Kwa nini wajumbe wa CCM mabaraza ya Katiba wanang'ang'ania Serikali mbili?

Kwa nini wajumbe wa CCM mabaraza ya Katiba wanang'ang'ania Serikali mbili?

Kwa kweli sehemu kubwa ni unafiki wa kufuata mkumbo tu.
 
Mkuu, hivyo ndivyo walivyoelekezwa na wakubwa wao!! taifa likifika hapo ni hatari sana!! yaani wananchi hawatoi mawazo yao isipokuwa matakwa ya watu wachache kwenye uongozi wa juu wa chama tawala na hapa matokeo yake ni kwamba tutaandika katiba nyingine baada ya miaka michache sana, maana sioni Tanzania ya sasa ikiendelea na muungano wa nchi mbili!! Muundo huo ambao wanachama wa CCM wanautetea hata wao hawautaki isipokuwa wanyeje maana wakifanya kinyume vibarua vitaota nyasi!!!!

Inaoneka kweli kuwa ni maelekezo,haiwezekani watu wote hao watoe mawazo yanayofanana......
 
Pia hawaungi mkono serikali tatu kwa vile hawaielewi. Huwezi kuacha mke ambaye umeishi naye muda mrefu mkiwa mmepitia katika aina tofauti za mafanikio na matatizo hadi mmefikia takriban miaka 49. Bado mwaka mmoja tusherehekee Jubilei ya miaka 50 ya ndoa yetu. Leo hii mnaachana kwa kutegemea mwenza ambaye hamjuani. Au umeishi na mke mmoja kwa muda mrefu. Baada ya kuona kuwa migogoro ya ndani imezidi, we unakimbilia kuongeza mke wa pili eti ndo unatatua kero za ndoa ya kwanza. Huo si utakuwa ulofa?

Hili janga lingine unakuja na mfano wa hovyo wenye maudhi kbao.Mafanikio unayoyaongelea ni yapi au huo uwizi wenu uliotukuka na ujangili.Kama kutatua icho unachokiita ni mgogoro hata ikibidi kuoa uyo mke mwingine its better kwani mapinduzi yana garama.Je ayo mawazo si ndo demeokrasia kwani yalitolewa na raia walio wengi wewe kwa udikteta na mfumo mbofumbofu wa lichama lako hamuutaki.
 
Wengi kama sio wote kati ya wajumbe wa mabaraza ya Katiba Mpya toka CCM-kwa mujibu wa vyombo vya habari wanapingana na mapendekezo ya Tume ya Katiba ya Jaji Mstaafu J.S.Warioba kuwa Muundo wa Serikali Tatu na wanataka tuendelee na mbili kama ilivyo sasa kwa visingizio vya ajabu kama gharama,kwani sasa hawaoni jinsi serikali ya sasa inavyoendeshwa kwa gharama kubwa sana?
Simple! Kwa sababu wako more realistic. Wanajua wananchi wa Tanzania ni masikini, dawa mahospitalini bado shida, shule hazijawa na miundombinu, maji shida, mishahara midogo, wanashindwa hata kulipa shs. 1,000 ya kodi ya line ya simu kwa mwezi. Halafu uwaambie wagharamie serikali tatu, marais watatu, ikulu tatu, safari za nje marais watatu, ofisi mpya kutosheleza serikali tatu, mabunge matatu, maspika watatu, mahakama tatu, majeshi matatu, polisi tatu, kila kitu tatu...NANI ANAGHARAMIA? KODI KUONGEZWA KWA HUYU MWANANCHI MASIKINI! Nakubaliana nao, gharama hizi mwananchi hataziweza. Labda wananchi hawajaeleweshwa kwamba serikali tatu itakula kwao. serikali haina fedha - inatoza kodi tu - TOKA KWA WANANCHI. Halafu nyie wa bara itakula kwenu zaidi. Zbr watasema hawana uwezo kugharamia serikali ya muungano, kwa udogo wao, uchumi wao - watasema tutoe kama idadi ya watanzania ilivyo (1.3m vs 43.6m), wao watoe 3% ya gharama za serikali ya muungano, bara watoe 97%. Itabidi Bara tukubali ili muungano usivunjike, na hivyo wananchi wa bara tutaumia zaidi. Think twice.
 
Njaa mbaya wanahofu kupoteza tonge kwa mfumo wa serekali 3.

Kukiwa na serikali 3 maana yake patakuwa na Bunge tatu NA mojawapo ni Bunge la Tanganyika, ndani ya bunge hilo la Tanganyika kuna uwezekano mkubwa wa CCM asifikishe idadi ya wabunge wanaotakiwa kupitisha budget na upumbafu mwingine waliouzoea kwani hawatakuwa na wabunge wa CCM toka Zanzibar tena
 
Wengi kama sio wote kati ya wajumbe wa mabaraza ya Katiba Mpya toka CCM-kwa mujibu wa vyombo vya habari wanapingana na mapendekezo ya Tume ya Katiba ya Jaji Mstaafu J.S.Warioba kuwa Muundo wa Serikali Tatu na wanataka tuendelee na mbili kama ilivyo sasa kwa visingizio vya ajabu kama gharama,kwani sasa hawaoni jinsi serikali ya sasa inavyoendeshwa kwa gharama kubwa sana?

na je ni kwanini na wa chadema wanalilia serikali tatu
 
Simple! Kwa sababu wako more realistic. Wanajua wananchi wa Tanzania ni masikini, dawa mahospitalini bado shida, shule hazijawa na miundombinu, maji shida, mishahara midogo, wanashindwa hata kulipa shs. 1,000 ya kodi ya line ya simu kwa mwezi. Halafu uwaambie wagharamie serikali tatu, marais watatu, ikulu tatu, safari za nje marais watatu, ofisi mpya kutosheleza serikali tatu, mabunge matatu, maspika watatu, mahakama tatu, majeshi matatu, polisi tatu, kila kitu tatu...NANI ANAGHARAMIA? KODI KUONGEZWA KWA HUYU MWANANCHI MASIKINI! Nakubaliana nao, gharama hizi mwananchi hataziweza. Labda wananchi hawajaeleweshwa kwamba serikali tatu itakula kwao. serikali haina fedha - inatoza kodi tu - TOKA KWA WANANCHI. Halafu nyie wa bara itakula kwenu zaidi. Zbr watasema hawana uwezo kugharamia serikali ya muungano, kwa udogo wao, uchumi wao - watasema tutoe kama idadi ya watanzania ilivyo (1.3m vs 43.6m), wao watoe 3% ya gharama za serikali ya muungano, bara watoe 97%. Itabidi Bara tukubali ili muungano usivunjike, na hivyo wananchi wa bara tutaumia zaidi. Think twice.

Hizo gharama zinazosemwa mbona hazitolewi mchanganuo wake kuwa ni zipi?
 
CCM inatokana na muungano wa vyama vya Afro Shirazi Party cha Zbr na Tanu cha Tanganyika. Kuwahadaa Wazanzibari Nyerere aliamua chama kipya kiitwe cha mapinduzi, kufuatia kwa Zbr kuwa na Serikali ya Mapinduzi.

Kwa hiyo ccm wanaona kuwa kukiwa na serikali tatu, WaZbr lazima huko mbele watadai chama chao. Kwani already wameshajitoa ktk muungano baada tu ya kuizindua katiba yao mpya ambayo imewapa mamlaka kamili ya kiserikali.
Muungano uliopo sasa hivi ni wa vyama tu nilivyovitaja hapo juu, lkn wa serikali unalazimishwa tu na waroho wa madaraka kutoka Tanganyika.
Ccm wai- disable katiba ya Zanzibar ndiyo wawe na moral authority ya kulazimisha serikali 2
 
Kwa hiyo kwa vile sasa tunaendesha serikali kwa gharama unataka tuwe na serikali nyingine ili tuendeshe kwa gharama zaidi

Ebu tueleze hizo gharama zitakazoongezeka ni zipi?

Kwanza rasimu imeweka wazi kuwa baraza la mawaziri litakuwa dogo na hatutakuwa na makamu wa maraisi kama sasa tulivyo na makamu wa raisi watatu.

Ebu tupe sababu kama kweli haujakaririshwa na nape?
 
Simple! Kwa sababu wako more realistic. Wanajua wananchi wa Tanzania ni masikini, dawa mahospitalini bado shida, shule hazijawa na miundombinu, maji shida, mishahara midogo, wanashindwa hata kulipa shs. 1,000 ya kodi ya line ya simu kwa mwezi. Halafu uwaambie wagharamie serikali tatu, marais watatu, ikulu tatu, safari za nje marais watatu, ofisi mpya kutosheleza serikali tatu, mabunge matatu, maspika watatu, mahakama tatu, majeshi matatu, polisi tatu, kila kitu tatu...NANI ANAGHARAMIA? KODI KUONGEZWA KWA HUYU MWANANCHI MASIKINI! Nakubaliana nao, gharama hizi mwananchi hataziweza. Labda wananchi hawajaeleweshwa kwamba serikali tatu itakula kwao. serikali haina fedha - inatoza kodi tu - TOKA KWA WANANCHI. Halafu nyie wa bara itakula kwenu zaidi. Zbr watasema hawana uwezo kugharamia serikali ya muungano, kwa udogo wao, uchumi wao - watasema tutoe kama idadi ya watanzania ilivyo (1.3m vs 43.6m), wao watoe 3% ya gharama za serikali ya muungano, bara watoe 97%. Itabidi Bara tukubali ili muungano usivunjike, na hivyo wananchi wa bara tutaumia zaidi. Think twice.

Yani wewe ni kichwa maji kabisa tena kichwa maji mara tatu kama ulivyokaririshwa kuwa kila kitu ni tatu.

Back to the topic, Hizo mahakama tatu na majeshi matatu zitatoka wapi wakati rasimu imeonyesha majukumu ya serikali ya muungano ambayo ni pamoja kusimamia majeshi yote, mambo ya kimahakama, kielimu, kiafya na mengineo.

Na serikali ya Tanganyika na Zanzibar zenyewe zitakuwa zinajiusisha zaidi na mambo ya tamisemi na mengine kama hayo.
 
Mbili au moja haziwezekani tena,na tatu ni kuirejeshea zanzibr mamlaka yake kamili,kazi kwenu watanganyika kusuka au kunyoa,zanzbr kwanza.
 
Simple! Kwa sababu wako more realistic. Wanajua wananchi wa Tanzania ni masikini, simu kwa mwezi. Halafu uwaambie wagharamie serikali tatu, marais watatu, ikulu tatu, safari za nje marais watatu, ofisi mpya kutosheleza serikali tatu.

Kama ni kukwepa gharama basi tuwe na serikali moja kama unaona hoja yako ni ya msingi.
 
Wengi hamjaangalia suala hili kwa jicho la tatu ingawa mdau mmoja hapo juu kagusia. Hakuna suala la gharama wala kuondoa umoja wala nini! Ni kwamba zikiwepo serikali tatu,CCM bara na zanzbar zitakua na wakati mgumu kwenye chaguzi na kwenye kupitisha hoja mbalimbali bungeni. Ccm ina survive kwenye kupata kura nyingi za urais kupitia Zanzbar! Pia inafanikiwa kupitisha miswaada wanayoitaka pale bungeni kutokana na kuongezewa nguvu na wabunge wa wakilishi wa zanzbar ambako vyama kama CDM,CCR nk hawana wabunge!.Ikitokea kukawa na serikali ya Tanganyika, na ya zanzbar,wakati wa uchaguzi huku tanganyika,mpambano kati ya cdm na ccm utakua mkali kiasi bunge linaweza likawa na wabunge idadi sawa kati ya ccm na cdm na zanzbar pia ndio zaidi kwani CUF kinaweza kupata wabunge wengi kuliko ccm hivyo kufanya ndoto ya kutawala daima ife. Hicho ndicho wanachoogopa ccm tangia tupate uhuru!.Lakini pia mbona hamjajiuliza kama kweli ccm wanakataa serikali tatu kwa hoja ya gharama na kulinda umoja,mbona hawatetei serikali MOJA ili tupunguze zaidi gharama na umoja wetu ukomae zaidi? Hilo hawawezi ku advocate sababu walishakutana na kigingi zanzbar ambao asilimia kubwa hawataki serikali moja wala mbili!Wanaotaka serikali mbili zanzbar ni wana ccm tu kwa sababu nilizokwishaeleza,tena nao pia wamegawanyika wengine wanataka serikali tatu! Kwa cdm and others wanaotaka serikali tatu,the other way round is true!
 
Back
Top Bottom