Mimi nafikiri niko tofauti kidogo kwani naona kwangu ndoa ni TAMU kuliko maisha ya uchumba. Yako mambo mazuri na matamu ambayo nisingeweza kumfanyia mke wangu au yeye kunifanyia wakati wa uchumba lakini leo tunafanyiana.
Hata hivyo ninaelewa point yako ambayo inatokana na watu kusahau ule upendo wao wa kwanza kwa wenzi wao. Kinachotakiwa ni kuwa unayemuoa/unayeolewa naye awe ni chaguo lako pekee la moyo wako na hakuna kumegana/kuonjana kabla ya kufunga ndoa. Huu utakuwa msingi mkubwa.
Ifike mahali hata kama Mungu angetoa ruhusa ya kuvunja ndoa zote na akaruhusu watu kuoana/kufunga ndoa upya na kutoa uhuru wa umchague umtakaye bado uwe RADHI na UTAMANI kuoana na huyo aliyekuwa wako.
Ninamshukuru Mungu kuwa kwa ndoa yangu ya miaka tisa bado mke wangu ni mzuri na mtamu kwangu na sitamani nimkose hata siku moja kwa hiyo siko miongoni mwa wale wanaotamani kukimbia ndoa.