Head teacher
JF-Expert Member
- Mar 10, 2012
- 1,796
- 412
Siku moja nilikuwa nafundisha kuhusu Muungano wetu katika shule moja ya sekondari. Niliwafafanulia jinsi Nchi mbili za Zanzibar na Tanzania Bara zilivyoungana na kuunda nchi moja "Tanzania" yenye serikali mbili. Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Tanzania. Mwanafunzi Mmoja akaniuliza kwanini serikali mbili na sio moja? Kabla sijajibu hili mwanafunzi mwingine akauliza kwanini zisiwe serikali tatu? Duh... yalikuwa maswali magumu ukizingatia hata mimi teacher sifahamu vizuri staili ya Muungano wetu. Si unajua mbinu za maticha, nikawaambia kila mmoja akatafute majibu ya haya maswali mawili.Topic iliyokuwa inafuata ilikuwa ni mambo ya Muungano. Nilijua kwa vyovyote tusingeelewana hadi haya maswali mawili yajibiwe na mimi nipate nafasi ya kuitafuta hati ya Muungano nione ni kwa nini Nyerere na Karume waliafikiana serikali mbili na si Moja..?. Kwa bahati nzuri sana kengere ya lunch break iligongwa name kupata mwanya wa kula kona...Ni noma humu madarasani, Muungano haueleweki.