Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

20. Mineral processing engr
21. Bachelor of art with education
22. Fine art and design
23. Statistics
24.Mathematics
25.Physics
26. Civil engr
27. Chemistry
28. Agroeconomy
29. Biochemistry
30. French
31. Arabic
32.
33.
34.
Yupi ana degree ya mineral processing na hana ajira namtaka mm
 
Civil engineering haijatajwa hapo.

Haya hizo zingine (Maths, Physics, Chemistry) ajira zake zinapatikanaje kirahisi na kwa wingi?
Kumbuka kutofautisha degree ya Ualimu wa Maths/Physics/Chemistry na Degree ya Maths/Physics/Chemistry.
Ofisi ya mkemia mkuu wa serikali ilitangaza ajira nawaliopata wengi ni bachelor of science in chemistry, physics na biology
 
Hapa tunazingumzia Elimu ya chuo kikuu kwa level ya kuanzia degree wala sio umuhimu wa elimu moja kwa moja. Narudia tena, kwa sasa degree kwa 90% haina mchango wowote kwenye issue ya kupata ajira au kipato moja kwa moja. Ni kupoteza rasimali tu.
 


Kufanikiwa Kwa MTU huwa kuna hitaji uwe na malengo na sio aina ya degree au kazi.

Kila njia inatoka cha muhimu fata mwelekeo sahihi .

Mfano Kiswahili watu wanakidharau Ila ndo kimewapa watu maisha makubwa sana .

Hata ukiwa bodaboda ukiwa na malengo utafika mbali Sana MTU mweusi hana malengo na ndo uchawi wake ulipo.


Kuna Andiko naliandaa ambalo litasema kazi yoyote huwa ni kianzio cha mafanikio na sio mafaniko halisi
 
Mjumbe wewe ni mrongo tena mrongo mkubwa. Hii blablabla yoooote ni yako, yako wewe, speak for yourself. Nina jirani zangu wengi tuu hawajui IFM wala SUA, wala darasani hawajawahi kuingia kabisa. Siyo kwamba wanakubaliana na wewe kwamba kusoma hakuna faida bali ni kwamba hawajapata fursa. Wewe umepata fursa kwa kiasi fulani ndiyo maana wao wakakosa. Ukianza kuwatukana hivi hawatakuelewa. Enzi za Nyerere ungefungwa kwa uhaini. Huo ni uhaini.
 
Tunarudi pale pale.
Kwa sasa Degree pekee kwa 90% ya wahitimu haina mchango wowote wa kukupa ajira au kipato.

Kumbe mtaani watu wanataka connection na ujuzi mahususi ili utoboe kwenye ajira, sio degree yako.
 
Mtu unaenda Chuo kikuu Kweli eti unasoma Bachelor of History, Linguistic, Geography, Maths in general, Kiswahili...serious?

Yaani mtu unajitapa msomi huku una degree ya Kingereza?

Yaani hiyo ni lugha tu kwa ajili ya kujifunzia masomo mengine yaani mwenzio anajua Kingereza Ili akitumie kujifunzia masuala ya uandisi, madini, sheria, n.k Sasa wewe eti hiyo ndo Elimu yako!

Ebu walimu waelimisheni wanafunzi jmn!
 
Sawa mimi ni uhaini, vipi connection za ajira hapo ulipi zipo ili vijana waliohitimu degree wapate ajira? Kuna utiriri wa wahitimu wa UDSM, IFM, SUA, UDOM ninao mtaani wanasaka ajira mwaka tatu huu na hakuna dalili.
 
Haya maisha yana siri nyingi mno.

Sio kila .wanaume au mwanamke anaoa au kuolewa.

Sio kila anayefanya kazi kwa bidii anakuwa tajiri.

Hivyo sio kila anayesoma anapata ajira.

Lakini huwezi sema elimu haina umuhimu.

Bado ina umuhimu kwakua kuna ambao wamesoma na wamepata ajira na zimewanufaisha.
 
From your perspective!. Muktadha wa elimu ni kuntengeneza mtaalamu tu. Kipato na ajira ni sekta nyingine.

Muhasib na digrii akilipwa laki 3 sawa na hela anatoibgiza muuza MITUMBA ilala nani alaumiwe?. Juzi Kuna jamaa yangu kapata mchongo casual cleaner nje y nchi na mshahara katika mkataba unasoma kama laki 7 na 25 elfu. Huyu na digrii holder kwa muktadha wako atakuwa Bora sabab ya unachokieleza hapa


Elimu haijajiw kwa kigezo cha ajira, although elimu pia haitoi 100% guarantee ya kumbadili mtu kila kitu. Tabia nyingine msomi anazipata kwa sabab ya watu ANAOISHI NAO
 
Ajira na kipato havimilikiwa na mfumo wa elimu
 
Ndugu yangu, soma mada utanielewa.
Nimerudia kusema, kwa hali ilivyo sasa, kwa 90% ya wahitimu wa chuo kikuu wa level ya degree, hawajaweza kuajiriwa kwa degree zao na wala hawajaweza kutengeneza kipato cha kueleweka kutumia degree zao.

Sasa mtu alimaliza degree ya Political science miaka minne iliyopita, akasaka ajira kwa miaka mitatu bila mafanikio Dar, Dodoma na Mwanza, akatupa degree yake kabatini, ndugu wakamchangia mtaji wa milioni tatu akaenda zake huko Mbeya vijijini kujumuika na wanakijiji walioishia darasa la saba, wakamfundisha kulima mpunga, mwaka huu kavuna na kuuza mpunga gunia kama 20, vipi hapo Degree yake ya political science imemsaidiaje kutoboa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…