Kwa sababu zilezile za Ndolanga: Sioni uwezekano wa Ally Mayai kuchaguliwa:

Truth Matters

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2013
Posts
2,302
Reaction score
4,603
Wote mnakumbuka miaka ile ya 90 jinsi komandoo Muhidini Ndolanga alivyokuwa anashinda chaguzi za FAT against all odds!
Licha ya nchi nzima kumpinga pamoja na Serikali Chini ya waziri Juma Kapuya, kumpinga lakini baada ya kila uchaguzi Ndolanga alikuwa akiibuka Kidedea!
Wengi hawakuelewa siri ilikuwa nini, wengine wakadiriki kudhani ni uchawi!
Siri ni kuwa idadi ya wapiga kura ni wachache wanajulikani well in advance na mgombea ana muda wa miaka minne kumshawishi mjumbe !
Na hili Malinzi kalifanya kwa umahiri mkubwa! wale wajumbe walikuwa na roster ya kuja Dar kula bata kwa gharama za Malinzi!
Sioni namna Ally Mayai ataepuka kikombe hiki!
 
Yupo na wanamikakati wa kutosha ushindi ni saa 4 asubhi
 
clouds hawajawahi kushindwa jambo wakiamua Labda kwa hili itakuwa Mara ya kwanza na sidhani, Mayai Analijua soka LA bongo na figisu figisu zake najua hajakurupuka Hata kama ni pingamizi najua atashinda hata Malinzi mwenyewe alikuwa Ameshakatwa Kipindi kile Lakini HAWA clouds walikuwa upande wake nadhani unajua kipi kilitokea Huu ni muda wa mabadiliko makubwa na ya kustua yuko wapi nguli Blattar?? Yuko wapi Issah Ayattoh? Muda wa mabadiliko umefika Malinzi arudi kwenye ndondi ndo fan yake siyo football
 
Clouds usiwape utukufu kiivyo sasa mbona dauda hua anakosa hata huo ujumbe kama kweli hawashindwi?
 
Mkuu naomba kufahamu Clouds wapo upande upi kati ya Mayai & Malinzi?
Wanashugulikaje pia kutoa support na kumpromote huyo walie upande wake?
Ahsante.
 
Uchaguzi wa TFF upo kwa namna ya kipekee sana.
Jamal Malinzi ameshaandaa wapiga kura wake ambao ni Wenyeviti wa vyama vya soka vya mikoa. Huku yeye mwenyewe akiwa Ni mwenyekiti mkoa wa Kagera.
Wenyeviti hawa walikuwa wanapangwa kutokana na matakwa ya Rais Jamal Malinzi kama ulifuatilia Uchaguzi kwa mikoa ya mbeya, Iringa na Katavi.
Mastermind wa haya yote alikuwa Wambura ambaye ameamua kujisogeza kugombea umakamu wa Rais ili watengeneze safu ya Uongozi pamoja na Malinzi.
Ni wazi kuwa kupiga kura ni formality tu na hakuna namna unaweza kumshinda Malinzi kwa aina hiyo ya wapiga kura.
 
Mm nawashangaa wanaompa ushindi Mayay, hawezi kushinda labda Malinzi hajitoe. Hata Malinzi asingeshinda km Tenga angegombea.
 
mbona wagombea wako kibao tu kwann mnamjadili mayai peke yake?
Chaguo lao. Watu wa malinzi wametulia tuliii.
Hawapo kujibu hoja JF. Wana mikakati yao.Kama Michael Richard Wambura yupo mlengo mmoja na Malinzi, ushindi ni asubuhi.
Simba Ukawa.
 
Kwani kipindi kile wale wagombea wa mikoa si ndio walikua wanamuunga mkono nyamlani lakini alifikia wapi
 
Mayai ana nini cha ziada kwenye uongozi?
Huyo malinzi si aliharibu ndondi huyo halafu tena ni power monger Mara ndondi ,Mara basket Mara mpira haeleweki


Mpeni then utaona ..hao wenye uzoefu kwenye uongozi wameifanyia nini Tff tokea kwenye Fat
 
Uchaguzi pia unachagizwa na uwezo wa kifedha wa mgombea! Je Ally anafedha za kuhonga wajumbe? Ingawa natamani Ally aongoze TFF lakini naliona Li Marinzi likishinda tena!
 
Huyo malinzi, alimradi ameshaingia hapo tff,hakuna Wa kumtoa, ni king'ang'anizi hatari, anavinasaba vya ndolanga...Mlibabaika kipindi kile alivyokuwa anatiatia huruma mkambebea bango la kumpigania ashinde, sasa mtaisoma namba..

Hawa watu ni Wa kuwaogopa kama ukoma, Jamal malinzi, Ismail Aden rage,muhidin ndolanga, Michael wambula...
 
DAWA YA MALINZI AIWEZI WACHA MAYAII..MAEMBE ..MADEGA SALAMA HATA KIDOGOO.UULIZE NYAMLANI.. ALIEMTUMA MAYAI KUMWAIBISHA TFF .MUNGU ANAMWONA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…