Kwa nini watu huachana hata wakiwa bado wanapendana?

Kwa nini watu huachana hata wakiwa bado wanapendana?

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Watu wawili wanaweza kupendana kwa dhati, kujali hisia za kila mmoja na kuwa na kumbukumbu nyingi nzuri, lakini bado wakaamua kuachana. Je, ni kweli kwamba upendo pekee hautoshi kuifanya mahusiano yadumu.

Ni nini hasa kinawafanya watu kuachana wakati bado wana hisia kwa wenza wao? Je, ni kukosekana kwa mawasiliano mazuri, kutokuaminiana, usaliti, tofauti za malengo ya maisha, migogoro ya kifamilia au changamoto za kifedha?

Au wakati mwingine mtu anaweza kumpenda mwenzake lakini akagundua kuwa uhusiano huo haumpei tena amani, heshima na usalama wa kihisia anaouhitaji?

Je, unadhani ni bora kubaki kwenye uhusiano kwa sababu bado mnapendana, au kuachana pale ambapo mnaona hamuwezi kujenga maisha yenye amani pamoja?

kuachana.png
 
Kuna vitu vingi sana,
Kuna kitu kinaitwa trauma, mtu unaweza ku penda mtu lakini ukawa huna uwezo wa kuishi nae vyema. Because you need to work on your issues first.

Mahusiano mengi yanashindikana kwa sababu watu hawaja heal old wounds.

So wanajikuta anaproject issues zake kwa mwenzake. So ukimkuta mtu anajijua kabisa anaamua kusave matatizo hayo yote na kuachana na mahusiano kabisa
 
Upendo uliozungumzia ni ule wa hisia, sasa huo pekee hautoshi kuwafanya mbaki pamoja lazima kuwe na subjects zingine zitakazofanya muendelee kuwa pamoja ndani ya hilo pendo, zikikosekana hizo ni vigumu kusurvive kwa sababu mioyo yenu inataka lakini mazingira yenu yanakataa kabisa kusupport hizo hisia zenu
 
Malizia hizo nyingine tujue maana kuna mahali nimewekeza hisia nataka nione kama naweza ongeza juhudi zingine labda tutapanda kiwango.

-Utofauti wa kidini
-Modern trend ya mahusiano ya kibiashara
-Harakati za kila mmoja kutengeneza career yake zinaweza kusababisha mkajikuta mnaishi mikoa au nchi tofauti
-Mahari. Vijana wanaacha ndala baada ya kutajiwa mahari mlima
 
Malizia hizo nyingine tujue maana kuna mahali nimewekeza hisia nataka nione kama naweza ongeza juhudi zingine labda tutapanda kiwango.
Jambo kubwa hapa ni kukinzana kwa mitazamo katika nyanja mbalimbali mfano
1. Imani. Kila mmoja ana imani yake na wote mna ego kwenye hizo imani hamuwezi kwenda pamoja
2. Uchumi, mwingine anaamini mwanaume ndie provider wa kila kitu mwingine anaona mnatakiwa kusaidiana
3. Career fighting. Kila mmoja anataka kujenga career yake hata kama mazingira ya mahusiano yenu yanahitaji mmoja wenu agiveup ili muweze kuendelea
3. Family backgrounds. Hapa kuna ishu za genetics mfano mmoja wenu anatoka katika familia yenye magonjwa ya kurithi kama sikoseli hivyo mwingine anaona hatoweza kuhandle hayo masuala kwenye kizazi chake. na masuala mengine kwenye familia kama vile marufuku ya kuoa au kuolewa na kabila fulani, mila na desturi fulani
 
Sio kweli kwamba wanapendana wote halafu waachane bali mmoja ndo anakuwa bado anampenda mwenzie,ikitokea bado wanapendana wote wanaweza kuhachana kwa muda sababu ya umbali au vizuizi
 
Watu wawili wanaweza kupendana kwa dhati, kujali hisia za kila mmoja na kuwa na kumbukumbu nyingi nzuri, lakini bado wakaamua kuachana. Je, ni kweli kwamba upendo pekee hautoshi kuifanya mahusiano yadumu.

Ni nini hasa kinawafanya watu kuachana wakati bado wana hisia kwa wenza wao? Je, ni kukosekana kwa mawasiliano mazuri, kutokuaminiana, usaliti, tofauti za malengo ya maisha, migogoro ya kifamilia au changamoto za kifedha?

Au wakati mwingine mtu anaweza kumpenda mwenzake lakini akagundua kuwa uhusiano huo haumpei tena amani, heshima na usalama wa kihisia anaouhitaji?

Je, unadhani ni bora kubaki kwenye uhusiano kwa sababu bado mnapendana, au kuachana pale ambapo mnaona hamuwezi kujenga maisha yenye amani pamoja?

View attachment 3653627
Mahusiano mazuri hujengwa kwa busara na maarifa, sio upendo tu. Upendo huisha, hasa ndani ya ndoa. Lazima kuwe na kitu kingine cha kufanya wawili hawa wazidi kudumu. Ni kanuni wala sio hisia. Ni amri, hasa kwa wanandoa.
 
Back
Top Bottom