Source:
KWA NINI TUNASEMA IBADA ZA WAFU NI IBADA ZA KIPAGANI SEHEMU YA I
ANGALIZO:
a. Ninajua, tena nina uhakika sio wote ambao watakubaliana na mafundisho haya, wapo ambao ni kwa sababu hawaujui ukweli, wapo ambao ni kwa sababu tu wamekaririshwa na dini zao na wapo ambao ni mawakala typically wa Ibilisi kwa hiyo wako kwa kazi maalumu ya kumsaidia shetani kuipindisha kweli ya Neno la Mungu.
b. Jambo la pili nimegundua kwamba, kuna watu ambao wanajiita Wakristo na nafsi zao zimeshiba dini na madhehebu yao, wako tayari kuchinjwa kwa ajili ya kufia madhehebu yao, lakini kamwe hawajui kilichoandikwa kwenye Biblia, wao wamekaririshwa historian a heresies na viongozi wao wa madhehebu, kwa hiyo itikadi za dhehebu ndizo wanazodhani ni fundisho la Neno la Mungu, hawa ni wasumbufu, wanasimamia wasivyovijua, na watakwambia viko kwenye Biblia wakati ukweli ni kwamba havipo na havijawahi kuwepo.
Hapa ninakuja na somo kuhusu IBADA ZA WAFU. Ibada hizo ziko sehemu mbili, ya kwanza ni ile ya kuwaomba Watu (au watakatifu) waliokufa zamani nay a pili ni ile ya kuwaombea watu waliokufa. Kwa mujibu wa Neno la Mungu ibada zote hizi mbili hazikubaliki na neno la Mungu.
KUWAOMBEA WAFU
Mnamo tarehe 24 Januari 2013, Askofu mmoja wa dhehebu fulani hapa Dar es salaam aliwahi kusema kwamba Kanisa linawaombea marehemu ili WATAKASWE, IKIWA WANAHITAJI KUTAKASWA kabla ya kupokelewa mbinguni wakati miili yao inapobaki ardhini ikingoja kurudi kwa Kristo na ufufuko wa wafu.
Hii ndiyo sababu kanisa linatolea sadaka ya misa kwa ajili ya marehemu. Pia kanisa linasali na kuwaombea marehemu kusudi wapate msaada wa kiroho na waamini walio bado hai wapate matumaini ya uzima ujao mbinguni
KATIKA KAULI HII YA ASKOFU HUYU TUNAPATA YAFUATAYO;
1. Anakiri kwamba Kanisa huwa linawaombea wafu
2. Anakiri kwamba Kanisa huwa linatoa sadaka kwa ajili ya marehemu
ISAYA 34:16 inasema Tafuteni katika kitabu cha Bwana mkasome.. Tutafute kwenye Kitabu cha Bwana yaani Biblia, tuone, Je, kuna mahali popote Biblia imewahi kuagiza kuombea wafu?
Na YEREMIA 6:16 inasema Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo
Swali langu hapa ni hili, je, kuna tukio lolote la mtu aliyekufa kuwahi kuombewa kwenye Biblia? Twende tusimame katika njia kuu, tuone, tuulize habari za mapito (walioenenda) zamani, je, kuna mtu aliyewahi kufa kwenye Biblia akaombewa ili atakaswe?
Wako watu ambao hawatakosa majibu, hata hivyo sidhani kama majibu yao yatazidi mawili, ambayo ni, kwanza watasema wafu ambao Yesu aliwaombea na Dorcas aliyeombewa na Petro. Katika hili itakuwa ni matumizi mabaya ya muda kujadili suala hili la Yesu kuombea wafu kama Binti Yairo, Lazaro na wengine. Ukweli ni huu, hawa watu hawakuombewa ili dhambi zao zitakaswe, waliombewa ili warudi katika maisha haya (uhai).
Jibu la pili wanaweza kujibu hivi; watasema kuwa maagizo ya kuombea wafu na kutoa sadaka kwa ajili ya dhambi za wafu yanapatikana kwenye VITABU VYA MAKABAYO; wako wanaodai kuwa vitabu hivi ni vitabu vya Biblia vilivyopotea.
Ukweli ambao wengi hawaujui na wataendelea kufichwa ni huu; vitabu hivi havikuwahi kupotea, isipokuwa vilikataliwa kwa sababu HAVIKUWA NA UVUVIO wa KIMUNGU zaidi ya hadithi na simulizi za kweli zilizowahi kutokea zamani. Simulizi hizi zinawahusu mashujaa wa zamani wa KIYAHUDI walioitwa MAKABAYO.
Katika Kitabu 2MAKABAYO 12:43-46: kwa kiingereza inasema hivi "And making a gathering, he [Judas] sent twelve thousand drachms of silver to Jerusalem for sacrifice to be offered for the sins of the dead, thinking well and religiously concerning the resurrection, (For if he had not hoped that they that were slain should rise again, it would have seemed superfluous and vain to pray for the dead,) And because he considered that they who had fallen asleep with godliness, had great grace laid up for them. It is therefore a holy and wholesome thought to pray for the dead, that they may be loosed from sins."
Nimeipata hii kwa Kiingereza, maana sina vitabu hivyo kwa Kiswahili.
Hapa ndipo baadhi ya watu wanachukulia fundisho la kuombea wafu kuwa ni sahihi; lakini sio kweli, kwa sababu kitabu hiki na vingine vine sio vitabu vya BIBLIA. Vilikataliwa kuingizwa katika orodha ya vitabu vya Biblia kwa sababu vilijaa hadithi kuliko uvuvio wa ROHO MTAKATIFU. Ziko sababu zaidi ya 21 za vitabu hivi kukataliwa, lakini kwa sababu sio somo lake, tuendelee na kuangalia kwa nini MISA ZA KUOMBEA WALIOKUFA NI IBADA ZA KIPAGANI.
WAEBRANIA 9:27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu Kumbe mtu anapokata roho tu anakutana na hukumu yake instantly, kuwaambia watu eti wamuombee na kumtolea marehemu sadaka ili atakaswe ni kuwaibia watu pesa zao na tena ni kuwaibia muda wao.
UFUNUO WA YOHANA 14:13 inasema Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, HERI WAFU WAFAO KATIKA BWANA TANGU SASA. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao
Yesu anajua fika kwamba, hakuna nafasi ya mtu kutengeneza na Mungu baada ya kufa, baada kuachana na maisha haya ya duniani, ndio maana anatangaza kwenye andiko hilo, ili watu wajiandae wakiwa bado duniani, na ni angalizo kwa wale ambao wanangoja kuingia Mbinguni kwa lifti ya sala za marehemu.
JE, KUNA MAHALI PANAITWA PUGATORI?
Kuna dini zinafundisha kwamba kuna sehemu inaitwa purgatory au toharani ambapo mtu anapokufa huenda huko kwanza, na wakati ndugu, jamaa na marafiki wanamuombea huku duniani dhambi zake zinatakaswa kule aliko, na zikishatakaswa zote ndipo sasa anaweza kupokelewa na Mungu. Na ili kutakaswa kwake kuwe kwa haraka, kuna pesa ambayo inatakiwa kutolewa kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya marehemu.
NI AJABU SANA!!! kama mambo haya yangekuwa ya kweli sioni ni kwa nini Yesu alikuja kupoteza muda wake hapa duniani ahubiri Injili ya watu kutubu na kuacha dhambi wakiwa bado wako duniani. Sioni ni kwa nini basi aliacha heshima na Utukufu Mbinguni kama dhambi zingekuwa zinaondolewa kwa shilingi za Tanzania au dola za Kimarekani, Yen ya Japan na Faranga za Kifaransa.
Kwenye Biblia hakuna kitu kinaitwa PURGATORI, HAKUNAAAA!!!!!! Inasadikiwa kwamba Gregory ndiye aliyeanzisha uzushi huu na wengi wakaufuata baadae. Hii ni kama miradi ya watu kujipatia Pesa kutoka kwa masikini na matajiri. Na YESU aliliona na akaonya katika MATHAYO 23:14 akisema;
[Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapata hukumu iliyo kubwa zaidi.]
NDUGU ZANGU: Sadaka za misa za wafu haziwezi kutusaidia, ZABURI 49:6-7 inasema hivi Wa hao wanaozitumainia mali zao, Na kujisifia wingi wa utajiri wao; Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake, Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake
WARUMI 6:23 inasema Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu Je, ni lini pesa ya mtu inaweza kutakasa dhambi ya mtu kama hakutakaswa na damu ya Yesu alipokuwa duniani?
NUSU HITIMISHO:
Misa za kuwaombea wafu, au arobaini, au hitima ya msiba, kama zinahusisha masuala ya kuombea watu waliokufa hizo ni ibada za KIPAGANI na sio ibada za Wakristo. Haijalishi zinafanywa na nani, ana wadhfa gani na ni maarufu kiasi gani. Ukweli ni kwamba sala hizi hazipo kwenye Maandiko Matakatifu.
MBINGUNI HAKUNA LIFTI: Yesu alikuja duniani ili tuhubiriwe, tutubu, maombi ya waliobaki duniani hayawezi kuwa lifti ya mimi kuingia Mbinguni kama nilikufa katika maisha ya dhambi.
Sadaka za kutoa kwa ajili ya kuwaombea marehemu ni batili, ni watu wasiojua maandiko ndio watakaoendelea kuliwa, maana tumesoma katika ZABURI 49:6-7 Wa hao wanaozitumainia mali zao, Na kujisifia wingi wa utajiri wao; Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake, Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake
AKILI KICHWANI KWAKO,
SEHEMU YA PILI YA SOMO HILI ITAFUATA.
MLIMA WA MAKIMBILIO - BOKO Basiyaya (Basihaya??)
DAR ES SALAAM TANZANIA