Jamani ivi ilo tatizo linasababishwa na nini?
Nawasilisha.
Mungu alipomuumba Adam aliona yafaa awe na msaidizi. Akamlaza usingizi akafanya upasuaji kwa kuchukua ubavu wa kushoto na kumtengeneza mwanamke wa kufanana na Adam. Waliishi vizuri tu kwa kukidhiana mahitaji baina na kati yao hadi pale Hawa alipokubali kudanganywa na Nyoka kupitia tamaa za Hawa. Naye kwa kutumia udhaifu wa Adam kwa mkewe, akamghiribu ale tunda ambalo Hawa alijua kabisa kwamba wamekatazwa. Delila naye akafuata njia za Hawa kwa Samson, sasa JKN alisema wakati fulani kwamba kiongozi hapaswi kuendeshwa na mkewe, kwamba akilala na kuamka anakuja na jambo jipya hata hamuwezi kutabiri kesho kutatokea nini, alikuwa anasisitiza kufuata sheria za nchi. Angalia viongozi wetu wanawake kwa mfano, wanaotufurusha kila leo katika misemo yao. Kumbuka Waziri na mwenyekiti wa kina mama wa CCM, kumbuka mwenye kigoda mjengoni,n.k. Wanapenda kujitawala huru huria na sasa kwa jina la usawa ati wanapambana na mfumo dume.
Mungu alimgawia kila mmoja roles zake, Adam atakula kwa jasho, Hawa atazaa kwa uchungu na tamaa zake zitakuwa kwa mumewe. Sasa wanawake wanamsahihisha Mungu kwamba wote sawa tu. Kwa kuwa wanaume hawataki kuachilia roles zao kwa wanawake, nao wanawake wamejipenyezea visheria vyao kuwalinda wafanane na wanaume (ingawa wanajua wanajidanganya) hapo ndipo penye utata na chanzo cha mafarakano. Mwanaume kupangiwa zamu ya kupika chakula cha familia sio gender role yake. Lakini kama umemzoeza mkeo kupangiana zamu za kupika halafu baadaye ukageuka na kudai huwezi kufanya kazi za kike, atajua umefunzwa huko nje na mtaanza kugombana.
Mwanamke mwenye busara huijenga nyumba yake, lakini mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe. Wanawake wanaoachika haraka ni wale vichwa maji ambao wanataka daima wawe juu ya wanaume, wao watoe amri tu na wanaume waitikie 'Rebeka mke wangu maulana". Wanawake jeuri utawaona hata katika sauti zao wanapoongea, hawana hofu na wanaume, feminism hamna. Kuna waziri mmoja alikuwa anakaa DSM wakati mumewe anakaa Morogoro, shida ati yuko kazini. Waziri mwingine alikuwa anakaa DSM wakati mumewe anaishi Moshi sti sababu ni kazi. Mawaziri wengine wawili nawajua hawajawahi kuolewa lakini wana watoto kibao kila mtoto na baba yake tofauti, shida ati hawataki kumilikiwa kama bidhaa au asset. Yupo waziri mwingine alikuwa anazunguka tu na kukaa DSM wakati mumewe anaishi Mbeya, shida alikuwa kazini. Sasa viongozi wakuu wa nchi wakizunguka na kina mama hao walikuwa anazunguka pamoja. Kwa nini waume zao wasipate wakati mgumu kujiuliza maswali yasiyo majibu? Wakati mwingine naambiwa mume mmoja alikuwa analalamika kwamba mke wake wakati mwingine anapigiwa simu usiku na wakubwa zake na kujadiliana mambo kibao kwa sauti zenye utii wa hali ya juu na milegezo isiyo kawaida, wakati anapoongea na mumewe huwa na sauti yenye mamlaka na amri daima dumu. Siku zingine mkewe alipelekewa gari usiku wanaondoka ati wanakwenda ofisini na harudi mpaka kesho. Kweli hayo nani atavumilia? Akiulizwa achague kazi au familia wanawake ati kwa ukisasa wanadai "bora kazi" hapo kuachika ni muhali kaka.
Hakuna mume anayeweza kustahimili yote hayo kufanyiwa na mkewe. Hata kama analeta zawadi kila siku. Heshima ni aghali sana. Hebu chukulia mfano wa Bhoke, kama angekuwa na mtu anataka kumuoa, leo hii atakuwa na ujasiri kama wa kwanza kabla hajaenda Sauzi kwa Ernest? Wanaume ni dhaifu nakubali, tena fimbo zao wanazitembeza kila wapatapo nafasi sawa, lakini wanawake wanapotaka kufanana na wanaume, wafanye kama wanaume nani anakomolewa? Anatomically they would suffer more irreversibly, kwani hata madhara ya kujamiiana yanawafika wanawake haraka na vyepesi zaidi kuliko wanaume sababu wao wanapokea na wanaume wanatoa kwao nanihiiino. Tamaa zao lazima wakubali ziwe kwa waume zao. Nakumbuka miaka ya nyuma niliwahi kuishi mikoa ya Kusini wakati Ukimwi haujapata nauli ya kwenda kule, wanawake ndio waliokuwa na jukumu pevu la kutafuta wanaume, kiasi kwamba wanaume wengi hawakuwa wanajua kutongoza, sababu mwanamke atakuwa na tamaa zake focused kwa mwanaume.
Hakuna mwanaume jeuri kwa mwanamke. Kama mwanamke anatumia busara zake za kike na kufuata roles zake sawa sawa kama alivyopewa na Mungu, ataijenga nyumba yake na hawaachiki hao. Mumewe akisema mke anainamisha kichwa chini bila kujibu mapigo. Mumewe akimaliza kuongea, mke anasema samahani mme wangu, nimekosa. Mambo yanaisha. Kama anadhani anaonewa anatafuta muda muafaka ule wa faragha na mumewe, katika mkao wa udhibiti wake anamwambia mumewe kwa upole na ushawishi sana kwamba alisema samahani kwa sababu ya heshima kwa mumewe tu, ila kwa kweli hakufanya alichotuhumiwa. Mumewe ataitikia kila kitu na maisha yanaendelea mbele. Mume anaposema na mkewe anapojibu kila mtu sauti ya juu, ujue ndoa haitadumu kwa amani.
Itoshe kwa leo.