Kweli kabisa wanadharaulika sana tena mno utakuta mzazi anamwambia mwanae umekosa vyuo vyote umeshindwa hata kwenda ualimu? Inaonyesha ni kazi ya watu wa hali ya chini na ndo maana mishahala yao ipo chini hata ukiwa na degree utaambulia mshahala kiduchu sana.Ni taaluma inayo dharauliwa sana kuanzia serikalini mpaka kwenye jamii.
Kitu kingine walimu wenyewe wamekuwa wapole mno kudai haki zao za msingi wao wapo wengi sana wanaweza goma au kushinikiza serikali kuwalipa vizuri.
wajameni, nimejaribu kufikia kwa muda mrefu kidogo sababu inayopelekea waalimu wetu (hasa wa shule za msingi) kudharaulika. Nimeshindwa kujua ni kwa nini waalimu wanaonekana kama watu wasio na hadhi kubwa kwa jamii yetu? Wamepewa majina tofauti na hata wakati mwingine utasikia "una nguo moja kama mwalimu!" au "uso umekupauka kama mwalimu"
Serikali nayo kwa upande wake, inawaona sijui kama nini! Mishahara yao na wajibu wao kwa jamii haulingani. Hivi tatizo ni nini hasa?
wajameni, nimejaribu kufikia kwa muda mrefu kidogo sababu inayopelekea waalimu wetu (hasa wa shule za msingi) kudharaulika. Nimeshindwa kujua ni kwa nini waalimu wanaonekana kama watu wasio na hadhi kubwa kwa jamii yetu? Wamepewa majina tofauti na hata wakati mwingine utasikia "una nguo moja kama mwalimu!" au "uso umekupauka kama mwalimu"
Serikali nayo kwa upande wake, inawaona sijui kama nini! Mishahara yao na wajibu wao kwa jamii haulingani. Hivi tatizo ni nini hasa?
Pamoja na mambo yote yaliyosemwa na wadau wengine hapo juu, walimu hawatekelezi wajibu wao ipasavyo. Walimu wengi hawafundishi ipasavyo, wanashiriki kufanya maovu(Si mfano wa kuigwa na jamii), hawatekelezi kazi zingine za kiualimu. Kwa hali hiyo walimu wataendelea kudharauliwa tu.Msongoru
Nafikiri umeuliza swali la msingi sana kuhusu hali ya walimu nchini Tanzania. Kuna vitu kadhaa hapa vya kujiuliza, wakati wa Nyerere aliweka wazi kabisa kwamba ualimu ni wito, lakini sote tuliona ni kwa kiasi gani Mwalimu alikuwa anaonekana ana thamani kumshinda mtumishi mwingine yeyote wa serikali. Pale vichaa walipochukua nchi na kuanza kumwona mwalimu ndo wa kumpunja mafao, mwalimu ndo wa kumcheleweshea mishahara, mwalimu ni profession unayoweza kusoma kwa miezi mitatu, ualimu ni profession unayoweza kusomea hata kama utakuwa na zero kama ambavyo ilifanyika wakati wa kuanza ule mpango wa MMES and the like ndipo hapo watu wanapojifunza kwamba kumbe hata fulani, kilaza kabisa na yeye amekuwa mwalimu, basi ualimu ni profession ya kila mtu hata mbumbu tu. Hapo ndipo tulipoanzia.
Na pengine kitu ambacho kinawafanya walimu waendelee kuonekana wapuuzi na waliokosa mwelekeo ni ulimbukeni mkubwa walionao, wa kutokuwa tayari kushirikiana kudai kilicho chao. Wanakubaliana wote tugome, lakini utasikia Mtwara walimu waliendelea kufundisha kama kawaida. Sasa hicho ni nini? Yaani walimu watadharaulika hata zaidi ya hivi wanavyodharaulika sasa. Kwa kuwa hawana umoja na wala hawana mpango wa kufuatilia na kujua haki zao kama raia wa tanzania na kama wafanyakazi. Hivi unamlipa mwalimu shilingi l50,000 hapo anaishi Dar, amepanga nyumba, ana watoto wanasoma na anahitaji chakula. Unategemea nini? Na bado wakati wa kampeni watageuzwa mabango ya CCM au ndiyo waandikishaji wa wapiga kura au wahesabiaji wa kura za CCM na watakuwa mstari wa mbele kupiga makofi kuwashangilia haohao wanaowafanya waishi maisha hayo wanayoishi.
Sisi walimu ni Wehu. Nikiwemo na mimi mwenyewe ambaye pia ni Mwalimu. Somewhere I read an article somebody wrote: "Ualimu Tanzania, ni headache??" Huwa napenda sometime kuexplore mambo ya elimu na huwa navutiwa kusoma issue zinazohusu elimu kutoka kwenye blog hii inayoitwa Elimu ya Tanzania na Mustakabli wa Taifa. Mnaweza kutembelea hapa: http://vangidunda.blogspot.com/2010/02/ualimu-tanzania-ni-headache.html muone jamaa anavyokomend kuhusu ualimu Tanzania, na Elimu ya Tanzania kwa ujumla.
Regards
mkuu unamaana wanalipwa kidogo kwa sababu hawatekelezi majukumu yao vilivyo?unataka kusema wabunge au watumishi wengine wanalipwa vizuri kwa sababu wana tekeleza wajibu wao vizuri na wanajieshimu? Na hapa kujieshimu mkuu una maana gani? sidhani kama hizo ndo sababu za walimu kutolipwa vizuri. ofisi za umma nyingi tumetembelea pengine unaweza kukuta walimu wanajitahidi kutoa huduma kwenye mazingira magumu kuliko mtu yeyote.May be kwa sababu watu waliofeli ni wengi kama watu wanadhani kupewa ajira ni kama kupendelewa tu na si haki yao.yaani hawajiamini vile. Kumbuka waziri mwantumu maiza aliwambia kama malipo ni kidogo si waache kusomea ualimu! wao kimya. Ukiwambia walimu wa kenya hivyo moto utawaka na lazima utajiuzulu tu.Wakati mwingine naunga EAC waje wawazindue hawa watumishi wetu. Na serikali yetu lazima ijiandae kwa hilo. Ni kama wananchi wa vijijini vile ambao hawajui wajibu wa serikali kwao. Hata kuji-organize kudai haki au kukataa kudharauliwa na waziri wao wanaona ni poa tu.Mishahara ya walimu na watumishi wengine ni sawa tu tena ya ualimu inazidi kidogo.TGSD ya ualimu aliye maliza chuo kikuu ni kubwa kidogo na GSD ya idara nyingine kwa Takriba Tsh1000. Lakini Per Day, Semina, Workshop, posho za kazini, gharama kodi za nyumba, matibabu usafiri nk hawa wenzetu hawana. Ukirejea pesa za budget zinazopitishwa bungeni haya mafungu yana-count kuliko mishahara.watumishi wengine wanamafungu haya. Walimu wanaambiwa zimeunganishwa humo humo wakati si kweli kwa sababu TGSD anayopewa na wa idara nyingie ni sawa wakati yule wa idara nyingie yuko legible kwa posho kibao.wenyewe kazini hakuna hata hizi chai za asubuhi. Nyumba miaka ya nyuma enzi za nyerere zilikwepo kwa sasa serikali inafahamu kabisa walimu wanapanga uraiani kama walivyo askari, manesi na watumishi wengine. wengine hao wanalipwa kodi za nyumba hata ma-lecture wametoa muda pesa za kodi za nyumba zilipwe haraka na juzi tu tanesco mumeona wanatoa units 750 kwa wafanyakazi wake. Hapo ndo umaskini wao unapoanzia. Walimu wanafahamu na hawadai vitu hivyo. Kenya wanapata kodi ya nyumba, afya, na zimeanishwa. Makato mengine ya PAYE, bima ya Afya, Ada ya ualimu, nazo ni kubwa mno.Pamoja na mambo yote yaliyosemwa na wadau wengine hapo juu, walimu hawatekelezi wajibu wao ipasavyo. Walimu wengi hawafundishi ipasavyo, wanashiriki kufanya maovu(Si mfano wa kuigwa na jamii), hawatekelezi kazi zingine za kiualimu. Kwa hali hiyo walimu wataendelea kudharauliwa tu.
Walimu wakitaka kuheshimiwa wajiheshimu wao kwanza kwa kufuata maadili ya ualimu kisha washikamane kudai maslahi zaidi katika kazi.
mkuu unamaana wanalipwa kidogo kwa sababu hawatekelezi majukumu yao vilivyo?unataka kusema wabunge au watumishi wengine wanalipwa vizuri kwa sababu wana tekeleza wajibu wao vizuri na wanajieshimu? Na hapa kujieshimu mkuu una maana gani? sidhani kama hizo ndo sababu za walimu kutolipwa vizuri. ofisi za umma nyingi tumetembelea pengine unaweza kukuta walimu wanajitahidi kutoa huduma kwenye mazingira magumu kuliko mtu yeyote.May be kwa sababu watu waliofeli ni wengi kama watu wanadhani kupewa ajira ni kama kupendelewa tu na si haki yao.yaani hawajiamini vile. Kumbuka waziri mwantumu maiza aliwambia kama malipo ni kidogo si waache kusomea ualimu! wao kimya. Ukiwambia walimu wa kenya hivyo moto utawaka na lazima utajiuzulu tu.Wakati mwingine naunga EAC waje wawazindue hawa watumishi wetu. Na serikali yetu lazima ijiandae kwa hilo. Ni kama wananchi wa vijijini vile ambao hawajui wajibu wa serikali kwao. Hata kuji-organize kudai haki au kukataa kudharauliwa na waziri wao wanaona ni poa tu.Mishahara ya walimu na watumishi wengine ni sawa tu tena ya ualimu inazidi kidogo.TGSD ya ualimu aliye maliza chuo kikuu ni kubwa kidogo na GSD ya idara nyingine kwa Takriba Tsh1000. Lakini Per Day, Semina, Workshop, posho za kazini, gharama kodi za nyumba, matibabu usafiri nk hawa wenzetu hawana. Ukirejea pesa za budget zinazopitishwa bungeni haya mafungu yana-count kuliko mishahara.watumishi wengine wanamafungu haya. Walimu wanaambiwa zimeunganishwa humo humo wakati si kweli kwa sababu TGSD anayopewa na wa idara nyingie ni sawa wakati yule wa idara nyingie yuko legible kwa posho kibao.wenyewe kazini hakuna hata hizi chai za asubuhi. Nyumba miaka ya nyuma enzi za nyerere zilikwepo kwa sasa serikali inafahamu kabisa walimu wanapanga uraiani kama walivyo askari, manesi na watumishi wengine. wengine hao wanalipwa kodi za nyumba hata ma-lecture wametoa muda pesa za kodi za nyumba zilipwe haraka na juzi tu tanesco mumeona wanatoa units 750 kwa wafanyakazi wake. Hapo ndo umaskini wao unapoanzia. Walimu wanafahamu na hawadai vitu hivyo. Kenya wanapata kodi ya nyumba, afya, na zimeanishwa. Makato mengine ya PAYE, bima ya Afya, Ada ya ualimu, nazo ni kubwa mno.
Very serious comment NonoWalimu walianza kudharaulika tangu pale serikali ya ccm ilipoona kuwa elimu sio kipaombele cha taifa hili.
Pale walipoona kuwa awaye yote anaweza kuwa mwalimu ili mradi amemaliza darasa la saba (msingi) na kidato cha nne (form 4). Walipoona kuwa mwalimu anaweza kuandaliwa kwa miezi mitatu (upe na voda faster sasa). Lakini kubwa zaidi tumejengewa ndani ya taifa hili na tumeendelea kukubaliana na mfumo huu chakavu na matokeo yake fani pekee yenye thamani Tanzania ni Siasa kwani utakufikisha kwenye ufisadi mapema.
nilikuwa na maana ya mchango wa chama cha walimu mkuu.Hivi wenzetu waalimu pia wanatakiwa kulipa ada? ndio ipi hiyo mkuu? I'm ignorant of that.