carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Habari wakuu,
Ukiangalia miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa hivi karibuni nchini Tanzania kuanzia ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), barabara kuu, madaraja makubwa, hadi miradi ya nishati na maji utabaini kuwa sehemu kubwa ya zabuni za thamani kubwa zimekuwa zikienda kwa makampuni na wakandarasi kutoka nje ya nchi (kama vile kutoka China, Uturuki, na kwingineko).
Pamoja na uwepo wa makampuni mengi ya ndani na jitihada za Serikali kupitia Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) na Sheria ya Nunuzi za Umma kutoa kipaumbele kwa wakandarasi wa ndani , bado wakandarasi wa ndani wanapata sehemu ndogo sana ya miradi hii yenye thamani ya bilioni au triloni za fedha.
Hata hivyo, wadau wengi wa ujenzi wanahoji: Je, kweli wakandarasi wetu hawana uwezo, au wanakabiliwa na mfumo unaowabana?
Na kipi kifanyike kusaidia wakandarasi wa ndani waweze kuendeshe miradi mikubwa nchini Tanzania?