Kwa nini uchaguzi wa CHADEMA ngazi ya Taifa uliteka watu wengi vile?

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
Uchaguzi wa viongozi wa CHADEMA Taifa uliteka watu wengi mithili ya uchaguzi Mkuu wa Nchi.

Uliteka kuanzia vijana, wazee, akina baba, akina mama, Watanzania wote pamoja na watu wa mataifa mbalimbali. Usiku ule watu wengi hawakulala wakisubiri matokeo yatangazwe. Hata mimi nilikesha nikifuatilia matokeo.

Soma Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Lakini pia nilichogundua kingine ni kwamba, viongozi wa serikali hata waitishe Press hakuna anayeshobokea lakini Lissu akiitisha Press asilimia kubwa ya Watanzania wanakuwa hewani kufuatilia kinachojiri.

Je, ni kwamba viongozi wetu wa serikali wamekosa mvuto kwa Watanzania kiasi hicho?
 
Ilikua ni Tanganyika dhidi ya CCM ya zanzibar iuzayo Mali za tanganyika na kujifaidisha!

Nadhani wenye nchi walitaka wapate mtetezi asie na bei Ili a push ajenda zao kuu ambazo mwenyekiti wa CCM amezibagaza badala ya kutekeleza kwa usahihi kama wenye nchi walivyotaka atekeleze!!

Wote tunaimba "No reform no election"!
 
Ulitrend kwa sababu ulijaa kutukanana. Ni kama vile bifu za kina mwijaku vs babalevo au j lokole vs mobetto uwa zinakamata mitandao.
 
Ilikua ni Tanganyika dhidi ya CCM ya zanzibar iuzayo Mali za tanganyika na kujifaidisha!

Nadhani wenye nchi walitaka wapate mtetezi asie na bei Ili a push ajenda zao kuu ambazo mwenyekiti wa CCM amezibagaza badala ya kutekeleza kwa usahihi kama wenye nchi walivyotaka atekeleze!!

Wote tunaimba "No reform no election"!
Hakika. Hata mimi naunga mkono kaulimbiu ya No reform no election. Mimi nadhani CHADEMA wasikubali hata kidogo kuingia kwenye uchaguzi bila kufanyika Reforms za msingi zinazofanya uchaguzi uwe huru, haki na wa wazi.
 
Uchaguzi wa viongozi wa CHADEMA Taifa uliteka watu wengi mithili ya uchaguzi Mkuu wa Nchi.

Uliteka kuanzia vijana, wazee, akina baba, akina mama, Watanzania wote pamoja na watu wa mataifa mbalimbali. Usiku ule watu wengi hawakulala wakisubiri matokeo yatangazwe. Hata mimi nilikesha nikifuatilia matokeo.

Soma Pia: Yanayojiri Uchaguzi Mkuu CHADEMA 2025: Tundu Lissu ashinda nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA Taifa kwa Kura 513 sawa na 51.5%

Lakini pia nilichogundua kingine ni kwamba, viongozi wa serikali hata waitishe Press hakuna anayeshobokea lakini Lissu akiitisha Press asilimia kubwa ya Watanzania wanakuwa hewani kufuatilia kinachojiri.

Je, ni kwamba viongozi wetu wa serikali wamekosa mvuto kwa Watanzania kiasi hicho?
Huyo anayeshobokewa na watu wengi zaidi akiitisha conference, huyo ndiye rais wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom