Kwa nini Uchumi unakuwa kwa 7% huku wananchi wako katika hali ngumu?

Kwa nini Uchumi unakuwa kwa 7% huku wananchi wako katika hali ngumu?

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
1576476928745.png
Wanajamvi, leo nimeona niandike kidogo kuhusu hili swala ambalo kwa muda mrefu watu wamekuwa wakililalamikia hata kufikia hatua ya kukataa ukuaji wa uchumi ambao unatangazwa na NBS.

Lakini ni vyema kujua kuwa, wanaposema uchumi umekuwa, ni kweli uchumi umekuwa, kitu ambacho mwananchi anaweza kukiona ni maendeleo ya uchumi. Ukuaji wa uchumi ni moja kati ya necessary condition ya maendeleo ya uchumi.

Hivyo basi, Ukuaji wa uchumi upo kwa kuwa wenyewe ni quantitative, na huwa ukuaji wa uchumi (Economic Growth) hauchukuliwi sana kama kigezo cha kuonyesha maendeleo ya uchumi. Lakini Maendeleo ya uchumi ni qualitative.

Hapa niweke kwa kiingereza kidogo, Economic growth is quantitative increase of national Income ambayo hii hupimwa kwa hiyo GDP, Gross Domestic Product. Economic development is redistribution of GDP/Economic growth to increase the real freedoms of the people.

Kwa hiyo basi tusishangae ule ukuaji unaohubiriwa bali tuhoji jinsi ukuaji huwa unavyokuwa redistributed ili mwananchi aweze kuishi kwa raha.
 
Back
Top Bottom