Kwa nini ukitongoza msichana/mwanamke unaye ishi nae mtaa mmoja anakukataa ?

Kwa nini ukitongoza msichana/mwanamke unaye ishi nae mtaa mmoja anakukataa ?

jamaikatz

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2023
Posts
400
Reaction score
1,429
Katika harakati zangu za kujitafuta nimesha hamia mitaa mingi lakini kila ninapo hamia kwenye huo mtaa huwa nakutana na vibinti vingi + wanawake wengi pamoja na mishangazi ,

Ila kila nikijaribu kushusha swagga napigwa chini sasa huwa najiuliza shida nini , lakini nikienda Mitaa ya jirani ,huwa nashobokewa sana na mademu kibao

Lakini nikisema nitongoze mtaani kwangu nakataliwa sasa sijui nafeli wapi , kama kupendeza, napendekeza nguo nabadilisha kila siku , muonekano ninao ila Dah???!!

Nipeni mbinu wadau au ndo nabii hakubaliki kwao😥 ?
 
ACHA NGONO MKUU NDIO MAANA HAUENDELEI
285ff89b5e892abe3ee3ed4202906ff2 (1).jpg
 
Katika harakati zangu za kujitafuta nimesha hamia mitaa mingi lakini kila ninapo hamia kwenye huo mtaa huwa nakutana na vibinti vingi + wanawake wengi pamoja na mishangazi ,

Ila kila nikijaribu kushusha swagga napigwa chini sasa huwa najiuliza shida nini , lakini nikienda Mitaa ya jirani ,huwa nashobokewa sana na mademu kibao

Lakini nikisema nitongoze mtaani kwangu nakataliwa sasa sijui nafeli wapi , kama kupendeza, napendekeza nguo nabadilisha kila siku , muonekano ninao ila Dah???!!

Nipeni mbinu wadau au ndo nabii hakubaliki kwao😥 ?
Sasa demu ana mabwana 12 toka mitaa ya mbali, akikubalia wewe wa jirani itakuwa ngumu kuwapanga.
 
1.Anahisi hauna “mystery” au mvuto wa kipekee

Kwa kuwa mnaishi mtaa mmoja, anaweza kukuona kila siku, hivyo hana ule msisimko au mvuto wa mtu mpya. Anahisi tayari anakujua vya kutosha, na kwa hivyo haoni “kile cha kipekee” kinachomvutia.


2. Anaogopa maneno ya mtaa (umbea/majungu)

Wanawake wengi wanaepuka kuanzisha uhusiano na mtu wa karibu kwa sababu watu wa mtaa wanaweza kuanza kuzungumza. Anaweza kuhofia aibu, chuki au maneno ya watu yakiharibu heshima yake.


3. Anakujua sana — labda hajakuvutiwa hata kabla ya kutongoza

Kwa sababu mnaishi karibu, anaweza kuwa tayari ana mtazamo juu ya tabia yako, mwenendo wako au maisha yako. Ikiwa anaona mambo fulani hafai, hata kama hujui, hiyo inaweza kuwa sababu ya kukukataa.


4. Ana mtu mwingine tayari

Anaweza kuwa kwenye uhusiano mwingine, hata kama haujulikani wazi. Na kwa kuwa uko karibu, anaweza kuona si salama kuwa na mahusiano ya karibu na watu wa mtaa ikiwa tayari amecommit kwa mtu mwingine.


5. Anaogopa ukiachana naye maisha yatakuwa magumu (kwa kuwa mko karibu)

Kuanzisha uhusiano na mtu wa karibu kunaweza kufanya mambo kuwa magumu zaidi kama kutatokea kuvunjika kwa uhusiano. Wengine huchagua “kutochanganya mchele na maharagwe” kwa kuogopa migogoro ya baadae.


6. Hana hisia zako (simple reason)

Pengine hajakukubali kwa sababu tu hana hisia zako. Hii inaweza kuwa sababu ya kawaida kabisa, bila sababu nyingine yoyote ya kina.
 
Utahama mitaa 100 ila shida ni ile ile
Lengo lako ni nini?😎
 
Kuwa na demu ambaye wote mnaishi mtaa mmoja ni miyeyusho mkuu..
 
Back
Top Bottom