Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Kwa sasa huenda 90% ya Degree hazina tena maana, hazikupi ajira wala maarifa ya kupata kipato

Elimu ni uwekezaji mzuri sana tu.

Kama una fursa ya kusoma no vyema uitumie vizuri, usiache kwa kigezo kuwa kazi hakuna.

Halafu hiyo elimu pia inapanua ufahamu wako na inaweza kukusaidia pindi utakapoamua kujikita kwenye sekta zingine za uzalishaji.
Kabisa mkuu 🤝
 
Fani zipi ndo uhakika mkuu?
Maana tuna walim,famasia huku mtaani pia sijawaona hapo?
Changamoto ziko kada zote lakini kwa Afya na Elimu kuna auheni kubwa ya kupata Ajira ya uhakika serikalini, japokuwa kunahitaji subira ya wastani wa miaka 3-5 kabla ya mfumo kumpa muhitimu ajira. Na hiyo ndio inaingia kwenye hiyo 10% ya wanaobahatika kupata ajira baada ya kuhitimu.

Changamoto kubwa nayo iko hapa.
1. Mshahara sio mkubwa (ni wastani)
2. Mazingira ya kuanzia ajira huwa ni magumu na mapya.
 
Ukweli usemwe na usemwe wazi ili kila mtu aujue. Wigo wa watanzania kusoma mpaka chuo kikuu ili kupata degree umekuwa mkubwa lakini huo mfumo umekuwa ni hasara na upotevu wa rasimali (muda, pesa na nguvu) kwa 90%.

Ajira mtaani kwa 90% hakuna kwa fani nyingi, ni sawa na kucheza kamili, na elimu ya vyeti vya chuo kikuu haina mchango wowote wa mhitimu wa level ya degree kuweza kujiajiri moja kwa moja. Hapa chini ni baadhi ya fani zinazoangukia kwenye kundi hilo.

1. Public administration
2. Political science
3. Business administration
4. Procurement and supply
5. Human resource
6. Sociology
7. Environment
8. Language
9. Mass communication
10. Tourism
11. Banking
12. Accounting
13. Economy
14. Finance
15. History
16. Insurance
17. Tax
18. Cooperative
19. Marketing
20.

Kama wewe ni mhitimu wa hizo fani kwa miaka ya karibuni utaelewa hicho nilichokiandika, na kama wewe ni mwanafunzi wa hizo fani anza kujiandaa kisaikolojia, hali ni mbaya mtaani. Wahitimu ni wengi na hawana ajira yoyote, wamechoka vibaya, wameshazunguka na mabahasha mpaka soli za viatu kuchakaa, wamejitolea mpaka basi, wameshikiza mpaka wamedondoka na wengi wamekata tamaa kabisa, vyeti vyao wamesahau hata vipo wapi, havina msaada. Bado wanakula, kulala na kutunzwa na wazazi wao, mashemeji au wajomba. Wengine wameamua kujiajiri katika fani zingine ambazo hazina uhusiano wowote wa fani walizosomea na zenye kuhitaji elimu ya darasa la nne tu.
Wajanja wengine wameamua kurudi chuo, hususani kwa ngazi ya Diploma kusoma fani za ualimu au afya ili kuingia kwenye mkondo wa kuja kupata ajira hapo baadaye.

Jamani hali ni mbaya na tete.
Ukweli usemwe!
Ninaumia sana nikikumbuka jinsi nilivyokuwa nikiteseka usiku kucha ninasolve hesabu ngumu k.m Laplace transform, abstract algebra, topology, Fourier series, fluid mechanics,rigid body mechanics, advanced complex analysis, data structure, functional analysis e.t.c ili niweze kupata GPA nzuri na nikafanikiwa kuwa na 4.6 ambayo ni first class, lakini nimezunguka mpaka nikanyosha mikono huu ni mwaka wa 10. NINAUMIA SANA MOYONI MWANGU KWA NINI NILIPOTEZA MUDA KIASI HICHO KUHANGAIKIA KUSOMEA DEGREE HII YA .... AMBAYO NINATESEKA KIASI HIKI MTAANI. Hata hivyo Mungu ni mkuu siku Moja serikali watatukumbuka na tutapata ajira
 
Nimesema huhitaji kuwa na degree ili uweze kuzifanya hizo kazi za elimu ya darasa la Saba. Ukiona mtu mwenye degree anazifanya hizo kazi basi ujue degree yake imeshindwa kumpa ajira na kipato alichokitarajia, hivyo ameitupa kabatini na kuishi bila degree ili maisha yaende.
Kufanya hizo kazi zinazofanywa na wasio na elimu sio vibaya hata kidogo.

Ila kwa kuwa ni 'msomi' namna atavyozifanya hizo kazi kutakuwa Kuna utofauti na wale wengine, Kama mfano ni Kilimo au biashara huyu 'msomi' akichanganya hiyo shughuli yake na maarifa aliyonayo tegemea matokeo mazuri mno na endelevu kuliko asiye na elimu kabisa.
 
Nina 12 yrs kitaa mkuu!
Acha kabisa!
Kwanza nilishaachana kabisa na mambo ya kuomba kazi mie
Tunapambana kivingine
Ni kweli inaumiza mno..

Lakini maadamu umeshatafuta 'plan B' hiyo elimu yako haijapotea bure, ufahamu wako umepanuka mno na uwezo wako wa kufikiri ni mzuri.

Namna unavyotekeleza hiyo 'plan B' hata kama haihusiani kabisa na elimu uliyosomea haiwezi kuwa sawa na yule asiyekuwa na elimu kabisa.

Hata 'maarifa' tu ya kitaa namna ya kuendesha shughuli ndogo ndogo ni elimu pia japo sio elimu rasmi.
 
20. Mineral processing engr
21. Bachelor of art with education
22. Fine art and design
23. Statistics
24.Mathematics
25.Physics
26. Civil engr
27. Chemistry
28. Agroeconomy
29. Biochemistry
30. French
31. Arabic
32.
33.
34.
Itoe 22 hadi 29
 
20. Mineral processing engr
21. Bachelor of art with education
22. Fine art and design
23. Statistics
24.Mathematics
25.Physics
26. Civil engr
27. Chemistry
28. Agroeconomy
29. Biochemistry
30. French
31. Arabic
32.
33.
34.
economics,agro economy,civil
ajira zipo mazee.

sema nini,ajira ni bahati
 
Back
Top Bottom