Kwa sasa hapa nchini hakuna kiungo fundi wa mpira kumzidi Gerson Gwalala wa Coastal Union

Kwa sasa hapa nchini hakuna kiungo fundi wa mpira kumzidi Gerson Gwalala wa Coastal Union

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Anaitwa Greyson sijui Grayson Gwalala kiungo mkatashombo wa Coastal Union ya Tanga, jana amekuwa man of the match kwenye mechi dhidi ys Singida Big Stars yenye viungo wa kimataifa waliooonyesha ufundi wa hali ya juu wakati wa mechi dhidi ya Yanga, dogo huyu wala hastahili kukosa national team.

Huyu anamkaribia kwa mbaali kiungo fundi wa zamani wa Coastal Union akiitwa Ally Maumba ama Over the Top.

Enzi zile Coastal kipa alikuwa marehemu Hamis Makene kulia Said Kolongo, kushoto Douglas Mhani ama huyu kocha msaidizi wa sasa wa Coastal Joseph Lazaro, Nne Yassin Abuu Napil sentahafu marehemu Idrisa Ngulungu, sita alikuwa Ally Maumba Over the Top, Maumba kama hukupata fursa ya kumuona kiungo huyo basi maisha yako hapa duniani yamekuwa ya mikosi sana, winga enzi hizo Kassim Mwajeki, Winga Razack Yussuf Careca, Nane Kassa Mussa, Tisa Juma Mgunda Kumi Hussein Mwakuruzo.Aiseeeeeeeeeeeeeeeeeee.

Sasa huyu dogo kwa sasa ukiwaondoa akina Kevin Nashon, Kenny Mwambungu, Yussuf Kagoma, Mzamiru, Mtenje Albano Salum Abubakari, Jonas Mkude na Andambwile huyu Gwalala hastahili kukosa national team kwa mtu ambaye anaujua kweli mpira na ana uzalendo wa nchi hii, mnaita wachezaji national team lundo halafu hawachezi huku huyu dogo mnamuacha bila sababu za msingi, kocha yoyote anayehitaji mafanikio katika timu yake au nchi kwa ujumla hawezi kumuacha Gwalala nje, yaani unamuacha Gwalala unamchukua Himid Mao, upuuzi mtupu.

Viongozi wangu wa Simba huyu mtoto mtakuja kuniambia, huyu dogo amemzidi sana Kagoma, Mzamiru, Andambwile, Mkude, Mtenje, kwa sasa hakuna mido wa chini hapa nchini zaidi ya huyu Gwalala, mnataka ndivyo ilivyo hamtaki ndivyo ilivyo.
 
Back
Top Bottom