Haija chuja, kinacho tokea jf ni kama kwenye jamii tunazo ishi, kuna transformation kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Maisha tuliyo ishi 2009 ni tofauti na maisha tunayo ishi leo, hii ni kama dunia, watu, huja,wanachangamka wanachangia then wana potea ni kama kuzaliwa, kufa au kuhama.
Ukiangalia hata wazee wetu utaskia "enzi zetu maisha yalikuwa mazuri kweli" kila kizazi huwa kinahisi kiliishi wakati ulimwengu ulipo kuwa bora kabisa
Huwa nafukua nyuzi nyingi za zamani zilikuwa nzuri kwa kipindi chao lakin mimi naona kawaida kabisa, na siye tulio jiunga mwaka jana na mwaka huu at least na mwaka juzi tunaona tunaenda sawa tu.
Sitegemei mpaka mwaka 2023 sisi tuliko leo jf tutaiona ni nzuri pia, ila watakao jiunga mwaka 2022 jf ya mwaka 2023 itakuwa kitu bora zaidi.
Wanasema change is difficult but we all need it, jf ingeendelea kuwa ile ile ya mwaka 2009-2013 au 2014, ingeboa pia isingekuwa nzuri. Acheni waje watu wapya na idea mpya na generations zina change it is good.
naipenda jf hivi ilivo