Kwa sasa Geita inachangia pakubwa kwenye pato la Taifa, “inastahili" kama Kilimanjaro enzi za kahawa!

Kwa sasa Geita inachangia pakubwa kwenye pato la Taifa, “inastahili" kama Kilimanjaro enzi za kahawa!

Hakuna wilaya inayoitwa Geita vijijini, bali wilaya ya Geita.

Sema hivi, kuanzia mwaka 2015, Jimbo la uchaguzi lililokuwa likiitwa Geita liligawanywa na kuwa Jimbo la Geita mjini na Geita vijijini

Pia, baada ya mji wa Geita kupewa hadhi ya mji, kukawa na halmashauri mbili ndani ya wilaya moja ambazo Ni
1. Halmashauri ya wilaya ya Geita ambayo ndani yake Kuna majimbo ya uchaguzi ya Geita vijijini(kwa Msukuma) na Jimbo la Busanda.
2. Halmashauri ya mji wa Geita yenye Jimbo la uchaguzi la Geita mjini.

Hivyo, wilaya ya Geita Ina halmashauri mbili na majimbo matatu.
This is very confusing! Wamefanya makusudi ili kuwa confuse watu?!
 
Nakubaliana nawe kwa asilimia kubwa, lakini kujenga uwanja wa ndege wa international- mmmm sijui kama utawasaidia wana Geita.

Ningependa hata bandari kuu Tanzania ijengwe CHATO - lakini!!!!!!!!!! Tunaweza kuorodhesha vingi tu vya ufahari vinavyoweza jengwa huko lakini swali hivyo vitu vitamsaidiaje mwana- Geita na mtanzania kwa jumla.
Hapo ni sawa na kuwajengea vitu wasivyovihataji kwa sasa
 
Hahahaaaa......hahahaaaa...... Nasikia Lema kaomba kazi UN Habitat!
Sijui Kama kweli Unapajua Geita au CHATO?
Zaidi ya juona kwenye vyombo vya Habari

Hata tumor miaka 50 ,sijui haliwezi kuizidi kichwa.
 
Ajabu ni kuwa maeneo yenye migodi yamesahaulika kabisa na maendeleo yanaelekezwa kijijini Chato ambapo tunasikia mpango ni liwe jiji kubwa kama Wuhan China!
Huu ni umobutu seseko,kwanini tusiyashuhudie haya kwenye kijiji kingine nchini badala yake ni Chato tu?
Bado li uwanja la kimataifa la mchezo wa mpira wa miguu,kwamba mechi za Taifa Stars tutakuwa tunaenda kuangalizia Chato!
 
This is very confusing! Wamefanya makusudi ili kuwa confuse watu?!
Sidhani. Na ujue si Geita pekee kwenye namna Kama hiyo.

Mfano, Kuna wilaya inaitwa Kilombero. Ndani ya wilaya hiyo ya Kilombero nako Kuna halmashauri mbili.
1. Halmashauri ya mji wa Ifakara.
2. Halmashauri ya wilaya ya Kilombero. Mpaka mwaka 2019 unaisha, halmashauri zote mbili zilikuwa na makao yake mjini Ifakara.

Mfano pia, wilaya ya Sengerema, Ina halmashauri mbili.
1. Halmashauri ya Buchosa
2. Halmashauri ya Sengerema.

Nadhani huwa Kuna vigezo wanavyovizingatia katika kuleta uwiano huo.
 
Wataanza kubeba mawe na madongo na kuyajaza wajenge Mlima mrefu kuliko Kilimanjaro
 
Geita haijaumbwa ili iwe mashimo baada ya kuchimba madini bali inastahili maendeleo kama mikoa mingine.

Nimeona niseme hili maana ujenzi wa kimaendeleo wa uwanja wa ndege na hospitali ya Rufaa unawanyima usingizi Chadema ambao wamewahi kuwa na wabunge makini kutoka kanda ya ziwa.

Geita na mikoa mingine iliyosahaulika ni lazima ikumbukwe sasa kama kahawa ilivyoinufaisha Kilimanjaro.

Kupanga ni kuchagua.

Maendeleo hayana vyama!

Mkuu, kitu ambacho hukijui ni kwamba zao la Kahawa lilikuwa linanufahisha Taifa kwa jumla - kahawa inauzwa Ulaya na fedha kwenda hazina - wakulima wa kahawa kupitia vyama vyao vya ushirika ndio walikubaliana kwamba wanapo uza kahawa kwenye vyama vya ushirika wanakatwa fedha kidogo kidogo kwa ajiri ya maendeleo ya Mikoa yao including kugharimia elimu za watoto wa wakulima maskini.

Wakulima wote wa cash crops nchini Tanzania wengeweza kabisa kuiga/jifunza kutoka kwenye mifano ya vyama vya ushirika vya Kilimanjaro na Kagera ili wajiletee maendeleo bila ya kutegemea saana Serikali, kwa bahati mbaya Serikali ilihamuru kuvunjwa kwa vyama vya ushirika kisiasa na kuwa telekeza wakulima katika lindi la maskini wa kutupwa kwa muda mrefu, juzi juzi hapa ndio nimeanza kuona Serikali inajitahidi kufufua vyama vya ushirika, lakini kasi ya ufufuaji bado ni ndogo sana.

Ninacho taka kusema hapa ni: Sio kweli kwamba mikoa iliyo kuwa inalima kahawa ndio ilikuwa inanufahika kimaendeleo, kinyume chake kama nilivyo sema tangu mwanzo kahawa ilikuwa inauzwa huko Ulaya kwenye minada ya Kahawa na fedha kwenda Serikalini, vyama vya Ushirika vinapewa fedha ndogo sana, siku wahi kuona Serikali ikisema itawapa kipa umbele cha maendeleo Mikoa inayo zalisha kahama kwa wingi, kama suala lingekuwa ni kwamba mikoa/miji yenye natural resources na cash crops nyingi ndio ipewe kipa umbele cha maendeleo mbona Shinyanga ingekuwa kama Ulaya kwa maneno mengine ndio ingekuwa inaongoza Nchini katika masuala ya maendeleo.

Tuwe wakweli hapa, Mikoa mingine inasahurika sana sana - mfano: Jaribu kutembelea mkoa wa Kagera, hivi sasa umerudi nyuma karibu kwa kila sekta,kusema kweli hali inatisha sana, mtu huwezi amini kama Mkoa huo ni part ya Tanzania, Serikali na wizara ya Kilimo wanazungumzia mazao mkakati sijui kilimo mkakati predominantely kwa ajili kanda ya kusini, kanda ya kati na Kigoma lakini sijawahi kusikia Wizara ya Kilimo au viongozi wa Mkoa wa Kagera wakizungumzia kuhusu kusambaza miche ya kisasa ya zao la michikichi Mkoani Kagera, wakati wazaliwa wa huko wanajua kwamba michikichi inastawi sana Mkoani, hipo mpaka migombani which means climate inakubali sana zao hilo.

Nakumbuka nilipo kuwa mdogo wakati wazazi wana lima mtama mwekundu kwa ajili ya kutengenezea pombe, sasa katika ukuuaji wa mtama palikuwa panajitokeza zao la ziada lenye maua mapana sana yanayo pendeza, sisi hatukujua hilo ni zao gani tulishia kuitana tu, jamani eeh (ija mulebe ebiua okwo byashemela) - yaani njoo muone maua yanavyo pendeza - kumbe zao lenyewe ni ALIZETI, ninacho taka kumaanisha hapa ni kwamba kumbe hata zao la Alizeti linakubali sana Mkoani Kagera - kwa nini mazao ya michikichi,Alizeti na kahawa hayapewi msisitizo kama misisitizo inayo wekwa kwenye Mikoa inayo lima Korosho na michikichi.
 
Mkuu, kitu amcho hukijui ni kwamba zao la Kahawa lilikuwa linanufahisha Taifa kwa jumla - kahawa inauzwa Ulaya na fedha kwenda hazina - wakulima wa kahawa kupitia vyama vyao vya ushirika ndio walikubaliana kwamba wanapo uza kahawa kwenye vyama vya ushirika wanakatwa fedha kidogo kwa ajiri ya maendeleo ya majimbo yao including kugharimia elimu za watoto wa wakulima - wakulima wote wa cash crops nchini Tanzania wengeweza kuiga mifano wa vyama vya ushirika vya Kilimanjaro na Kagera kujiletea maendeleo bila ya kutegemea saana Serikali, kwa bahati mbaya vyama vya Serikali ilihamuru kuvunjwa kwa vyama vya ushirika kisiasa na kuwa acha wakulima maskini wa kutupwa kwa muda mrefu, juzi juzi hapandio nimeanza kuona Serikali inajitahidi kufufua vyama vya ushirika kasi yenyewe naona bado ni ndogo sana.

Ninacho taka kusema hapa ni:sio kweli kwamba mikoa iliyo kuwa inalima kahawa ndio ilikuwa inanufahika, kinyume chake kama nilivyo sema kahawa ilikuwa inauzwa huko Ulaya jwenye minada ya Kahawa na fedha kwenda Serikalini vyama vya Ushirika vinapewa fedha ndogo sana, siku wahi kuona Serikali ikisema itawapa kipa umbele cha maendeleo Mikoa inayo zalisha kahama kwa wingi - jaribu kuyembelea mkoa wa Kagera hivi sasa umerudi nyuma karibu kwa kila kitu - hali inatisha sana huwezi kuamini kama Mkoa huo ni part ya Tanzania, hakuna anaye jari hata kidogo.
Hata madini ya Geita yaliuzwa SA na Ulaya lakini bodi yake ilikuwa Kilimanjaro!
 
Back
Top Bottom