Kwa “nonsense” ya Sukari, Rais Samia anastahili pongezi. Je, tuishie kwenye "nonsense" ya Sukari tu au tuangazie na "nonsense" nyingine zote?

Hiyo Sera ya kulinda viwanda vya ndani,ilitufanya tuvae makaniki ya ajabu ajabu enzi za Nyerere.Soko huria ndiyo jambo lenye nafuu ya maana.Na hii inafanya viwanda vya ndani visibweteke.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Binafsi nimekuelewa..mambo haya ya kijima "kulinda viwanda vya ndani" kayaleta magufuli..
Miongoni mean sababu za kuanguka kwa uchumi wa marekani na ulaya "the great economic depression" ya mwaka 1929 Ni hii ya kulinda soko la ndani..yaani marekani ilianzisha upuuzi Kama huu wa kulinda soko la ndani..yakawakuta makubwa..
Sasa kukataa sukari ya zanzibar sio ujinga Bali Ni upumbavu mkubwa Sana..
 

Mteuen Huyu mtu Jaman kawa Kero!
 
Ninafikiri kutugeuza soko la bidhaa za nje na wakati huohuo tunajinasibu na sera za kustawisha viwanda ndiyo nonsense kamili.
Nani katugeuza soko wakati tuna upungufu mkubwa wa sukari uzaliahaji wa ndani Ni mdogo??
Kwa mfano mafuta ya Kula tunazalisha 40% tu..je tukiagiza kwa wenzetu mafuta ya Kula tumegeuzwa soko..
 
Nani katugeuza soko wakati tuna upungufu mkubwa wa sukari uzaliahaji wa ndani Ni mdogo??
Kwa mfano mafuta ya Kula tunazalisha 40% tu..je tukiagiza kwa wenzetu mafuta ya Kula tumegeuzwa soko..
Wenzako wanazalisha kwa gharama nafuu compared na sisi. Hawawezi ku-compete fairly na wenzetu wenye mitaji mikubwa na wanaowezeshwa na serikali zao.
 
Kongole mkuu Pasco kwa makala iliyo jaa waledi na uchambuzi makini hakika nikwa 'maslahi ya taifa'

Ila tunakuomba ulete uchambuzi wako kuhusu kesi ya Mbowe ukiwa Kama mwandishi na mwanasheria nguli. Asante sana
 
Ukiisoma hii makala hapa unafaidi kuliko ukiisoma kwenye magazeti maana hapa kuna viambatanisho hadi vya video. Nonsense nyingine ni kuzuia vifaranga toka nje kwa ajili ya kulinda viwanda vya ndani wakati viwanda vya ndani havina uwezo wa kukidhi mahitaji. Matokeo bei ya vifaranga imepanda maradufu pia ukishalipa unasubiri hadi miezi mitatu upate hivyo vifaranga
 
Mkuu naona ni bora ungejikita katika kujadili hoja yake iliyo mezani kuliko kumshambulia yeye binafsi ,tujifunze kuheshimu misimamo ya watu hasa pale wanapo chagua upande fulani tofauti na yetu.ila naheshim mawazo yako kama GT mkuu
 
Nimependa uchambuzi wako ila kwa issue ya sukari ya Zanzibar pana shida kidogo kiwanda chao kinazalisha sukari na Zanzibar yenyewe haiinunui yote wanataka kuileta Bara pana ukakasi kidogo. Kwanini wasinunue sukari yao wenyewe wanaagiza kwa njia za panya na sukuri yao inadoda kiwandani hili ndio tatizo. Kuhusu kulinda viwanda vya ndani hapa kuna shida kidogo kwani sukari ya ndani ni gharama kuizalisha kuliko ya nje, unaporuhusu waagize nje hao hao wanye viwanda unategemea nini? Viwanda vitageuka vachuuzi wa sukari na kuacha kuzalisha kwa sababu ya gharama za uzalishaji ni kubwa. Kuvilinda viwanda ni pamoja na kuweka mazingira yanawezesha ushalishaji cempetitive yaani production costs should be low. Angalia bei za umeme, mafuta mazito, vilainishi n.k. Kuvilinda viwanda vya ndani sio kukataa bidhaa za jirani (EAC) or any other country in this World. How could the Country produce goods with competitive price this is more than what we see in the news. The Gov should think more on this tutamezwa na soko la pamoja la EAC. Viwanda vyetu havitauza kitu na definately vitakufa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…