Kwa nini Watanzania Tunahusudu mambo ya Kenya kuliko nchi nyingine EA

Ni kwakuwa hata upande wa wataalamu wa afya pamoja na vifaa vya afya maranyingi tunategemea kenya.
Utadikia daktari pale Ocean Road anasema " njoo baada ya siku tatu vipimo tunavituma nairobi"
Yan huwa naumia sana, sijui kama na wao huwa wanatuma vipimo bongo kwa ajili ya uchunguzi.
 
Wasema kweli, hasa miaka ya nyuma, ukiwa na mapeni yako, ukiumwa Kenya, kusomesha watoto mpaka chuo Kenya, shopping Kenya, kuajiri wafanyakazi wenye kimombo kizuri Kenya..
Ila kwa sasa sidhani, kidogo tumeshika hatamu.
Ila ni lazima ya Kenya tuyafuatilie, kuanzia ulinzi na usalama mpaka uchumi..NI LAZIMA TUYAFUATILIE KABISA...
 
Mitale wa midimu Iddy Mbarak, nikupongeze kwa kuchangia chochote hapa jukwaani maana hapa ndio kijiwe chetu cha kuondolea uchovu. Mimi napenda maendeleo na kwa nchi za maziwa mkuu SI Unit yangu kiinchi ni Kenya. Huwa kabla ya kutamani Tz iwe kama US au Japan huwa natamani wangalau tuwe kama Kenya.

Kwa muda mrefu nchi hii kumekuwa na kilio cha utendaji wa mifumo. Kwahili la uchaguzi Kenya wamethibitisha pasi na shaka wako vizuri kwenye uwezo wa mfumo. Nasikitika bado nchi yetu inafanya kazi kwa nia njema ya rais, ni aibu kwa hapa tulipofikia kufanya kazi kwa nia njema ya rais. Nawaonea wakenya wivu kwa maendeleo waliyo nayo kuanzia uchumi, kijamii na sasa kidemokrasia. Sitaki kukashifu nchi yangu, lakini kutuweka kwenye mizania na kenya ni aibu.
 
Inaniuma sana lakini ukweli ni kwamba hawa wakenya wametuzidi mkuu, hakuna sababu za kujidanganya na wala kukubali hilo si kukosa uzalendo!

Kwao matokeo ya urais yanahojiwa mahakamani

Kwao separation of power ipo kwa vitendo..

Rais mahakama inaheshimika..

Kwao wanachagua mtu na sio chama.. Tofauti na wale wanaochaga chama hata kikisimamisha asiyefaa!
 
Utaangaliaje ya mbali uache ya karibu? Ujinga wao na uwezo wao sie vinatuhusu kwani wametukaribia kwa upande wa kask mash mwa nchi yetu
 
Kenya ni tofauti sana na nchi nyingine za Afrika mashariki, hakuna mkumbo Kenya ni hoja.Hata wakati wa kampeni Kenya ilikuwa rahisi kujua nani alikuwa madarakani na nani hkuwa madarakani, kwamba aliyekuwa madarakani alikuwa anashawishi kura kwa kuanisha nini amekifanya kwa manufaa ya wakenya katika kipindi kinachoisha na anakusudia kufanya nini akipewa nafasi tena. Wakati aliyekuwa anataka kuingia alikuwa anaeleza aliyekuwepo ofisini alishindwa nini na yeye akipewa nafasi anakwenda kufanya nini. Hapa kwetu huwezi kujua tofauti hiyo kwa kuwa kilammoja utadhani ndio kwanza anawania nafasi.Halafu vyombo vya ulinzi na habari havinaga ubaguzi, Lakini pia unaona kabisa uhuru wa vyombo vyenye mamlaka mbalimbali katika utekelezaji majukumu. Hizi ni baadhi ya sababu za wengi wetu kuipenda Kenya kwa namna wanavyoendesha siasa. ingawa dosari ni pale mtu alipo uawa na kukatwa viganja vya mkono.
 
Umejibu vizuri sana mkuu hili ndo jawabu

blame no body
 
Wewe mleta uzi hivi hujui sababu ya waTZ kufuatilia mambo ya Kenya? Hivi Uganda, Rwanda na Burundi kuna kitu gani cha kujifunza wakati uongozi wao ni wa ubabe tu hauna tofauti na wa mkulu?
 
Mkuu kama wafanyabiashara wa Arusha wanaitegemea kenya asilimia kubwa zaidi wanayo sabaubu kuu za kuzifuatilia siasa za kenya kwa Maana hiyo nchi ndo inafanya wapate ugali wao wa kila sikuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…