Kwa nini wasafiri wa ndege huwa hawasali kwa pamoja kama wa bus za abiria?

Kwa nini wasafiri wa ndege huwa hawasali kwa pamoja kama wa bus za abiria?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kwa nini wasafiri wa ndege huwa hawasali au kufanya dua/maombi ya kuombea safari kwa pamoja kama wasafiri wa bus za abiria?

Bus zote za abiria ambazo nimesafiri nazo lazima wafanye maombi hata hadi ya dakika 10 kuombea safari, kwenye ndege sijawahi kushuhudia kabisa hili jambo la maombi ya jumla.
 
Labla kwa sababu ndege inapanda juu moja kwa moja karibu na mbinguni maskani kwa Sir God hvy wanawasiliana internal tofauti na huku chini barabarani wanakuwa karibu na maskani ya Bwana Shetani hvy n lazima uumpige mkwara kdg.
 
Kwa nini wasafiri wa ndege huwa hawasali au kufanya dua/maombi ya kuombea safari kwa pamoja kama wasafiri wa bus za abiria?
Kuna ndege nyingi za kwa Bibi kule Shinyanga tunapopanda zile UFOs zetu za duara au mnyama wetu yule pendwa mwenye miguu mirefu ya mbele huwa tunashusha sala nzito kwanza mpaka mbengo zinafengoka
 
1. Tofauti ya Mazoea ya Safari
Watu ni wale wale wa kila siku, wenye tamaduni zile zile, ndege mnakutana watu tofauti tofauti.

2. Usalama
Hizi kimbinyiko ajali popote uharibifu popote, ndege haipo hivo.

3. Mazingira ya Kusali
Mabasi mengi unakuta dereva au konda au urahisi wa kuanzisha sala.
Ndege aisee iko strict timed, ratba yake inafanya hata huyo pilot au hostes ashindwe kuanzisha sala, kwanza haiwezekani.

4. Imani na Desturi
Kuna tofauti ya imani kati ya wapanda ndege na hawa wapanda mabasi.
Huku swala la kawaida sana kusali compared na kule.
 
Kwa nini wasafiri wa ndege huwa hawasali au kufanya dua/maombi ya kuombea safari kwa pamoja kama wasafiri wa bus za abiria?
Kwenye ndege kiyoyozi naagiza ninachotaka naweza kulala kujisomea naweza kutafakari chochote bila bughudha ya aina yoyote..
nikimuita air host atanisikiliza na kutatua shida yangu kwa wakati.... Hata kama kwenye ndege mtu ana ear phone au laptop sauti itakua ya kistaarabu na muda huo uhakika ndege inafanyiwa service kwa muda unaotakiwa na juu ya anga na chini kuwa watu ambao Wana I monitor. Hapo hata sala itakua ya sauti ndogo itakayoweza kupaa kama Moshi wa ubani mpka kwa Mungu baba mwenyezi.

Kwenye bus
Sauti ya tv/radio iko juu hakuna kusikilizana.... Bodi ya gari iko vizuri lakini ukweli wa hiyo gari anaujua dereva, konda na bosi kwa kulitambua hilo dereva na konda wake lazima waite mchungaji uchwala apige kelele akusanye sadaka.

Dereva kapiga mipombe kalala na malaya Yuko kwenye gia na mi hang over kwa Nini abiria tusisali kwa kelele kuu Mungu akatusikia tufike salama????
Gari ikifika sekenke dereva anavua shati huku anahema anaendesha huku anajua ubovu wa gari lake na anajiandaa lolote likitokea awe stand by!!
Dereva akimwambia boss gari bovu liende service jibu lake ni tusi na kumwambia kama kazi imekushinda nipe funguo wengi wanataka hiyo chuma.

Kwenye bus abiria anakomolewa gari stand haisimami inasima kwenye hoteli zao!!!! Kimbembe kinaanzia hapo maji ya elfu moja yanauzwa elfu mbili,, soda take away ya elfu moja inauzwa elfu mbili kwa Nini abiria nisisali gari isimame stand hata dakika tano ninunue vinywaji kwa bei rafiki!!!! Hapo chakula cha kawaida tu portion inauzwa elfu kumi na mbili ambayo hata mtoto wangu wa mwisho hashibi kwa Nini nisisali kwa sauti gari hata itupeleke sehemu itakayoniuzia msosi nikashiba!!!!
Unapewa dakika kumi ukojoe, uninunue chakula!!! Hicho kipengele kama umezaa kama paka kama mie uhudumie watoto wote kwa hizo dakika kumi ni lazima upige yowe la Sala walau usiachwe na bus.
Ndani ya bus ni kelele huku maombi huku amapiano full watoto kulia yaani abiria wengine wameshafakamia mayai, ndizi, energy ni mwendo wa kuachia harufu hewa nzito ukifungua dirisha utaambiwa nasikia baridi mara ooh! Mwanangu anapigwa upepo kifua kitam bana......
Lazima usali dereva akimbize hilo bus muwahi kufika uepukane na hizo kero.
Njia Ina mashimo lami zimeharibika ni mwendo wa kurushwa tu kama magunia na dereva hajali Wala nini ukijitia mdomo utachambwa na dereva na konda wake lazima usali kimya kimya maana Wana midomo michafu.
 
Back
Top Bottom