Ndiyo trend za habari zilivyo Tanzania, angalia YouTube, Instagram, Facebook na mitandao ya kijamii habari ndiyo hizo pongezi kwa kupata ulaji, tanzia, mazishi, skandali za ma-celeb, 'mzungu' n.k lakini habari za kina, uchambuzi na kuelimisha ni chache sana.
Habari za kutokea Tanzania ni za kijamii zaidi tena za mtaa.
Upo umuhimu wa kuwa na mchanganyiko wa habari zaidi motomoto za kila aina ikiwemo hizo zinazo trendi sana kwa sasa zile zetu za kijamii, kidini na kiimani kama kishirikina n.k
Tunajua utamaduni wetu unaegemewa wapi lakini tujiongeze katika suala la matumizi mapana ya mitandao, vyombo vya habari na TEHAMA .