Kwa nini Tusiwe na Serikali Moja.....!

Kwa nini Tusiwe na Serikali Moja.....!

Head teacher

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2012
Posts
1,796
Reaction score
412
Siku moja nilikuwa nafundisha kuhusu Muungano wetu katika shule moja ya sekondari. Niliwafafanulia jinsi Nchi mbili za Zanzibar na Tanzania Bara zilivyoungana na kuunda nchi moja "Tanzania" yenye serikali mbili. Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanzania. Mwanafunzi Mmoja akaniuliza kwanini serikali mbili na sio moja? Kabla sijajibu hili mwanafunzi mwingine akauliza kwanini zisiwe serikali tatu? Duh... yalikuwa maswali magumu ukizingatia hata mimi teacher sifahamu vizuri staili ya Muungano wetu. Si unajua mbinu za maticha, nikawaambia kila mmoja akatafute majibu ya haya maswali mawili.Topic iliyokuwa inafuata ilikuwa ni mambo ya Muungano. Nilijua kwa vyovyote tusingeelewana hadi haya maswali mawili yajibiwe na mimi nipate nafasi ya kuitafuta hati ya Muungano nione ni kwa nini Nyerere na Karume waliafikiana serikali mbili na si Moja..?. Kwa bahati nzuri sana kengere ya lunch break iligongwa name kupata mwanya wa kula kona...Ni noma humu madarasani, Muungano haueleweki.
 
Zanzibar itanezwa.... Yaani wao wanaona mikoa ya bara imememzwa..... and so will be zenji kama tukiwa na serikali moja.
 
ungewaambia ni muungano wa Zanzibar na Tanganyika. wewe ulisema na Tanzania bara. walimu wa siku hizi bwana!
 
Nafikiri mpango wa serikali tatu ni mchakato kuelekea kuuvunja Muungano taratibu pasipo maumivu makali kwa upande wowote. Subiri Mtaona!
 
Hakuna nchi ya Tanganyika ndani ya katiba.

ilikuepo baada ya uhuru na kabla ya muungano. kabla ya kuungana mwaka 64, Tanganyika ilikua ikitajwa. sidhani kama mwalimu ana sababu ya kukwepa hili kosa alofanya
 
Nafikiri mpango wa serikali tatu ni mchakato kuelekea kuuvunja Muungano taratibu pasipo maumivu makali kwa upande wowote. Subiri Mtaona!

tukivaa unafiki wetu kabisa tunasema tunaupenda muungano, lakini aslimia 90 Hatuutaki, japo kwa unafiki tunasema tunautaka, japo jina lomezoeleka!
 
ilikuepo baada ya uhuru na kabla ya muungano. kabla ya kuungana mwaka 64, Tanganyika ilikua ikitajwa. sidhani kama mwalimu ana sababu ya kukwepa hili kosa alofanya
Nafundisha jambo linaloruhusiwa kisheria, kusema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kuvunja katiba ambayo inasema Tanzania imetokana na muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar. upo..!
 
tunataka nchi moja ya tanganyika .zanzibar ijitenge tuwe na nchi yetu.
 
Mwalimu pole na mkasa. Ungewaambia wanafunzi wako "wawe na uzalendo na nchi yao". Hata sisi wazazi wao tunapouliza maswali mengi serikalini ndivyo tunavyoambiwa na viongozi wetu. Lakini pia ujue definition ya "mzalendo", maana wanaweza kukuuliza pia. Sasa kama utachukua ile iliyoko kwenye mwongozo wa kamati kuu ya chama tawala, sawa au kama ile ya kamusini, sawa vyote jiandae tu mwalimu. Wanafunzi na vijana tuliokuwa nao sasa ni tofauti kidogo na wa miaka ile.
 
tukivaa unafiki wetu kabisa tunasema tunaupenda muungano, lakini aslimia 90 Hatuutaki, japo kwa unafiki tunasema tunautaka, japo jina lomezoeleka!
You are Wrong ni 99 percent hawautaki isipokuwa 1% ambao ni viongozi wa CCM wanautaka kwa malengo yao
 
Vigumu kuipata maana wazanzibar wangekuwa wanahitaji muungano wangekuwa na subira kwenye kutangaza kuwa wao ni nchi. Hatutaki huu muungano wa kinafiki maana tunaweza kushirikiana kama vile east African community countries na hao wazanzibari. serikali moja? hivi mnawajua wapemba nyie? wanauchungu na nchi kuliko kitu kingine chochote na hawatakubali upuuzi wa serikali moja.
 
Back
Top Bottom