezekana kila anayepewa fedha ziingie kwenye mfumo wa kibenki. Cha ajabu ni kuwa hili linaeleweka hata kwa benki kuu lakini ukienda seminars watu wanapewa cash cash tu bila hata kujiuliza. Baada ya muda BOT inakuja kutangaza tenda ya treasury bills kwa ajili ya kupunguza fedha mitaani. Mwisho wafadhli wote wanaotoa fedha wabanwe kuwa fedha zote zinazoingia nchini zipitie kwenye vyombo vya fedha hasa hasa benki kuu. Kinachotokea sasa ni kuwa ukiangalia fedha inayooahidiwa na kusemekana kutolewa na wafadhili ni kubwa kuliko ile ambayo actually inaingia kwenye account za serikali. Ifahamike tu kuwa mtindo wa wafadhili kutoa misaada directly kwa walengwa na nyingine kwenye mifuko yao binafsi inaadhiri kuwepo kwa fedha nyingi mifukoni. Kwa ambao wanataka kusoma zaidi wadownload na kuanalyze hizi docs
Naomba kuwasilisha.