MADAI YA SERIKALI 3 NI MATUNDA YA UDINI NA UARABU. Kwa kiasi kikubwa wale vinara wa kudai Serikali tatu wanasukumwa, hasa mambo makuu mawili:
1. Kwanza, ni Wazanzibari wenye msimamo mkali, na ambao wengi wao wanadhani wakipata Serikali ya Zanzibar yenye mamlaka kamili wataweza kupata manufaa kutoka nchi za kiarabu.
2. Pili, ni Watanganyika wakristo (wenye msimamo makali wenye udini)
na ambao wengi wao wanadhani kwa kutengana na Zanzibar watapata
nguvu zaidi ya kukamata nchi kwa ukamilifu na watanufaika zaidi
kama dini, hawa wanadhani hivi sasa Wazanzibar wanawaletea kiza.
Hapa kibaya zaidi kampeni hizi zinaendeshwa hata kwenye nyumba za ibada, na upande mwingine hata baadhi ya viongozi wa kisiasa na wanataaluma wakubwa wenye kutegemewa wameshanaswa kwenye mtego huu. Hii ndiyo hali halisi tuwe waangalifu kuzicheza karata hizi tusifuate mkumbo. Ukiangalia mfano, waliokuwa viongozi wa G.55 na Mchngaji ‘Mtaka kesi' n.k. walitaka pawepo na Serikali ya Tanganyika kwa mlengo wao wa udini kwa upande wa Bara, na kwa upande wa Zanzibar kuna wafuasi wa iliyokua chama cha Hizbu na hivi sasa Uamsho wana mlengo wa kiarabu. Hivyo zinahitajika juhudi za ziada kujinasua hapa la sivyo hawa wenye uchu wanauua Muungano wetu mzuri kwa sababu ya Udini na Uarabu.