Msongoru
Nafikiri umeuliza swali la msingi sana kuhusu hali ya walimu nchini Tanzania. Kuna vitu kadhaa hapa vya kujiuliza, wakati wa Nyerere aliweka wazi kabisa kwamba ualimu ni wito, lakini sote tuliona ni kwa kiasi gani Mwalimu alikuwa anaonekana ana thamani kumshinda mtumishi mwingine yeyote wa serikali. Pale vichaa walipochukua nchi na kuanza kumwona mwalimu ndo wa kumpunja mafao, mwalimu ndo wa kumcheleweshea mishahara, mwalimu ni profession unayoweza kusoma kwa miezi mitatu, ualimu ni profession unayoweza kusomea hata kama utakuwa na zero kama ambavyo ilifanyika wakati wa kuanza ule mpango wa MMES and the like ndipo hapo watu wanapojifunza kwamba kumbe hata fulani, kilaza kabisa na yeye amekuwa mwalimu, basi ualimu ni profession ya kila mtu hata mbumbu tu. Hapo ndipo tulipoanzia.
Na pengine kitu ambacho kinawafanya walimu waendelee kuonekana wapuuzi na waliokosa mwelekeo ni ulimbukeni mkubwa walionao, wa kutokuwa tayari kushirikiana kudai kilicho chao. Wanakubaliana wote tugome, lakini utasikia Mtwara walimu waliendelea kufundisha kama kawaida. Sasa hicho ni nini? Yaani walimu watadharaulika hata zaidi ya hivi wanavyodharaulika sasa. Kwa kuwa hawana umoja na wala hawana mpango wa kufuatilia na kujua haki zao kama raia wa tanzania na kama wafanyakazi. Hivi unamlipa mwalimu shilingi l50,000 hapo anaishi Dar, amepanga nyumba, ana watoto wanasoma na anahitaji chakula. Unategemea nini? Na bado wakati wa kampeni watageuzwa mabango ya CCM au ndiyo waandikishaji wa wapiga kura au wahesabiaji wa kura za CCM na watakuwa mstari wa mbele kupiga makofi kuwashangilia haohao wanaowafanya waishi maisha hayo wanayoishi.
Sisi walimu ni Wehu. Nikiwemo na mimi mwenyewe ambaye pia ni Mwalimu. Somewhere I read an article somebody wrote: "Ualimu Tanzania, ni headache??" Huwa napenda sometime kuexplore mambo ya elimu na huwa navutiwa kusoma issue zinazohusu elimu kutoka kwenye blog hii inayoitwa Elimu ya Tanzania na Mustakabli wa Taifa. Mnaweza kutembelea hapa:
http://vangidunda.blogspot.com/2010/02/ualimu-tanzania-ni-headache.html muone jamaa anavyokomend kuhusu ualimu Tanzania, na Elimu ya Tanzania kwa ujumla.
Regards