Kwa sasa MIMBA ni hatari kuliko DHAMBI

Kwa sasa MIMBA ni hatari kuliko DHAMBI

Watu wana ajenda zao, ukisikiliza hayo matangazo yao, kwa mwenye akili unaishia kusikitika, ila tutafanyaje na wenye nguvu ndio madhalimu, pinga ukose misaada.

😂 😂 Tunacheka kama mazuri ila inasikitisha.
Kweli mkuu yote haya ni kuwa masikini tu
 
Mwanadada uliebahatika fursa ya kuwa na kizazi fyattttua! Kisawasawa! Watoto!, unamuogopa nani!? Unataka kumwachia nani hayo mayai kwani!? Na kijana mwenye mayai yakutosha, fyattttua! Watoto kisawasawa, mambo sijui ya malezi, mwachie Mungu! Na ustawi wa jamii!, Dunia inaenda kasi mno!
 
Ulimwengu wetu uko kasi sana, ukiangalia tulikotoka na tunakoelekea utashuhudia mwenyewe.
Kwa sasa kuna matangazo mengi sana ya jinsi ya kutumia uzazi wa mpango na matangazo elimu kwa vijana juu ya njia za kujikinga na kupata mimba.

Kwanini elimu hii isitolewe kwa wanandoa? Unamfundisha mtoto mambo ya uzazi kwani kuolewa? Kama hajaolewa elimu ya uzazi inamhusuje?
Jamii haioni kama itahamasisha ngono kabla ya ndoa? Kwanini jamii isitumie nguvu kufundisha madhara ya ngono kabla ya ndoa?.

Kamwe siwezi kuruhusu mtoto wangu atembelee vutuo vya aina hiyo badala yake anapaswa kujua kufanya ngono kabla ya ndoa ni dhambi na matokea ya dhambi hiyo ni mimba zisizotarajiwa, magonjwa ya zinaa,kuaibia kwa jamii n.k.

Shetani anapambana sana hachoki wala hakati tamaa. Tuwe makini sana
(2Timotheo 3:1-5)
Kabla ya dhambi ilianza tamaa na kabla ya tamaa kulikua na kishawishi na baadae tamaa ikakua ikashika mimba nayo mimba ilikua imetokana na dhambi na baada ya dhambi kinachofuata ni mauti

Nawasilisha..
 
Ndo maana vita, magonjwa, njaa na umaskini haviwezi kuisha kamwe, na kila siku matatizo yanaongezeka

Binadamu tumekuwa waovu sana, yaani kwa kizazi cha sasa sijui kama kuna mtu tena anakumbuka kufanya ngono ni dhambi, tena ni dhambi ambayo inamchukiza Mungu

Kidini wanasema ni dhambi ambayo unaifanya ndani ya mwili, na ndani ya mwili wako kuna hekalu la roho mtakatifu, hivyo unavyofanya dhambi hii unamfukuza roho mtakatifu ndo hapo mikosi, laana, magonjwa umaskini hukuandama maana hauna tena roho wa Mungu ndani yako ni upo upo tu umebeba mwili wenye nyama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa hapa nimeelewa chanzo cha umaskin wangu
 
Harafu mi kabla sijaanza ngono bahati kwangu ilikuwa ndogo na mikosi ilikuwa mingi sana. Ila nilipoanza tu hiyo dhambi kidogo nikaanza kuiona furaha ya maisha
 
Dunia ya sasa, watoto wa sasa, uwafundishe usiwafundishe wanazaliwa tayari wana experience zote...
 
Back
Top Bottom