Kwa “nonsense” ya Sukari, Rais Samia anastahili pongezi. Je, tuishie kwenye "nonsense" ya Sukari tu au tuangazie na "nonsense" nyingine zote?

Aliyeandika post hii hajui tofauti ya maneno nonsense, stupid na ignorant; ndio wadakiaji wa maneno hao. Nyerere alikuwa ni intellectual, na alikuwa anajua sana kuchagua maneno yake, hakuwa mropokaji wa kutumia neno nonsense kwa maana ya ignorant; no way!.
 
Kiongozi asiefahamu maana ya integrity ni nonsense mwenyewe, anything within a person's capacity iko na forum sahihi. Matusi ya hadharani hayavumiliki wala kusafishika.
 
Kwa hiyo Paschal unamaanish Bei ya Sukari itashuka bei baada ya kuruhusiwa vibali?
Tutoe muda gani ili tutegemee sukari kushuka?
 
Nani katugeuza soko wakati tuna upungufu mkubwa wa sukari uzaliahaji wa ndani Ni mdogo??
Kwa mfano mafuta ya Kula tunazalisha 40% tu..je tukiagiza kwa wenzetu mafuta ya Kula tumegeuzwa soko..
Sukari imeshuka baada ya nonsense kuondolewa? Au tutarajie itashuka lini??
 
Mkuu ulimsikiliza Waziri au unasikiliza ya upande mmoja na kutoa hitimisho?


Na je tumeruhusu hiyo sukari kutoka nje, je sukari imeshuka bei? Kama bado, tuipe muda gani ishuke?
 
Mkuu ulimsikiliza Waziri au unasikiliza ya upande mmoja na kutoa hitimisho?


Na je tumeruhusu hiyo sukari kutoka nje, je sukari imeshuka bei? Kama bado, tuipe muda gani ishuke?
Sijakuelewa au wewe hujanielewa mimi narespond kwa hola nzuri aliyotoa Mayalla period.
 
Sijakuelewa au wewe hujanielewa mimi narespond kwa hola nzuri aliyotoa Mayalla period.
Hoja aliyotoa Pascal ni kuwa uamuzi wa kuingiza sukari freely ni mzuri

Nikakujibu sio mzuri, sababu waziri alikuwa na hoja nzuri tu, ila pascal hajazigusia
 
Nonsense linategemea nani amelitamka. Mfano unabishana na kichaa akikuambia nonsense ukafadhaika utakuwa kichaa zaidi yake. Hii tabia ya viongozi wakiwa madarakani kujiona wana akili kuliko watu wote inatuumiza sana kwa sababu hatuna utaratibu wa kupima iq na afya ya akili kwa viongozi wetu kwani baadhi kwa matendo na maamuzi yao walitakiwa kuwa Mirembe badala ya ikulu
 
Tangu yakutokee haya ya kuitwa Bungeni,na kuambulia Kura 1,sijui 2 kwenye mchujo, akili yako imevurugika kabisa.
Nimesoma nimekodoa macho nikifuatilia nione ulivyo halalisha kauli ya 'nonsense' ya Hangaya,umepiga piga kiwi tu,umeishia kurukia Mambo mengine.
Nilitegemea Kama mwandishi uliyebobea uje na data ni kiasi gani Cha sukari kinachozalishwa nchini kwa Sasa na je kweli tunahitaji hiyo ya nje?

Umekimbilia kumupongeza Hangaya tu,kwa hiyo waziri mkuu na Mkenda ni wajinga kweli kwenye hili au njaa ya teuzi Kama jina lako lilivyo?
Hiii Baghosha!.
 
Hoja aliyotoa Pascal ni kuwa uamuzi wa kuingiza sukari freely ni mzuri

Nikakujibu sio mzuri, sababu waziri alikuwa na hoja nzuri tu, ila pascal hajazigusia
Nilijaribu kuqualify alichokizungumza na kuongeza kidogo ili kuiboresha na wala sijahitimisha wewe waweza ongeza ili kuboresha au kutoa wazo mbadala.
 
Hata hivyo umeandika nonsense
 
Ulianza vizuri hoja ya sukari ila umeitelekeza njiani ukahamia bidhaa zingine. Tafadhali hitimisha walau kwa kueleza nini kifanyike ili kuondoa nonsense kwenye sintofahamu ya sukari.
 
''Yaani Tanzania bara inakabiliwa na uhababa wa sukari, Zanzibar inayo sukari ya ziada bwelele, Zanzibar inakataliwa kuingiza sukari yake bara, na badala yake, wenye viwanda ndio wanaoruhusiwa kuagiza sukari ya bei chee kutoka ng’ambo, kufidia huo upungufu!, kwa uamuzi kama huu, ni neno gani zuri zaidi ya kulitumia zaidi ya neno “nonsense?”.

Mkuu Paskal you nailed it.
Lakini natamani tuangalie angle nyingine kwa nini tuna ''nonsense'' nyingi kiasi hiki:-

Je,kwamba viongozi wa kisiasa (watembelea maviieitee) hawafahamu hali halisi ya capacity ya viwanda vyetu? Au na wao ni miongoni mwa shareholders kwa maana ''they make scarcity'' ili demand na supply ifanye kazi? Na kama ni hivyo basi hawana uhalali wa kuwa viongozi wetu maana wana sifa ya unyonyaji.

Je,kwamba tuna mpango mkakati wa kukuza viwanda vyetu vya ndani bila kuzingatia namna bora ya kuimarisha ushindani na bidhaa kutoka nje ili kuhakikisha viwanda vinazalisha bidhaa bora na zenye affordable price?

Je,viongozi wetu hawaguswi na upandaji wa bei za bidhaa kwa kuwa kuna immaterial effect kwao? Kwa kipato chao hawawezi kuathirika na sukari ya kilo moja Tsh.2500/=,Petrol Lita mojaTsh.2500/=,Mfuko mmoja wa saruji Tsh.24,000/= Kwa hiyo tuseme they don care!!! Kama jibu ni hili basi hawatufai kwa sababu ni wachoyo na wabinafsi (wapo siyo kwa ajili yetu ila kwa ajili ya matumbo yao na familia zao)

Je,hatuna malighafi za kutosha kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zenye upungufu nchini mwetu? Tukumbuke mfano, sukari ilianza kupaa bei tangu 2016 kama sikosei.Kama tatizo lilikuwa ni malighafi je,hatuna ardhi ya kilimo cha miwa kwa ajili ya kupata malighafi za viwanda vya sukari kisha tupate sukari ya kutosha. Kwa nini nchi ndogo (ukilinganisha na Tanzania) kama Uganda wana uwezo wa kuwa na surplus ya kuweza kuuza nje sisi tunakwama wapi?

Mwisho (japo kuna mengi) viongozi wetu muwe wazalendo hebu muipende nchi yenu tambueni mnatupa mzigo mkubwa sana kuyamudu maisha yetu ya kila siku.Hivi mnafahamu kuna watanzania ambao hawana uwezo wa kupata milo 2 kwa siku? Na vipi bei za bidhaa zinapopanda kiholela wataenda chooni hawa,watakuwa salama kimwili na kiakili? Hamtatuua kwa njaa?

Punguzeni tozo kwenye mafuta ili vyuma vilegee#
 
Wanaokugeuza soko sasa hivi waliumia zamani ili kustawisha viwanda vyao. Umia kwa ajili ya vizazi vijavyo, boya wewe.
Ni sawa waliumia,
lakini waliumia kwa namna nyingine, factor kubwa inayosababisha ongezeko la bei ni bei ya umeme kwa unit.
Tanzania tungeweza kufua umeme kwa wingi na kuuza kwa bei ya chini ingesaidia sana kupunguza mfumuko wa bei na kuhamasisha ongezeko la viwanda kwa wingi sana.
 
Ulianza vizuri hoja ya sukari ila umeitelekeza njiani ukahamia bidhaa zingine. Tafadhali hitimisha walau kwa kueleza nini kifanyike ili kuondoa nonsense kwenye sintofahamu ya sukari.
Nafikiri ukiendelea kusoma utaona sijatoka kwenye sukari, ila niliongelea nini cha kufanya, kwa serikali kuangalia viwanda vyetu viweze kuzalisha sukari kwa bei nafuu.
 
Kwa taarifa zilizopo, inasemekana kuwa kampuni zote za kikandarasi iwe ujenzi, umeme, nakadhalika zilizosajiliwa Tanzania bara zimeondolewa haki ya kuomba kazi Zanzibar kama kampuni zilizosajiliwa katika Jamhuri ya Muungano Tanzania. Kwa sasa kampuni hizi za kandarasi zinawekwa sawa kama kampuni zinazotoka nje ya Jamhuri ya Muungano Tanzania. Yaani kampuni hizi za Tanzania bara zinatozwa kodi sawa na kampuni za kifaransa, kichina, kituruki, kimisri nakadhalika!!! (Kama taarifa hizi siyo sahihi nitaomba nipewe taarifa sahihi)

Nadhani mambo kama haya ndiyo yanazidisha "nonsense"!
 
Nafikiri ukiendelea kusoma utaona sijatoka kwenye sukari, ila niliongelea nini cha kufanya, kwa serikali kuangalia viwanda vyetu viweze kuzalisha sukari kwa bei nafuu.
Okay nilizungumzia vitu kama umeme, mafuta, vilainishi nk (Production costs). vikiwa ni vitu ambavyo viwanda vya sukari hutumia kuzalisha sukari, kama serikali ikiangalia vyote hivi vinaweza kupunguza bei ya sukari yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…