PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,689
- 25,848
1. Maandiko yalilenga imani na ukombozi wa Waisraeli, si historia ya Misri.Kwa kipindi kirefu na hata mpaka leo hii watu wengi sana wanashangazwa na piramidi za kale za Misri. Kuna mjadala mkubwa sana jinsi zilivyojengwa, ni nani waliozijenga na walipata hiyo teknolojia ya ujenzi. Piramidi ni sehemu ya maajabu saba makubwa zaidi ya dunia.
Jambo la kushangaza ni kwamba Waisraeli katika maandiko yao ya agano la kale hawataji kabisa kuhusu mapiramidi.
Inawezekanaje Pyramids zikakosena katika maandiko ya watu waliokaa utumwani kwa mamia ya miaka huko Misri? Kwamba hilo jambo halikuwa kubwa, la kushangaza, kufikirisha na uzito kwao wa kutajwa katika vitabu vyao?! Kuna jambo haliko sawa.
2. Piramidi zilijengwa kabla ya kipindi cha utumwa wa Waisraeli.
3. Hakuna ushahidi kwamba Waisraeli walikuwa wa mwanzo kujenga na piramidi. Inawezekana Walihusishwa tu katika kuongezea mengine. Ila yalishakuwepo.
4. Piramidi zilihusishwa na dini za kipagani zisizofaa kwa simulizi za Waisraeli.
5. Ukimya unaouongelea kuhusu piramidi unadhihirisha msisitizo wa kiimani, si kihistoria