Wanajukwaa,
Sote tunafahamu kwa nchi yetu na maeneo mengi haoa ulimwenguni, ikifikia kipindi cha sikukuu au likizo za wanafunzi abiria wanakuwa wengi kupita kiasi.
Lengo la uwepo wa usafiri wa uhakika umma ni kuhakikisha watanzania wanawahi ratiba zao mbalimbali huko waendako bila kulazimika "kutoboa mifuko yao".
Imekuwa ni desturi nchini kwetu kuwepo kwa changamoto ya kupata nafasi kwenye mabasi, treni au ndege kipindi cha high season mfano sikukuu za Krismas au kipindi cha shule kufunga/kufungua. Inasikitisha kwamba changamoto hiyo ni endelevu, ipo kila mwaka. Mara chache mashirika ya ndege huwa yanajiongeza kuweka safari za ziada, lakini wasafirishaji wa barabara na treni ya SGR hawaweki mkakati wowote. Hii sio sawa kibiashara na kihuduma.
Natoa wito hili nalo wakalitazame ili kuwezesha mashirika/makampuni kutengeneza pesa za ziada kwa msimu huo na kuwapa huduma bora wateja wao..