Kuna nini cha sisi Watanzania kujifunza kutoka Uganda, Rwanda na Burundi kuliko Kenya?
Demokrasia na siasa nzuri?
Maendeleo na uchumi?
Ujirani na mahusiano mema?
Maingiliano mengine (undugu, kuolena, kutembeleana, kutaniana)?
Uerevu (exposure)?
Hata uugwana na Tanzania una ufanano na Kenya kuliko hizo nchi nyingine. Kenya wametuzidi mno kwenye mambo mengi, mengi mno kiasi kuwa wao kuwa sehemu ya sisi kujifunza ni sawa tu.
Pamoja na matatizo yao ya ukabila, u-much-know, kiburi na majigambo lakini tuna mengi ya kujifunza toka kwao. Kenya tunawazidi katika bongofleva labda na uvivu!!