Dr Restart
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 4,949
- 24,046
Amani iwe nanyi.
Mimi ni mmoja wa watumiaji wa mitandao ya kijamii, specifically Whatsapp. Katika matumizi hayo, napitia sana Status za marafiki pamoja na jamaa zangu.
Ninao jamaa ambao nawafahamu wanafanya kazi katika idara na majeshi husika. Japo hawapost mara nyingi, ila wanapopost huwa wanamweka Magufuli katika kurasa zao hizo, ikiambatana na caption mbakimbali kama Mwamba, emoji za machozi, nk
Ukifatilia trend, hata hapo majuzi wakati wa Sikukuu ya Noeli, video ya Magufuli ndiyo iliyotrend zaidi ya video ya Mh Rais Samia. Video ile ilisambazwa kwa wingi na sehemu kubwa ya Watumishi majeshi tajwa.
Watu hao katika post zao tisa kwa wastani, basi Mh Samia atapostiwa mara moja pekee au asipostiwe kabisa.
Sina shaka na kuwaamulia watu hao nini cha kupost, ila nina hamu kufahamu nini haswa kinawafanya wamkumbuke Rais Magufuli zaidi ya Mh Samia?
Katika kuwadodosa, wanasema wazi Magufuli aliboresha maisha yao na kuwapa meno kwa kiasi kikubwa..
Rais Samia kwa upande mwingine anaonekana kuwabana na kuwarudisha katika mstari wa kusimamia haki na kuwalinda Raia.
Je,nini haswa kinawafanya Wamkumbuke Rais Magufuli kuliko Amri Jeshi Mkuu wa sasa?
Kuna siri nyuma ya pazia ambayo hatuifahamu?