Kwa sababu za kiafya, maombi ya dhamana ya Dr. Slaa yasajilliwa kwa hati ya dharura Mahakama ya Rufani

Je, ni Sheria ipi ilimruhusu slaa kuandika uongo juu Rais na mbowe?

Ukiua kwa upanga unauawa kwa upanga.
Si ndio maana kapelekwa Mahakamani na uzuri TUHUMA/KOSA lake lina dhamana..kwa hali ya sasa ni kama anahukumiwa kabla Mahakama haijamtia hatiani..tuheshimu Katiba na sheria za nchi
 
Hakuna aliyemnyima dhamana, dhamana yake ipo wazi.
Mashauri ya kisheria ya kesi yake yakiisha atapata dhamana.

Halafu, mbona alipowekwa jela yule mmiliki wa mabibo bia and wine na yule mwenzake hamkupiga kelele? Hawakuwa wazee? Hawakuwa wagonjwa?
Au nyie ni waumini wa haki za upendeleo? "Huyu mupe huyu muruke"
 
Kuna maelfu ya watu kama shaibu Slaa wako mahabusu hawasemewi.
 
Si ndio maana kapelekwa Mahakamani na uzuri TUHUMA/KOSA lake lina dhamana..kwa hali ya sasa ni kama anahukumiwa kabla Mahakama haijamtia hatiani..tuheshimu Katiba na sheria za nchi
Kazoea kusingizia idara

Acha aitumikie sasa
 
Hakuna aliyemnyima dhamana, dhamana yake ipo wazi.
Mashauri ya kisheria ya kesi yake yakiisha atapata dhamana.

Halafu, mbona alipowekwa jela yule mmiliki wa mabibo bia and wine na yule mwenzake hamkupiga kelele? Hawakuwa wazee? Hawakuwa wagonjwa?
Au nyie ni waumini wa haki za upendeleo? "Huyu mupe huyu muruke"
Sababu alizozitoa huyo Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umezielewa kweli?..kukata rufaa kwa Serikali kwenye ngazi nyingine kuna mzuia vipi Hakimu kutoa dhamana..nadhani kuna nia OVU

Pia mimi simtetei Slaa kupata Dhamana ati kwa kuwa ni Mzee ..laa hasha..mimi naamini mtu yeyote ana haki ya kupata dhamana ( kwa makosa yote yenye dhamana kwa mujibu wa Katiba) bila kujali jinsi,umri, kabila wala rangi
 
CCM hebu acheni kuzichezea namna hii hizi mahakama, mnautia aibu huu muhimili muhimu sana wa HAKI katika taifa letu.
 
Sababu alizozitoa huyo Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umezielewa kweli?..kukata rufaa kwa Serikali kwenye ngazi nyingine kuna mzuia vipi Hakimu kutoa dhamana..nadhani kuna nia OVU

Pia mimi simtetei Slaa kupata Dhamana ati kwa kuwa ni Mzee ..laa hasha..mimi naamini mtu yeyote ana haki ya kupata dhamana ( kwa makosa yote yenye dhamana kwa mujibu wa Katiba) bila kujali jinsi,umri, kabila wala rangi
Hiyo rufaa ikikubaliwa na hiyo mahakama ya juu wakati hakimu wa mahakama ya chini keshampa dhamana utafikiri nini kitatokea?
 
EAC viongozi wote wajinga, Mseven ana hangaika na Besigye kesi ya kutunga ambayo haina maana, Samia yale yale ana hangaika na Slaa kesi ambazo haieleweki, Ruto maandamano na utekaki vimeshamiri, Kagame vile vile kuua wapinzani, Congo M23 wameshika kasi, haya yote ni tamaa za uongozi na mifumo mibovu za elimu ambazo zina zalisha viongozi dhaifu ambao muda wote wana hofu, lakini una jiuliza hofu ya nini ilihali Polisi ni wako, jeshi ni lako, Tume ya uchaguzi ni yako, kila kitu ni chako , sasa incompetence ni ya nini?
 
Mahakama bado haijamtia HATIANI lakini..ni kama anahukumiwa kabla ya Mahakama..sio sawa
24/7 mnahukumu humu jamvini kabla ya mahakama…

And you don’t even trust mahakama kabisa but you want kwenye hili mahakama ndio itoe haki

Mbona unajichanganya sana?
 
Wakuu,

Mwanasiasa na mwanaharakati mashuhuri, Dkt. Wilbrod Peter Slaa, ameomba Mahakama ya Rufaa ya Tanzania impatie dhamana akisubiri rufaa yake ya jinai kusikilizwa.

Ombi hili limewasilishwa chini ya hati ya dharura kubwa na wakili wake, Hekima Mwasipu, likieleza kuwa Dkt. Slaa amewekwa rumande kinyume cha sheria na kwamba afya yake inaendelea kuzorota akiwa gerezani.

Kwa mujibu wa Mwasipu, Dkt. Slaa anashikiliwa katika Gereza la Keko bila msingi wowote wa kisheria, licha ya kuwa kosa linalomkabili linastahili dhamana.

"Mteja wangu amenyimwa haki yake ya msingi kwa kuwekwa mahabusu bila sababu za kisheria kwa kosa ambalo kimsingi ni la kudhaminika," amesema Mwasipu katika maombi rasmi kwa Mahakama ya Rufaa.

Wakili huyo ameeleza zaidi kuwa afya ya Dkt. Slaa ni mbaya na kwamba kuendelea kwake kubaki gerezani kunahatarisha maisha yake.

"Mgonjwa anapaswa kupata matibabu sahihi, na kuzuiliwa kwake gerezani bila uhalali wowote wa kisheria ni sawa na kuhatarisha maisha yake bila sababu," ameandika katika ombi hilo.

Katika maombi yake, Mwasipu amesisitiza kuwa Mahakama ya Rufaa inapaswa kushughulikia suala hili kwa haraka kutokana na athari zisizoweza kurekebishwa endapo mteja wake ataendelea kuzuiliwa.

"Kufungwa kwa Dkt. Slaa katika Gereza la Keko ni kitendo kinachosababisha madhara yasiyorekebishika. Kwa misingi hiyo, tunaiomba Mahakama itoe uamuzi wa haraka juu ya maombi haya ya dhamana," amehitimisha.

Mdomo huu ni hatari!
 
Mwacheni asote kwanza hadi pale atakapotambua kwamba Urais hauchezewi
Huyo muNGU wenu naye atapita tu kama moshi .Atanyauka kama maua. Ubaya wake hautakumbukwa milele .

Tunajua wanamuogopa Dr. Slaa maana wale wazee wa CCM hawana uwezo wa kupingana kwa hoja na Dr.Slaa.

Huyo muNGU wenu ndiye aliyekua analichukia jeshi la polisi kwa kuonea watu mpaka akaunda haki jinai lakini leo kwa sababu linamsaidia kubaki madarakani na kulinda ufisadi na mafisadi na magaidi halisi yaliyojificha kwa kujifanya machawa basi mnaona ni sawa
 
Wakuu,

Mwanasiasa na mwanaharakati mashuhuri, Dkt. Wilbrod Peter Slaa, ameomba Mahakama ya Rufaa ya Tanzania impatie dhamana akisubiri rufaa yake ya jinai kusikilizwa.

Ombi hili limewasilishwa chini ya hati ya dharura kubwa na wakili wake, Hekima Mwasipu, likieleza kuwa Dkt. Slaa amewekwa rumande kinyume cha sheria na kwamba afya yake inaendelea kuzorota akiwa gerezani.

Kwa mujibu wa Mwasipu, Dkt. Slaa anashikiliwa katika Gereza la Keko bila msingi wowote wa kisheria, licha ya kuwa kosa linalomkabili linastahili dhamana.

"Mteja wangu amenyimwa haki yake ya msingi kwa kuwekwa mahabusu bila sababu za kisheria kwa kosa ambalo kimsingi ni la kudhaminika," amesema Mwasipu katika maombi rasmi kwa Mahakama ya Rufaa.

Wakili huyo ameeleza zaidi kuwa afya ya Dkt. Slaa ni mbaya na kwamba kuendelea kwake kubaki gerezani kunahatarisha maisha yake.

"Mgonjwa anapaswa kupata matibabu sahihi, na kuzuiliwa kwake gerezani bila uhalali wowote wa kisheria ni sawa na kuhatarisha maisha yake bila sababu," ameandika katika ombi hilo.

Katika maombi yake, Mwasipu amesisitiza kuwa Mahakama ya Rufaa inapaswa kushughulikia suala hili kwa haraka kutokana na athari zisizoweza kurekebishwa endapo mteja wake ataendelea kuzuiliwa.

"Kufungwa kwa Dkt. Slaa katika Gereza la Keko ni kitendo kinachosababisha madhara yasiyorekebishika. Kwa misingi hiyo, tunaiomba Mahakama itoe uamuzi wa haraka juu ya maombi haya ya dhamana," amehitimisha.

ni vizuri huyo mzee akatibiwa akiwa huko huko korokoroni tu :pulpTRAVOLTA:
 
Back
Top Bottom