Kwa nini wanawake wanakuwa hivi?

Kakungulume

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2008
Posts
213
Reaction score
54
Naomba msaada wenu wana JF mnisaidie maoni.
Mimi nina GF wangu akikosea usimwambie, ukimwambia umekosea kufanya jambo fulani basi
hapo atatafuta kila njia na namna na wewe uonekane kukosea ili aseme mbona wewe umefanya vile
na vile, hata kukusingizia kosa kwa mfano; nimekuona na msichana mwingine sehemu fulani ili mradi tu
apate kianzio cha kukushutumu....

Hivi hii ni kwa wanawake wote au kwa huyu wangu tu?
 
Hiyo ipo kwa baadhi ya wanawake, sio wote kaka..
 
Wala hatuko hivyo huyo wako ana ka tabia ka ajabu sana ..ila jitahidi ajirekebishe kabla hakajazaa mambo makubwa ..hii mambo ya mbona mbona sio fresh kabisa .
Awe anakubali kosa kama amekosea aombe msamaha na ajirekebishe ,na wewe kama kweli umekosea akwambie na kuwa anasema mbona wewe ulifanya hivi mara vile .
 

sio wote mpendwa ni baadhi tu ya wanawake tena wao hupenda kumpasha mtu ila wao hawapendi kupashwa.
 
Labda hajakomaa kifikra ndio maana hakubali kuambiwa kuwa amekosea mweleweshe pole pole mwisho atakua anakubali unachomweleza na pia atambue kuwa wewe ndio pekee wa kuweza kumwelewesha/kumwelimisha
 
Suala sio kukomaa ila hapo ni kunya anye kuku akinya bata kaharisha
 


FL1...hapo si anataka ku-balance makosa yake kwa kusingizia
 
labda namna unavyomwambia inamfanya awe defensive...jaribu kutumia njia ingine....
 
Hili ni tatizo walilonalo baadhi ya watu (wanaume na wanawake). Jaribu kuongea naye politely labda ataelewa na hatimaye atajirekebisha kama ame-determine kuwa na wewe.

Kwa upande mwingine wewe usiwe chanzo cha upinzani/ukinyume anaofanya kwako. Tengeneza (facilitate) mazingira ya maelewano yenu, kisha naamini mtakwenda muswanu du!
 
Wengine wanakumbushia makosa ambayo yalishasamehewa na kusahaulika kitambo. Utasikia "wewe umesahu ulivyonifanyia wakati ule?" So what, unalipa kisasi?
 
Wengine wanakumbushia makosa ambayo yalishasamehewa na kusahaulika kitambo. Utasikia "wewe umesahu ulivyonifanyia wakati ule?" So what, unalipa kisasi?
anakukumbusha kama hata wewe unakoseaga!!! stop criticizing
 
anakukumbusha kama hata wewe unakoseaga!!! stop criticizing

Ili iweje? kwani past mistakes ziletwe kwenye majadiliano ya leo ;;;yaani wakati mwingine utakuta mtu anakuhesabia all past mistakes ; mie huwa naona hiyo wanaitumia ku justify there present mistakes; na si fair!:A S angry:
 
anakukumbusha kama hata wewe unakoseaga!!! stop criticizing
I am not criticizing, but rather raising a point. Hii inaapply either way. Kama kila jambo likitokea mnakumbushia past mistakes hii ligi haitakuwa na mwisho na wala hamtajenga. Kwa nini ulijimbikizie mzigo wa mambo yaliyoisha moyoni? Unless ulisamehe lakini hukusahau. Kama umekosea omba msamaha, sio kutumia makosa yangu kujustify makosa yako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…