Kwa poor performance aliyonayo kipa Emmanuel Msejja kwa nini hakutemwa dirisha dogo? nani anambeba?

Bado kipa ni dhaifu sana, magoli yote aliyofungwa kwenye kombe la Mapinduzi alikuwa analengwa yanampita mkononi
 
Bado kipa ni dhaifu sana, magoli yote aliyofungwa kwenye kombe la Mapinduzi alikuwa analengwa yanampita mkononi
Basi tufanye hivi
Mechi ya kwanza simba ilitoka na matokeo ya 1-1 point 1
Mechi ya pili 3-1 point 3
Ya tatu tufanye 0-0 point 1
Ya nne 0-0 point 1
Jumla point 6
Bado timu ya Simba ingetolewa tu Azamu na URA wangepita vile vile walishashinda mechi tatu.

Je hapo tatizo ni la golikipa ?
 
No sina maana hiyo, nakubaliana na wengi kuwa ushambuliaji sio mzuri Simba ila pia kipa ameonesha performance ya chini sana.
However, kipa mzuri anaweza kuboost morale ya wachezaji na mbovu anaweza kushusha morale ya wachezaji
 
Ngoja tufanye mpango wa kumrudisha yule Elias Maguli
 
Mkuu jitahada zifanyike tumchukue yule Elias Maguli
 
Mkuu jitahada zifanyike tumchukue yule Elias Maguli
Jitihada zilifanyika mkamchukua Manula
Jitihada zilifanyika mkamchukua Nyoni
Jitihada zilifanyika mkamchukua Kapombe
Jitihada zilifanyika mkamchukua Boko
Jitihada zilifanyika mkamrudisha Okwi lakini bado NDOO itaelekea ilikozoea kupiga kambi....Jangwaniiiiiiii!
 
nimecheka sana ulivyo malizia et Asante kwasi, kuna jamaa yangu hataki sikia hili jina
 
nimecheka sana ulivyo malizia et Asante kwasi, kuna jamaa yangu hataki sikia hili jina
Ha..ha..ha...hizi timu zitatutoa Roho siku moja.
Watu wanazipenda sana hadi unashindwa kuwadhibiti.

Eti mtu anakata Roho kisa timu imefungwa, wengine timu ikifunga Wanakata Roho pia.
Hakuna jema hapo, timu ikifungwa au kufungwa mtu anakufa.
Haya ni mapenzi mabaya sana, penda kidogo ili uumie kidogo kwenye matokeo.

Kila kitu kiwe kwa kiasi
Wandugu.
 
hayo yanaitwa mahaba mkuu, mzee wangu ni msimbazi damu wakati mwingine huwa naiombea ishinde ili awe na furaha maana wakipigwa huwa ni utata.

atakumbushia makosa ya zamani, atafoka hapo ila ikishinda kreti la soda na vinono vingi anakwambia 'njoo ule matunda ya simba, taifa kubwa"
 
Simba, Simba, toto football kwa saaana, magoli hakuna. Hata haieleweki shida nini.
Striker hawalioni goli au…………!!! mtamlaumu Mseja tu.

Nadhani makocha kuna haja ya kubadilisha mfumo, shoo game ioneshwe baada ya kuzifumania nyavu.
Ushindi ndio muhimu.
 
Ni kweli mkuu,
Timu zote zinazocheza na Simbs huwa zinautafuta mpirq kwa tochi.
Angalia timu ya Azamu inavyokimbiza na ina vijana wadogo kabisa na inazidiwa umuliki wa mpira kwa asilimia 61 kwa 39.
Huwezi amini lakini ndio ukweli.
Simba inacheza mpira mkubwa sana uwanjani inashindwa kumalizia tu golini pa adui na mwisho wake wanaishia kufungwa.
Ni kama timu ya Uholanzi wakati ule. Kuna siku ktk kombe la dunia Uholanzi ilimiliki mpira kwa 70 dhidi ya 30 za Italia na ikaishia kufungwa goli moja bila.

Simba inabidi ibadilike, ianze kutia nia katika kulifikia lango la adui na sio kupiga pasi nyingi uwanjani zisizo na tija kwa timu.
Simba inahitaji kusajiri washambuliaji vijana wenye kasi kama anayoionesha Emanuel Gyan.
Au kocha amjaribu Gyan namba tisa au kumi anaonekana kuwa na kasi nguvu na uchu wa goli.

Naipenda Simba Daima.
 
Poleni sana mashabiki wa simba kwa timu hii pendwa kuingiliwa na wachezaji wasaka tonge bila kujitoa kwa faida ya timu
Njooni tuujenge mpira singida united.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…