Zamiluni Zamiluni
JF-Expert Member
- Feb 11, 2014
- 13,997
- 15,112
Mwanzo » Habari
[h=2]Madawa ya kulevya yazidi kuwaharibu wanafunzi Dar[/h]
Na Moshi Lusonzo
14th February 2015
B-pepe
Wengi wamegeuka ni 'mateja', Wanashiriki kucheza kamari , Wanao mtandao kukwepa polisi
Waziri wa Elimu na Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
Wanafunzi wa shule za sekondari jijini Dar es Salaam, wamejiingiza katika wimbi la utumiaji wa dawa za kulevya na uchezaji kamari, hali inayoodhofisha elimu nchini.
Uchunguzi uliofanywa na NIPASHE katika shule mbalimbali jijini Dar es Salaam, umebaini kuwa baadhi ya wanafunzi wameathirika na dawa hizo na kuwa mateja.
Madawa yanayoongoza kuuzwa ni bangi, heroin na cocaine.
Wanafunzi wanaojihusisha na utumiaji wa madawa hayo ni wa shule za serikali za kata, binafsi na taasisi za kidini.
Wanafunzi hao kwa sasa wameunda mtandao maalum wa kuwakutanisha na wafanyabiashara wa madawa hayo ili kuepuka kukamatwa na polisi.
Moja ya eneo lililoshamiri kwa matukio hayo ni Toangoma jirani na shule mbili za sekondari ya Malela na Toangoma, ambapo katika tukio la hivi karibuni wanafunzi sita walikamatwa wakiwa na kete 116 ya bangi na misokoto sita.
Wakizungunza na NIPASHE, baadhi ya wananchi walisema eneo hilo huwakutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali kwa ajili ya utumiaji wa madawa hayo.
Hamisi Zuberi ambaye aliongoza zoezi la kupambana na mtandao huo, alisema wanafunzi hao sita ni miongoni mwa wengine zaidi ya 100 waliokutwa wakinunua na kutumia.
Kwenye kamata kamata hiyo, mfanyabiashara mmoja aliyetajwa kwa jina la Bashir Hemed (22), mkazi wa Mbagala alitiwa mbaroni akituhumiwa kumiliki shehena hiyo ya bangi.
Zuberi alisema eneo hilo walikuta paketi mbili za vifungashio aina ya lizra na kiberiti kimoja.
Ni tukio baya hasa kutokea kwa idadi kubwa ya wanafunzi wakivuta bangi nje ya shule, ni mtandao mkubwa unaowahusisha wafanyabiashara na wanafunzi, alisema Zuberi.
Baadhi ya wanafunzi waliohojiwa na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina yao, walisema wafanyabiashara wanauza dawa hizo kati ya Sh. 200 na 300 kulingana na aina na ujazo wake.
Wanaokuja kuuza majani (bangi) mbona wapo wengi tu, tunaomba serikali iongeze kasi ya kuwakamata ili tuweze kusoma vizuri kwani mara nyingi wanapotoka kuvuta wanatusumbua darasani, alisema mwanafunzi mmoja
Makamu wa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Toangoma, Florian Kilindo, alikiri kuzidiwa na mtandao huo na kuitaka serikali kuingilia kati.
Alisema pamoja na walimu kuchukua jitihada binafsi kuzuia, lakini wamerudi nyuma kutokana na kutishiwa usalama wao na wanafunzi hao.
Imefika wakati sisi kama walimu tumeona hatuwezi tena kuwadhibiti, kila mara tumeomba msaada wa polisi kuja kuwakamata lakini bado mtandao unazidi kukua na kuhatarisha usalama wetu na wanafunzi wengine darasani, alisema.
WAZAZI LAWAMANI
Mwalimu Kilindo, aliwalaumu wazazi kukwepa majukumu ya kuwafuatilia watoto wao, badala yake wanaona kazi hiyo inafanywa na walimu pekee.
Alisema, watoto wanaojihusisha na vitendo hivyo hawaingii madarasani na kusababisha kupata matokeo mabaya katika mitihani mbalimbali wanayoifanya.
Licha ya mtoto kuwa na matokeo mabaya au kutopata kabisa kutokana na kutofanya mitihani, hakuna mzazi anayekuja kuuliza, jambo hili linawafanya watoto kuwa na uhuru wa kuendelea na vitendo vyao, alisema.
WANAFUNZI WASIMAMISHWA
Katika hatua nyingine, uongozi wa shule hiyo imewasimimasha masomo wanafunzi wanaohusishwa na utumiaji wa dawa hizo hadi hapo Bodi ya shule hiyo itakapokaa na kuwajadili.
Polisi wametuambia wamewaachia huru kwa sababu hawana sheria ya kuwashikilia wanafunzi kwa muda mrefu, hapa tunavyoongea wameachilia lakini sisi tumewasimamisha masomo, alisema Kilindo.
Hata hivyo hakueleza lini bodi hiyo itakaa kwa ajili ya kujadili suala hilo.
DIWANI: INASIKITISHA
Diwani wa Kata ya Toangoma, Rashid Mikuki, amesema amesikitishwa kuona wanafunzi wanaacha shule na badala yake wanaishia porini kuvuta bangi.
Alisema mtandao huo upo kwa miaka mingi, lakini huko nyuma walijaribu kuudhibiti kwa kufanya zoezi la ukamataji kila mara.
Hata hivyo kwa tukio hili nimesikitika kuona watoto wetu ambao tunajitahidi kuwaboreshea mazingira ya kujisomea wanajiingiza kwenye vitendo vya kipuuzi, alisema.
Katika kuhakikisha wanafunzi wa shule za sekondari Manispaa ya Temeke, jumla ya maabara 80 zimejengwa sawa na maabara mbili kwa kila shule kwa ajili ya masomo ya sayansi.
WAZIRI: NIMESHTUKA
Waziri wa Elimu na Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alionyesha kushtuka na kusema kwamba hakutarajia kulisikia na aliahidi kulifanyia kazi.
Nashukuru kwa swali lako ndugu mwandishi, kwa kweli nimeshtuka sana lakini kutokana na sehemu nilipo siwezi kulizungumzia, niache nilifanyie kazi halafu nitalisemea, alisema Dk. Kawambwa.
CHANZO: NIPASHE