Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Kuna watu walipendanaKuna tofauti hazitatuliki, dawa ni kuachana hata kama mnapendana.
Tofauti gani hizo mkuu?Kuna tofauti hazitatuliki, dawa ni kuachana hata kama mnapendana.
Upendo uliozungumzia ni ule wa hisia, sasa huo pekee hautoshi kuwafanya mbaki pamoja lazima kuwe na subjects zingine zitakazofanya muendelee kuwa pamoja ndani ya hilo pendo, zikikosekana hizo ni vigumu kusurvive kwa sababu mioyo yenu inataka lakini mazingira yenu yanakataa kabisa kusupport hizo hisia zenu
Jambo kubwa hapa ni kukinzana kwa mitazamo katika nyanja mbalimbali mfanoMalizia hizo nyingine tujue maana kuna mahali nimewekeza hisia nataka nione kama naweza ongeza juhudi zingine labda tutapanda kiwango.
Mahusiano mazuri hujengwa kwa busara na maarifa, sio upendo tu. Upendo huisha, hasa ndani ya ndoa. Lazima kuwe na kitu kingine cha kufanya wawili hawa wazidi kudumu. Ni kanuni wala sio hisia. Ni amri, hasa kwa wanandoa.Watu wawili wanaweza kupendana kwa dhati, kujali hisia za kila mmoja na kuwa na kumbukumbu nyingi nzuri, lakini bado wakaamua kuachana. Je, ni kweli kwamba upendo pekee hautoshi kuifanya mahusiano yadumu.
Ni nini hasa kinawafanya watu kuachana wakati bado wana hisia kwa wenza wao? Je, ni kukosekana kwa mawasiliano mazuri, kutokuaminiana, usaliti, tofauti za malengo ya maisha, migogoro ya kifamilia au changamoto za kifedha?
Au wakati mwingine mtu anaweza kumpenda mwenzake lakini akagundua kuwa uhusiano huo haumpei tena amani, heshima na usalama wa kihisia anaouhitaji?
Je, unadhani ni bora kubaki kwenye uhusiano kwa sababu bado mnapendana, au kuachana pale ambapo mnaona hamuwezi kujenga maisha yenye amani pamoja?
View attachment 3653627